Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Semua Post

MFANYA BIASHARA MAARUFU AJIUA KWA RISASI..!!

21:57
Mfanyabiashara huyo alikuwa akijishughulisha na biashara za maduka ya bidhaa za jumla na nyumba za kupangisha katika eneo la Karanga pia ni Mmiliki Serengeti Villa Bar and G house.



Tukio hilo lilithibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela.

Kamwela alisema lilitokea juzi majira ya saa 11 alfajiri na kuongeza kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa uchunguzi zaidi.


 Kamwela alisema mke wa marehemu, aliyetajwa kwa jina la Elizabeth Mallya, ndiye aliyebaini tukio la mumewe kujiua kwa kujipiga risasi moja kifuani akiwa sebuleni kwake, ambapo alitoa taarifa polisi.

Shemeji wa marehemu huyo, Peter Masawe alidai shemeji yake alijiua kwa kutumia bastola aina ya Browing yenye namba 96682, iliyokuwa na risasi nane na inadaiwa alikuwa akiimiliki kihalali.

Masawe alidai tukio hilo lilitokea siku moja kabla ya mfanyabiashara huyo hajatakiwa kusafiri kesho kwenda India, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya tumbo kwa muda mrefu.

“Kwa taarifa za familia hii, tunafahamu kwamba Malya hakuwa na ugomvi na mtu yeyote akiwamo mkewe na wanawe wanne,” alisema.

Alisema katika tukio hilo la kujipiga risasi, Mallya alifariki papo hapo akiwa nyumbani kwake na hakuna taarifa zaidi zilizotolewa juu ya chanzo cha tukio hilo.

Hata hivyo, Masawe alisema Mallya mara kadhaa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo, ambalo hujaa baada ya kumaliza kula.

Masawe alisema mipango ilikuwa imekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kufika siku ya safari.


Serikali ya Tanzania iko hatarini kukosa msaada wa dola za Marekani milioni 700

Serikali ya Tanzania iko hatarini kukosa msaada wa dola za Marekani milioni 700

20:54
Serikali ya Tanzania iko hatarini kukosa dola za Marekani milioni mia saba sawa na trilioni 1.1 kwa fedha za Tanzania kwa ajili ya mradi wa pili wa mfuko wa changamoto za Milenia (MCC) kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa nchini humo.
 Haya yanajiri wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo.
 Marekani imebainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.

 

Katika tamko hilo kwa umma ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa maamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL.
Taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.

Uamuzi huo wa Marekani ambayo inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha ni mtihani wa pili kwa Rais Kikwete baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.
Wanaotakiwa kuwajibishwa na Rais Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Novemba mwaka huu, Serikali ya Marekani kwa kupitia MCC, ilikubali kutoa ruzuku ya hadi Dola za Kimarekani milioni 9.78 kwa ajili ya maandalizi ya miradi ya uwekezaji yenye matokeo makubwa katika sekta ya nishati nchini.
Tanzania ilikuwa mojawapo ya nchi kumi zilizojadiliwa na Bodi ya MCC iliyokutana kuangalia kama nchi hizo zimekidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa kuandaa mikataba mipya.
Wakati wa mkutano wa 16 na 17 wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alidokeza kusudio la Marekani kukataa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya MCC, lakini Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alikanusha taarifa hizo.
Jaji akubali rufaa dhidi ya Pistorius

Jaji akubali rufaa dhidi ya Pistorius

02:49






Kiongozi wa mashitaka aliyewasilisha kesi ya rufaa dhidi ya Pistorius

Mahakama nchini Afrika Kusini imemruhusu kiongozi wa mashitaka kukata rufaa dhidi ya kosa alilopatikana nalo hatia Oscar Pistorius la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Kesi hio, sasa itaanza kusikiliza katika mahakama ya juu zaidi upande wa mashitaka ukitaka Pistorius ahukumiwe kwa kumuua mpenzi wake kwa kusudi.

Oscar Pistorius
Jaji Thokozile Masipa, alisema hataruhusu rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa ya miaka mitano dhidi ya Oscar mwezi Oktoba.
Kiongozi wa mashitaka Gerrie Nel aliambia mahakama kuwa hukumu hio ni ndogo sana ikilinganishwa na kosa la Oscar.




Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala amenukuliwa akisema "Nataka kuwa Waziri mkuu''

Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala amenukuliwa akisema "Nataka kuwa Waziri mkuu''

02:38





Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala Yousafzai raia wa Pakistani amesema kuwa siku zijazo anatarajia kuwa mwanasiasa.
Malala amesema ndoto yake hiyo anatarajia kuikamilisha baada ya kumaliza masomo yake na amesema ikiwezekana anapenda kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Binti huyo ambaye amekuwa akiendesha kampeni ya elimu dhidi ya wasichana alipigwa risasi na wapiganaji wa Talban miaka miwili iliyopita.
Mshindi huyo wa Nobel Malala yupo mjini Oslo ,Norway anatarajiwa kupokea Nishani anayoshirikiana na Bindi raia wa India Kailash Satyarthi





MSANII KULAZWA KWA KUKOSA KUNYWA MAJI SAFI NA SALAMA

MSANII KULAZWA KWA KUKOSA KUNYWA MAJI SAFI NA SALAMA

02:11





MSANII wa filamu na muziki wa taarabu Bongo, Upendo Mushi ‘Pendo’ yu kitandani baada ya kuugua ghafla kwa kile ambacho madaktari waligundua ni kunywa maji yasiyochemshwa.
Msanii wa filamu na muziki wa taarabu Bongo, Upendo Mushi ‘Pendo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, msanii huyo anayeishi Mwananyamala jijni Dar es Salaam, baada ya kupimwa na kukutwa na ugonjwa huo, alipatiwa matibabu na kurejea nyumbani ambako bado hali yake haijakaa sawa.
“Ni kweli, lakini nilishangaa sana madaktari walivyoniambia eti nilikunywa maji yasiyochemshwa wakati mimi siku zote nakunywa maji ya dukani, namshukuru Mungu lakini naendelea vizuri tofauti na nilivyopelekwa hospitali,” alisema Pendo baada ya kuulizwa kuhusu ishu hiyo





