Jarida la maswala ya burudani, liitwalo Vibe Tz lililotoka hivi karibuni,limepambwa kwa picha za muigizaji wa filamu hapa Bongo, Irene Uwoya amabe ni mrembo aliebarikiwa suru na umbo matata bila kusahau rangi yake,kitu ambacho huwafanya vidume wengi kupagawa na kuwa na mashabiki wengi wa kazi zake mbali nakipaji chake katika sanaa.
Japokuwa kuwa kwasasa ni mama wa mtoto mmoja , Uwoya amefanya kile kinaitwa siku hizi –KU-BREAK THE INTERNET, kwenye picha alizopigwa na jarida hilo.
Irene ametokelezea kwenye kurasa za mbele yani “Cover Pages” akiwa mavalia mavazi ya ufukweni za rangi nyeusi na nyeupe, moja akiwa anatazama mbele na nyingine akitupa mgongo. Vivazi hivyo vimefanya sehemu kubwa ya mwili wake kuonekana na watu kuweza kujionea uumbaji wa alieviumba. Pia picha zingine zimeonekana kwenye kurasa za kati za jarida hilo akiwa katikati mapozi tofauti tofauti. Hakika Bidada AMETULIA…