MAJANGA: FILE LA KESI INAYO MKABILI MAMA LWAKATALE LAIBIWA

MAJANGA: FILE LA KESI INAYO MKABILI MAMA LWAKATALE LAIBIWA

02:06





Sakata la Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude Rwakatare (pichani) kufunguliwa kesi ya uharibifu wa mali katika Kituo cha Polisi cha Wazo Hill, limechukua sura mpya baada ya faili la kesi hiyo kupotea katika mazingira ya kutatanisha, huku ikidaiwa kwamba limeibwa.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Assemblies of God jijini Dar, Dk. Getrude Rwakatare.

Kufuatia kudaiwa kuibwa kwa faili hilo lililopewa namba WH/RB/9029/ 2014, UHARIBIFU WA MALI, mlalamikaji, Grayson Justine Mghamba amemwandikia  barua mkuu wa upelelezi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni akilalamika kwamba anahisi kuna njama zinaendelea ili kumnyima haki yake.
 Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya Jeshi la Polisi, Kinondoni jijini Dar, zinadai kwamba Grayson alimwandikia barua mkuu huyo wa upelelezi Desemba 2, mwaka huu akiomba msaada kuhusu shitaka hilo aliloripoti polisi Novemba 20, 2014 akimtuhumu mama Rwakatare kumvunjia nyumba yake na kumpora kiwanja kilichopo eneo la Bunju B, Kinondoni.
 Sehemu ya barua hiyo ambayo Uwazi inayo nakala yake, inasomeka:
“Nasikitika kusema kuwa kila nifuatiliapo faili langu ili niweze kumjua mpelelezi wa kesi yangu, naambiwa kwamba halionekani wakati wao ndiyo waliniambia nifuatilie.”
Uwazi lilipomtafuta Grayson na kumuuliza kuhusu sakata hilo, alikiri kuandika barua hiyo na kusema kwamba amefuatilia zaidi ya siku tano kwenye Kituo cha Polisi cha Wazo Hill alikofungulia kesi hiyo lakini anaambiwa faili halionekani.
 “Nimejaribu kuwaambia kama hilo faili la kwanza limeibwa basi wafungue lingine lakini wamekataa,” alisema Grayson ambaye habari yake ya kuvunjiwa nyumba na mama Rwakatare iliripotiwa kwa mara ya kwanza na Gazeti la Uwazi wiki iliyopita ikiwa na kichwa cha habari: MAMA RWAKATARE AFIKISHWA POLISI.
Katika malalamiko yake, Grayson anadai kuvunjiwa nyumba yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 na mchungaji huyo, ambayo aliijenga kwa fedha alizochukua mkopo kazini kwake.
Grayson alidai kwamba nyumba yake hiyo ilivunjwa na greda kipindi alipoenda Moshi kwenye msiba wa baba yake na kiwanja chake anachodai kukinunua kihalali kwa kuandikishana na aliyemuuzia kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa wa Bunju B, kuzungushiwa ukuta.
Uwazi lilipomtafuta Mchungaji Rwakatare na kumhoji kuhusu sakata hilo, alisema kwamba kiwanja hicho ni mali yake tangu mwaka 2005 na alivunja nyumba hiyo kwa sababu alikuwa akikifanyia usafi kiwanja hicho alichodai kilivamiwa.




Mrembo akikatisha mitaani akiwa na bonge la kapelo

04:15









Umuhimu wa kushirikiana katika kazi hasa ya muziki

03:24










MTOTO ANYONGWA NA BABA WA KAMBO , FUATILIA KISA HAPA

MTOTO ANYONGWA NA BABA WA KAMBO , FUATILIA KISA HAPA

03:17







Baba mzazi wa marehemu (kushoto) akiwa na waombolezaji.
“Kaka yake alifika, vurugu kubwa ikazuka, baadhi ya vitu vilipotea na kuvunjika kutokana na purukushani hiyo. “Kulipokucha Hamis akaenda kuripoti ofisi ya serikali ya kijiji ambapo mgambo walifika nyumbani na kutuchukua hadi Kituo cha Polisi Mvomero ambapo baada ya kuhojiwa tuliamriwa tumlipe Hamis shilingi laki nne kufidia hasara iliyotokea nyumbani kwake, tulilipa nusu hadi sasa tunadaiwa iliyobaki.
” UGOMVI SIKU YA TUKIO “Novemba 28, mwaka huu, siku mbili kabla ya mauaji ulizuka ugomvi tena kati yangu na Zamili  akipinga kulipa lile deni. Jumamosi tuligomba tena, alikuwa akilalamika kwamba Hamis anamlipisha fedha wakati anamtunzia mwanaye, nikamwambia kama anakereka kumtunza mwanangu anipe talaka, akagoma akidai bado ananipenda.

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Zamili Shabani kwa madai ya kumnyonga hadi kumuua mtoto wake wa kambo, (mwaka mmoja na nusu) huku mauaji hayo yakihusishwa na wivu wa mapenzi. 
Abdulrahman Hamis Clemensi enzi za uhai wake.
Tukio hilo la ajabu lililowaacha vinywa wazi wakazi wa eneo hilo lilijiri saa 6 mchana wa Desemba 2, mwaka huu kwenye nyumba waliopanga wanandoa hao, Zamili na mkewe, Rehema Mustafa (21) iliyopo Kijiji cha Mbogo, Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani hapa.
ALIVYOSEMA SHUHUDA Kabla ya kuzungumza na mama wa marehemu, Uwazi lilipata mawili-matatu kutoka kwa shuhuda mmoja wa tukio hilo. ”Mimi moja kwa moja namlaumu mama wa mtoto, Bi. Rehema. Awali alikuwa kwenye ndoa na mumewe Hamis, wakabahatika kumzaa Abdulrahman.
“Mwanzoni mwa mwaka huu alifika Zamili akitokea Zanzibar. Kwa taarifa tulizonazo Zamili alikuwa na ishu kubwa kule  ndiyo maana akaamua kuja huku. “Unajua vijijini, mtu akitokea mjini wanawake wanamshobokea. Dada yetu Rehema akadanganywa na Zamili akatoka kwenye ndoa yake na kuolewa naye mwezi wa saba mwaka huu.
Rehema Mustafa mama mzazi wa mtoto Abdulrahman Hamis Clemensi.
“Toka waoane kila siku ni ugomvi hadi juzi yalipotokea mauaji hayo,” alidai Said Seleman Kindu, mkazi wa kijiji hicho.   MAMA WA MTOTO SASA Baada ya kuzungumza na Said, Uwazi lilimhoji Rehema ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Awali nilifunga ndoa na Hamis Clemensi, tukabahatika kumzaa mtoto mmoja ambaye ni huyo marehemu.
Baada ya kuachana na Hamis nilikaa nyumbani miezi mitatu, nikaja kufunga ndoa na Zamili, Julai 28, mwaka huu. “Tukio zima nahisi kama lilianzia Agosti,  mwaka huu kwani nakumbuka siku moja nikiwa sokoni nilikutana na Hamis akamsalimia mwanaye, kumbe kuna mtu alituona akaenda kumwambia Zamili.
“Aliporudi usiku tuligombana sana akitaka nimpeleke mtoto kwa baba yake, nikamwambia mwanangu bado ananyonya siwezi kumpeleka kama vipi asubiri atimize miaka mitatu nitampeleka hata kwa mama yangu mzazi.
“Licha ya kumwambia hivyo, Zamili akagoma, nikamwambia basi anipe talaka nirudi kwetu pia akakataa.”  “Siku iliyofuata, usiku alichukua kisu na kuniamuru nimpeleke mtoto kwa baba’ke,  tukatoka mimi, yeye na mtoto, lakini baba yake alipotuona alijificha juu ya dari huku akimpigia simu kaka yake anaitwa Kilimo na kumjulisha.

Hata hivyo, aliahidi kwamba atafanya mauaji.” SIKU YA TUKIO “Siku ya tukio Jumanne, saa 5 asubuhi, Zamili alinituma dukani, nikataka kwenda na mwanangu, akasema nimwache atanichelewesha, nikamwacha. “Niliporudi sikumuona mtoto, nikamuuliza Zamili mtoto yuko wapi? Akanijibu  kalala, nikaingia jikoni na kusonga ugali, tukala.
“Tulipomaliza, mimi nikaenda chumbani kumwamsha mwanangu ili naye ale. Nilishangaa kumuona kalegea. Kwa utoto wangu sikujua kama amekufa, nikaenda kuita wakubwa walipofika wakamuona mtoto kichwa kimegeukia mgongoni, wakaniambia mbona amekufa! “Palepale nikaangua kilio, watu wakajaa, baadaye viongozi wa kijiji wakaja na mgambo wakamkamata Zamili na kumpeleka polisi na mimi nikakodi bodaboda, nikabeba maiti ya mwanangu kuja hapa Mkindo kwa wazazi wangu.

Waombolezaji wakiwa msibani.
Mwanangu tumemzika jana (Alhamisi iliyopita),_nimebaki na kumbukumbu ya picha tu,” (akaanza kulia). Rehama alipotakiwa kutoa picha ya Zamili alisema: ”Huyu Zamili hana picha, hata kwenye harusi yetu aligoma kupigwa picha, nadhani alikuwa akitafutwa kule Zanzibar.
Alipoulizwa kama atakuwa tayari kuishi tena na Zamili, alisema: “Siko tayari mimi nataka talaka yangu.” BABA WA DAMU WA MAREHEMU Naye baba mzazi wa marehemu, Hamis Clemensi ambaye alikuwepo kwenye msiba huo wa mwanaye alipohojiwa na Uwazi alisema:  “Huyu jamaa ni wakuja, tulipata taarifa zake kwamba hakuwa mtu mzuri kule Zanzibar.
Alishataka kuniua mimi baada ya kunivamia kwangu usiku akiwa na mke wangu  na mtoto, eti amemleta mtoto wangu, nikapanda kwenye dari na kumpigia simu kaka yangu. Nasikitika kwa kumuua mwanangu.”





AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI

03:08











Cursed Generation, See how these woman is spurted

03:06









Hot woman of the day !!! Look at these cute pics

Hot woman of the day !!! Look at these cute pics

03:04











Ona kilichotokea baada ya mwanamke huyu kuamka mapema asubuhi

03:02




                            

Some ladies just know how to shake it, the lady in the video below is one of them and she has been giving men sleepless nights with her s3ductive dance moves. This video has been online for quite some time but men keep asking for more. See her doing it; *The LINK>>>>* *The Kenyan DAILY POST*





VIJANA WAMVAA  MIZENGO PINDA

VIJANA WAMVAA MIZENGO PINDA

02:04







BARAZA la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), limeitaka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa (Tamisemi), kutoa majibu ya haraka juu ya kuenguliwa kwa wagombea wa chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BAVICHA, Julius Mwita, alisema kuwa wagombea wa chama chao wameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho kwa sababu zisizokuwa za kimsingi.
Alifafanua kuwa, hizo ni mbinu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kutumia viongozi walioko madarakani kutaka kuwapitisha wagombea wao ili kuwasaidia katika uchaguzi mkuu ujao.
“BAVICHA hatuko tayari kuona uonevu wa kiasi hiki tunaufumbia macho, tunamtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutoa majibu ya haraka kuhusiana na hili kabla ya siku ya uchaguzi,” alisema Mwita.
Alitaja baadhi ya maeneo aliyopata taarifa kuwa Kamati ya Rufaa imewaengua wagombea wao ni Same, Vunjo, Njombe, Simanjiro na Mwanza.
Aliongeza kuwa, kuna baadhi ya maeneo ambayo wabunge wa CCM wanawalazimisha wakurugenzi wawaengue wagombea wa CHADEMA.
Akizungumzia miaka 53 ya Uhuru wa Tanganyika, Mwita aliwataka vijana kuadhimisha kwa kutafakari hali yao kimaisha, kwani Watanzania walio wengi bado ni masikini, hivyo ni wakati wa kufanya mabadiliko kuanzia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
“Kesho ni sikukuu ya uhuru wa Tanganyika, ni wakati muafaka wa kuangalia je ndani ya miaka 53 tumeweza kupigana na adui umasikini, ujinga na maradhi huku jingine limeongezeka rushwa, hivyo basi ni wakati muafaka kwa Watanzania kufanya mabadiliko kuanzia ngazi ya kata,” alisema.





ANUSURIKA KIFO , NI BAADA YA KICHWA CHAKE KUCHIMBWA A SULULU

01:17




HAKUNA neno jingine la kutumia zaidi ya kusema; KWELI MUNGU MKUBWA! Ni miezi mitano sasa imekatika tangu kusambaa kwa picha mitandaoni zilizomwonesha mwanaume mmoja akiwa ameshindiliwa sululu kichwani huku kisa kikiwa hakijulikani.


“Kwanza kabisa napenda kusema kweli Mungu ni mkubwa, nimepona! Ingawa mwili bado hauna nguvu sawasawa lakini naendelea vizuri. “Ilikuwa tarehe 19, Julai mwaka 2013  katika machimbo ya Mgodi wa Miombo- Rwamgasa  wilayani Geita, mimi ni fundi wa kuchimba maduara yanayotumika kuchimbia dhahabu.
“Baada ya kumaliza kazi zangu majira ya jioni, nikaenda kupumzika ili kujiandaa kwa siku iliyofuata. “Nilikuwa nimepumzika na wenzangu zaidi ya mia moja, unajua tena migodini. Kufika saa 3 hivi usiku nikiwa nimeanza kusinziasinzia, nilishtukia kitu kizito kinaingia kichwani mwangu upande  wa kushoto.” ALISHINDWA KUPIGA KELELE “Nilishindwa kupiga kelele nadhani kwa sababu ya kule kusinzia. Wenzangu ambao nao walianza kulala walishtuka kwa kusikia harufu ya damu, wakaamka na kuja wakanikuta sululu ikiwa imezama kichwani.

Oka Kaombe kabla ya kufanyiwa upasuaji.
“Hii sululu kule machimbo ni maarufu kwa jina la Moko, hutumika kuchimbia madini katika migodi. Nilichukuliwa na sululu yangu kichwani na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza  kwa ajili ya matibabu ya haraka.” SIKU NNE BILA FAHAMU Oka anazidi kusimulia: “Mengine ninayosimulia niliambiwa kwani nilipoteza fahamu kwa siku nne.
Nilianza kujitambua baada ya siku nne nikiwa palepale Bugando na kujikuta nipo hospitali lakini nilikuwa siwezi kuzungumza wala kusikia vizuri. Maumivu yalikuwa makali sana kutokana na sululu kuzama kichwani maana ilipoingia ilikwenda kutokea upande wa pili wa kichwa. “Nikiwa nimeshafanyiwa upasuaji kwa kuchomolewa sululu, niliendelea kukaa Bugando kwa siku 52.”
ATOROKA BUGANDO, AMSAKA MBAYA WAKE Oka alisema kuwa, hiyo siku ya 52 aliamua kutoroka hospitalini hapo kwa sababu alishindwa kulipia gharama za matibabu ambazo ni shilingi laki tisa (900,000). “Kiasi hicho cha pesa kwangu kilikuwa kikubwa na hata sasa bado ni kikubwa ndiyo maana niliamua kutoroka,’’ alisema Oka. ALIYEMZAMISHA SULULU AJULIKANA Oka anaendelea kusimulia:
“Nilipotoka hospitalini kitu cha kwanza nilianza kumtafuta mtu aliyenifanyia kitendo kile cha kinyama, marafiki zangu wakanipa ushirikiano  na kuniambia unyama ule ulifanywa na jamaa mmoja anayeitwa  Masha. “Huyu Masha ni mchimbaji wa madini kwenye ule mgodi lakini alikimbia baada ya kufanya tukio na mpaka sasa hajulikani alipo.”
KISA CHA KUPIGWA SULULU PIA CHAJULIKANA Oka alisema taarifa alizopata baadaye kutoka kwa wachimbaji mgodini hapo ni kwamba,  lengo la Masha kumpiga na sululu lilikuwa ni kumtoa kafara (ndagu) ili aweze kupata dhahabu nyingi na awe bilionea kwa siku za usoni. “Ila Mungu ni mkubwa alitupilia mbali wazo hilo mpaka sasa niko hai,” alisema Oka.
AFYA YAKE KWA SASA Oka alisema kwa sasa anaamini amepona kabisa kidonda chake kichwani ila hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na mwili kukosa nguvu za kutosha.
UPASUAJI MWINGINE Aliendelea kusema kuwa, akiwa Bugando aliambiwa na madaktari kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine na kuwekewa vyuma kichwani baada ya kuwekewa vyuma hivyo itabidi akae miaka mitatu bila kufanya kazi yoyote ndipo atapata nguvu za kufanya kazi kama zamani.
MAISHA YAKE KWA SASA Oka alisema maisha yake kwa sasa ni magumu kwani ana watoto 5, lakini pia alitengana na mke wake hivyo yeye ndiye baba na mama wa familia kwani hata wazazi wake wamezeeka, hivyo wanamtegemea yeye. ANACHOWAOMBA WATANZANIA Alisema kwa sababu bado ana safari ya kujitibu na pia kutunza familia, amewaomba Watanzania wenye kuguswa na mkasa wake wamsaidie pesa kwa kiasi chochote atakachojaliwa mtu kwa kutumia simu yake ya mkononi ambayo ni 0682 013479. 





HAUSIGELI NUSURA AUAWE..SOMA HAPA YALIYOMKUTA....

HAUSIGELI NUSURA AUAWE..SOMA HAPA YALIYOMKUTA....

00:24
Msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli), Rehema Ally (17), mkazi wa Yombo, Machimbo Mwisho, Ilala jijini Dar, amechanwachanwa kwa wembe na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyosababisha alazwe katika Hospitali ya Amana kwa matibabu.

 http://api.ning.com/files/3pbaBKayUO8h4-zaVFwJTaPlJbecBMjC3mKeeNh*DFQnxOKGVHw1jULmAFIWrXz481-unOB*EnC5QHw6tZM-iQSdYybhxmPb/IMG_1608.JPG
 Rehema Ally akiwa na majeraha mwilini mwake baada ya kujeruhiwa.

Akizungumza na Uwazi nyumbani kwa mwajiri wake aliyejulikana kwa jina moja la Ghati, Yombo jijini Dar, Rehema aliyefika jijini hapa Januari, 2013 akitokea nyumbani kwao, Masasi mkoani Mtwara, alikuwa na haya ya kusema:
“Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni Jumapili ya Novemba 30, saa moja usiku nikiwa nje ya nyumba ya bosi wangu. Akatokea msichana mmoja aitwaye Fatuma na mwenzake aitwaye Ashura huku wakiwa wamebeba kisu na wembe. Wakanikamata kwa nguvu na kunikaba, wakaniangusha chini na kuanza kunichanachana mwili mzima.
“Wakati huo nilikuwa naelekea nyumbani kwa akina Fatuma kuchukua sanduku langu ambalo alilichukua kwa bosi wangu akidai kwamba nimempotezea ‘memori kadi’ ya simu yake hivyo alisema kwamba mpaka nitakapomrudishia ndipo nitakapochukua sanduku langu.

“Walinijeruhi sana na kukimbia, nikarudi ndani lakini bosi wangu hakuwepo nyumbani na aliporudi alinichukua na kunipeleka polisi, tukapewa kibali cha matibabu (PF3) na kwenda Hospitali ya Amana kutibiwa. Tulirudi nyumbani na baadaye tukafuatilia kesi yetu polisi, wakasema turudi nyumbani tukaelewane mbele ya mjumbe ili kesi imalizike.
“Tulienda kwa mjumbe pamoja na Fatuma na wazazi wake na mimi nilikuwa na bosi wangu, wakataka kesi imalizike yaani tusameheane lakini kwa upande wa wazazi wangu waliopo Masasi, nilipowapa taarifa walikataa kumaliza kesi kienyeji na kutaka ifike mahakamani kwa vile watuhumiwa walikuja na silaha na walidhamiria kuniua,” alisema Rehema.
Kwa upande wa mtuhumiwa, Fatuma Zuberi (17), alipoulizwa na waandishi wetu, alidai kwamba wakiwa njiani na mdogo wake wakienda dukani kununua vocha, walivamiwa na Rehema na kushambuliwa akitaka wamrudishie sanduku lake.
Naye mama mzazi wa Fatuma aliyejitambulisha kwa jina la Sharifa Mwinyi Kondo, alidai kwamba mwanaye pia amejeruhiwa hivyo waliamua mambo yote yaishe kwa kusameheana mbele ya mjumbe wao. Mjumbe wa shina namba 22, Rose Kiravu alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alikiri kupokea taarifa hizo na kudai kwamba suala hilo lilifika polisi lakini lilirudishwa kwake kwa upatanishi ambapo alikaa na pande zote mbili pia wajumbe wa nyumba kumi wawili na wote waliamua kusameheana.

Kijue kikombe cha umeme chenye uwezo wa kukuonyesha kama una kiu..na kupima aina ya kinywaji unachokunywa..!!

Kijue kikombe cha umeme chenye uwezo wa kukuonyesha kama una kiu..na kupima aina ya kinywaji unachokunywa..!!

23:34
Watengezaji wa kikombe hiki wanakiita Vessly, kitaanza kuuzwa mwakani na kitapatikana kwa kiasi cha dola 99 tu.

 cup 
Haya ndiyo maendeleo ya kiteknolojia ambapo unaambiwa hiki kikombe kina uwezo wa kupima cafeine kutoka iliyopo kwenye kinywaji unachokunywa, pamoja na kitu kingine chochote ambacho kimo ndani ya kinywaji hicho hata kama ni kilevi, iwapo ukanywa halafu ukashusha kikombe chini na una kiu bado kinakupa ishara kwamba unatakiwa unywe tena kinyaji unachokunywa.
Kikombe hicho kinatumia app maalum ambapo unaweza kukifanyia sync kupitia Bluetooth, iPhone Operating System na Android app, unaweza kukichaji kwa Wireless, kina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa siku tano mpaka siku saba na kinaweza kuingia chupa moja ya soda ya kawaida.

HIVI NDIVYO IRINE UWOYA ALIVYO UPAMBA UKURASA WAKE WA VIBE.COM, NI SHEEDAH TAZAMA PICHA HIZI(18+)

01:10






Jarida  la  maswala ya burudani, liitwalo Vibe Tz  lililotoka hivi karibuni,limepambwa kwa picha za muigizaji  wa filamu hapa Bongo, Irene Uwoya amabe ni mrembo aliebarikiwa suru na umbo matata bila kusahau rangi yake,kitu ambacho huwafanya vidume wengi kupagawa na kuwa na mashabiki wengi wa kazi zake mbali nakipaji chake katika sanaa.

Japokuwa kuwa kwasasa ni mama wa mtoto mmoja , Uwoya amefanya kile kinaitwa siku hizi –KU-BREAK THE INTERNET, kwenye picha alizopigwa na jarida hilo.
Irene ametokelezea kwenye kurasa za mbele  yani “Cover Pages” akiwa mavalia mavazi ya ufukweni za rangi nyeusi na nyeupe, moja akiwa anatazama mbele na nyingine akitupa mgongo. Vivazi hivyo vimefanya sehemu kubwa ya mwili wake kuonekana na watu kuweza kujionea uumbaji wa alieviumba. Pia picha zingine zimeonekana kwenye kurasa za kati za jarida hilo akiwa katikati mapozi tofauti tofauti. Hakika Bidada AMETULIA…







Starehe kwanza , mengine baadae by Tamrina

01:04





https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjbKmGZXolVFE9fxhOI5u44V6XNqoPDQridK9CKBF4MyEHHwrRqwwLwgHGg1AUllqFU6u_rogOyHHAxVkzeOM0uCN_PJJHCTbHBK7gZcVBG1kQnjwxPrQSD69n2FqKYqz7ABfTSAu360FM/s1600/199451_356859541067694_913345479_n.jpg “Jamani niacheni na mavazi yangu, ukifika muda nitarejea naona mnanisema sana, kama wewe Mungu amekujalia kusali, mshukuru mimi muda huo bado haujafika,” alisema Amanda ambaye wakati huo alikuwa ametupia kivazi kilichomuacha wazi sehemu kubwa ya mwili wake hasa tumboni.








Pingamizi la Quick Rocka

Pingamizi la Quick Rocka

00:56







Quick Rocka amekanusha kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu, Kajala Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM, Quick amesema ana girlfriend hivyo uvumi huo unaweza ukamharibia uhusiano wake.“Nasema hapana Kajala mimi sister yangu, tunafanya naye kazi na nimeunganishwa na Lamata. Lamata ni director ninayemmfahamu zamani kidogo kipindi kile tunafanya ‘Mbwa Mwitu’ tulikuwa wote, Lamatah, Hemedy! Unajua mnavyofanya movie ni tofauti na kufanya video, kwa mfano wakati tunafanya ile movie ya Wolper, tulikaa Magomeni kambini ili kujenga chemistry. Unajua mnapoigiza kuna vitu lazima viendane. Sisi ni kambi moja inabidi mchongo tuufanikishe,” alisema rapper huyo. “I have a girlfriend, anavyosikia hivi vitu mimi kwa upande mmoja inaniharibia na sijui yeye pia ana mtu wake huko kwahiyo tuna wazazi, tuna watu wetu wa karibu ambao wanatuangalia, watu ambao wametupenda na wametuamini hivyo halafu wakija kusikia mambo haya kwenye media wataona kumbe huwa hamfanyi kazi, wao wanachukulia serious. Sio vitu vya kweli.





Fumanizi, kaka mutu kuendesha kesi

Fumanizi, kaka mutu kuendesha kesi

00:54





Kaka mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Nicholaus kwa kushirikiana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, amesimamia fumanizi la dada’ke ambaye ni denti wa sekondari moja jijini Dar (majina yanahifadhiwa kwa sababu maalum) ambapo alimfumania chumbani na njemba mmoja sharobaro aliyetajwa kwa jina la Abuu Ally, mkazi wa Mbagala-Charambe, Dar.
Njemba sharobaro, Abuu Ally akiwa na denti baada ya fumanizi.
OFM ikiwa kazini, ilipokea malalamiko kutoka kwa Nicholaus aliyedai kwamba amekuwa akiumizwa na taarifa kwamba kila ikifika saa 2: 00 usiku kuna mwanaume amekuwa akijipenyeza na kuingia chumbani kulala na mdogo wake wa kike kisha kuchomoka alfajiri.
Kaka mtu wa denti huyo akimwajibisha Sharobaro(mwenye boksa).
Nicholaus alisema kuwa mara nyingi vitendo hivyo hufanyika wikiendi ambapo katika kuhangaika kumnasa anayemharibu mdogo wake aliwataarifu OFM ambao waliingia mzigoni na kuweka mtego uliomnasa sharobaro huyo.
Sharo yaani Abuu Ally akijikomiti kulipa faini kwa kosa la kulala na dada wa mtu.
OFM hawakuwa wenyewe kwani walimtaarifu Mjumbe wa Mtaa wa Maji-Matitu, Hawa Ally kuwa wana kazi eneo lake hivyo akatoa ushirikiano uliofanikisha kumnasa Abuu.
Ama kweli za mwizi arobaini! Saa 5:11 usiku, jamaa huyo aliingia chumbani kwa denti huyo na kuanza makeke yake akimfanyia binti huyo mavituzi.
Waraka wa kujikomiti wa Sharo alioundika mbele ya mjumbe, Hawa Ally.
OFM walisubiri kwa muda wa robo saa kisha wakaingia ndani ya nyumba hiyo kwa msaada wa wapangaji na kumnasua binti huyo ili aendelee na masomo.Sharobaro huyo alikiri kuingia mara kadhaa ndani humo na kubanjuka na denti huyo.
Baada ya kukiri kosa mbele ya kiongozi huyo wa serikali za mtaa, pande zote zilikubali kusuluhishwa ambapo Abuu alikubali kulipa faini ya shilingi laki moja na kupewa muda wa siku moja kutekeleza adhabu hiyo.








Watu waliokuwa na silaha wamevamia gereza katika mji wa Minna, katikati mwa Nigeria, na kuwaachilia huru wafungwa 200.

Watu waliokuwa na silaha wamevamia gereza katika mji wa Minna, katikati mwa Nigeria, na kuwaachilia huru wafungwa 200.

00:48





http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/304/amz/worldservice/live/assets/images/2014/11/06/141106113053_boko_haram_nigeria_prison_304x171_.jpg
Walingia kwa nguvu kwenye jela Jumamosi katika jimbo la Niger.
Polisi wanasema haijulikani ikiwa uvamizi huo ulifanywa na kundi la wapiganaji Waislamu, Boko Haram, au gengi la wahalifu.
Boko Haram wamevamia magereza kadha katika miaka ya karibuni.





Umoja wa mataifa kuzindua msaada wa kimataifa leo hii.

Umoja wa mataifa kuzindua msaada wa kimataifa leo hii.

00:45






Ombi hilo ni la kila mwaka na hulenga kupata fedha za kukabiliana na madhara ya vita na mizozo ya kibinadamu duniani kote.
Kadhalika ombi hilo linajiri wakati mashirika ya misaada yanaonya kuwa yameishiwa na fedha za kukimu oparesheni za mwaka huu.
Wiki iliyopita, shirika la mpango wa chakula duniani lilitangaza kuwa limelazimika kupunguza msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Syria.
Mwaka mmoja uliopita, Umoja wa mataifa uliomba dola bilioni 13 za Marekani, kwa utoaji misaada duniani - nchini Syria, Sudan Kusini, au Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Lakini hiyo ilikuwa kabla ya mgogoro uliojiri Ukraine, kabla ya kuzuka kwa kundi la Islamic State Iraq, na kabla ya janga la Ebola. Dola bilioni 13 hazikutosha - na pesa hizo hazikutolewa kikamilifu na nchi wafadhili.
Na sasa unapojaribu kukabiliana na mahitaji ya mwaka huu, mashirika ya misaada ya umoja huo, yataomba fedha za miezi 12 ijayo. Chakula na vifaa vya matibabu kwa wakimbizi vinafaa kununuliwa mapema, hospitali zinahitajika na zinafaa kujengwa.
Misaada ya kibinadamu haipatikani mara moja, mashirika ya misaada yanahitaji kupanga, lakini ili kufanya hivyo, yanahitaji fedha.
Ombi la mwaka 2015 litadhihirisha mizozo mingi iliopo duniani na changamoto kubwa zinazoyakabili mashirika ya umoja huo yakijaribu kuwasaidia wale waliokumbwa na migogoro hiyo.





Ni aibu, mbunge anaswa akicheza game kikaoni

Ni aibu, mbunge anaswa akicheza game kikaoni

00:41





 http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2014/12/08/141208081111_candy_crash_512x288_bbc_nocredit.jpg
Mbunge wa chama tawala cha Conservative nchini Uingereza , amekiri kucheza mchezo maarufu kwenye tabiti yake wakati wa kikao cha kamati moja la bunge hilo.
Jarida la The Sun, limechapisha picha za mbunge huyo kwa jina Nigel Mills akicheza Candy Crush Saga kwenye tabiti yake, wakati wa mkutano wa kamati hio kuhusu mageuzi ya sera ya serikali kuhusu malipo ya uzeeni.
Jarida hilo linasema Bwana Nigel alicheza mchezo huo kwa zaidi ya saa mbili.
Hata hivyo amejitetea akisema alifahamu kilichokuwa kinaendelea katika kamati hiyo na kwamba lihusika katika kuuliza maswali. Hata hivyo alikiri kucheza mara mbili na kusema atajaribu kujizuia kucheza mchezo huo katika siku za usoni akiwa kazini.





Mwanasheria mkuu wa serikali nchini Mexico, Jesus Murillo Karam,ametoa ahadi kuwa hakutakuwa na uonevu wowote katika kesi ya kupotea kwa wanafunzi nchi humo miezi miwili iliyopita

Mwanasheria mkuu wa serikali nchini Mexico, Jesus Murillo Karam,ametoa ahadi kuwa hakutakuwa na uonevu wowote katika kesi ya kupotea kwa wanafunzi nchi humo miezi miwili iliyopita

00:39












.
Kutoweka kwa wanafunzi hao kumesababisha maandamano ya wiki kadhaa nchini humo waandamanaji wakipinda rushwa na ukatili uliozunguuka kesi hiyo.
Bwana Karam amesema kwamba uchunguzi wa kusaka walikopotelea wanafunzi hao unaendelea mpaka hapo wahusika wa tukio hilo watakapokamatwa.
Zaidi ya hayo amethibitisha mwili wa mmoja kati ya wanafunzi hao arobaini na tatu kuwa umetambuliwa kuwa ni wa Alexander Mora,mwili uliogunduliwa katika jaa la taka katika jimbo la Guerrero.
Mwanasheria mkuu huyo wachunguzi mahiri wa miili kutoka nchini Austria wakiunganisha mifupa kwa kuifananisha na kipimo cha vinasaba vya ndugu wa marehemu huyo9,ndipo walipoutambua.





Former Youth Fund CEO, Evans Gor Semalang’o, Look at these cute pics.

00:36






Former Youth Fund CEO, Evans Gor Semalang’o, claims that former Prime Minister Raila Odinga may have gone mad after he said that he had given Luo Elders 3 days to decide whether he will contest for the Homabay Senate seat in the forth-coming by-election. Gor claims that Raila will taint his image and lose his huge political following if he joins the race to succeed the late Otieno Kajwang. Below is what he had to say via social media ; *The Kenyan DAILY POST*





Bibi huyu adhihirisha kauli ile ya Uhuru Kenyatta kwamba usalama uanza na wewe.Ona alicho kifanya hapa

00:35











Ona kilichotokea kwa jimama hili kipindi lina jaribu kucheza jirani na swimming pool.Noii huko Kenya mida ya jana jioni

00:30





 
 





Maneno ya kizalendo ya Diamond platnum "There is no place like Home... Ever!

00:27






Japokuwa nina show Canada tareh 2 lakini ilinibidi kwanza nilete Mzigo
nlioagizwa na Wananchi Nyumbani kisha ndio nirudi kuendelea na shughuri zangu!... Kama wasemavyo
"There is no place like Home... Ever!"






Nyota ya Diamond yazidi kungara ,apokea tuzo nyingine huko Lagos Nigeria

Nyota ya Diamond yazidi kungara ,apokea tuzo nyingine huko Lagos Nigeria

00:24






tuzo
Diamond Platnumz ameshinda tuzo nyingine ambayo hizi zilikua zikitolewa Lagos nchini Nigeria ambazo hizi hazikuwa na utaratibu kama wa tuzo zingine kwa kupiga kura.

Baada ya kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kupokelewa na Meneja wake Salaam,Diamond alipost maneno haya>>’Thanks God,we have cheated another one on the future Awards Africa in Lagos Nigeria…#samenight Thank you Allah’
Tuzo hizi zinaitwa The Future Awards Prize in Entertainment ambapo kipengele alichokuwa akiwania Diamond alikuwa na wakali mbalimbali akiwemo Panshack au Ice Prince jina lake la zamani wa Nigeria na Michael Kwesi wa Ghana.




Kafulila ampendekeza Dk.slaa kuwa mgombea urais UKAWA, Gazeti la mwananchi leo juma tatu

Kafulila ampendekeza Dk.slaa kuwa mgombea urais UKAWA, Gazeti la mwananchi leo juma tatu

00:20










EXTRAVAGANZA: IDRIS SULTAN MSHINDI BIG BROTHER AFRICA-HOTSHOT

EXTRAVAGANZA: IDRIS SULTAN MSHINDI BIG BROTHER AFRICA-HOTSHOT

12:04
Hatimaye Mshiriki wa Big Brother Africa kutoka Tanzania aibuka kidedea.

 photo idristayowin_zpsa1003304.png

Ni furaha ya Idris pale alipotangazwa mshindi baada ya kumpiku mshindani mwenzake Tayo.

 

Idris akitahamaki na kwa kuanguka kwa furaha baada ya kutangazwa mshindi.



TOP 8 ya washiriki Big Brother Africa.





 
Newer Posts
Older Posts
Home
Subscribe to: Posts (Atom)

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL
  • KAULI YA UHURU KWENYE MTANDAOWA KIJAMII (TWITTER) KENYATTA HII HAPA
    Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto. Baadhi w...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • Ukistaajabu ya Mussa ?Nusu ya sura yake inafanana na binadamu na Nusu nyingine inafanana na CHURA, ni mtoto aliye zaliwa huko dodoma
    MKAZI  wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nus...
  • MASKINI MSUSI WA NYWELE AKUTWA AMEKUFA GESTI ,FUATILIA KUJUA ZAIDI
    Askari polisi pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya mtaa kata ya Gongoni manispaa ya Tabora akiangalia mwili wa mwanaume ...
  • Kafulila ampendekeza Dk.slaa kuwa mgombea urais UKAWA, Gazeti la mwananchi leo juma tatu
  • In long, dimly lit hallways, clusters of people wait anxiously outside courtrooms for their cases to come before a judge.
    The New York Immigration Court is an extraordinarily busy place. In long, dimly lit hallways, clusters of people wait anxiously outside co...
  • ZITHO "SHARTI MOJA , NARYDI CHADEMA"
    MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kuwa mwanasiasa yeyote makini kutoka vyama vya upinzani mwenye dhamira ya ku...
  • The New York clinic where Joan Rivers suffered a cardiac arrest during a medical procedure failed to follow standard protocols while treating her.Clinic cited for multiple failings
    Joan Rivers had been sedated during the procedure examining the back of her throat The comedian died on 4 September, aged 81,...
  • IT 'S MATTER OF FEW MINUTES FOR WORLD CUP 2014 START SHINNING !!!!
    The World Cup  The 2014  Brazil™ is now just a matter of minutes away and to mark the occasion FIFA have launched an updated version of th...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis