Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Semua Post Berkategori Michezo
Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts
Mwaka mpya wa Diamond Platnumz huko Rwanda Utakuwa hivi.

Mwaka mpya wa Diamond Platnumz huko Rwanda Utakuwa hivi.

01:30







Diamond na The Boss Lady wakifanya yao.
Diamond Platnumz (katikati) akiwa kamshika mkono mpenzi wake wa sasa Zarinah Hassan ‘Zari’  au ‘The Boss Lady baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Rwanda






Umuhimu wa kushirikiana katika kazi hasa ya muziki

03:24










Maneno ya kizalendo ya Diamond platnum "There is no place like Home... Ever!

00:27






Japokuwa nina show Canada tareh 2 lakini ilinibidi kwanza nilete Mzigo
nlioagizwa na Wananchi Nyumbani kisha ndio nirudi kuendelea na shughuri zangu!... Kama wasemavyo
"There is no place like Home... Ever!"






Nyota ya Diamond yazidi kungara ,apokea tuzo nyingine huko Lagos Nigeria

Nyota ya Diamond yazidi kungara ,apokea tuzo nyingine huko Lagos Nigeria

00:24






tuzo
Diamond Platnumz ameshinda tuzo nyingine ambayo hizi zilikua zikitolewa Lagos nchini Nigeria ambazo hizi hazikuwa na utaratibu kama wa tuzo zingine kwa kupiga kura.

Baada ya kushinda tuzo hiyo ambayo ilienda kupokelewa na Meneja wake Salaam,Diamond alipost maneno haya>>’Thanks God,we have cheated another one on the future Awards Africa in Lagos Nigeria…#samenight Thank you Allah’
Tuzo hizi zinaitwa The Future Awards Prize in Entertainment ambapo kipengele alichokuwa akiwania Diamond alikuwa na wakali mbalimbali akiwemo Panshack au Ice Prince jina lake la zamani wa Nigeria na Michael Kwesi wa Ghana.




Ukweli kuhusu video ya zari iliyovuja mtandaoni

Ukweli kuhusu video ya zari iliyovuja mtandaoni

14:10


Dearest friends, my fans all over the world, relatives and well wishers, as you may be or may not be aware, the print media in Uganda is awash with stories infringing on my fundamental inalienable human rights by attacking my modesty both as a woman and a mother to the utter prejudice of my private life and family. The clear motive of such publication is undoubtedly to deter and/or downplay my tireless efforts in my preparations for The Zari All White Party slated for 18/12/14 which to a large extent has rubbed some of my detractors the wrong way. I have no doubt in my mind that the pictures that appeared in today's Red Pepper issue were leaked by someone  for their own selfish motives. Be that as it may, I would like to affirm that what goes on in my private life is absolutely my business that has no reason whatsoever to find it's way in the public realm. Privacy to/for/of a person is not a right granted by anyone, but it's inalienable. I am therefore steadfast in my resolve to hold the Zari All White Party for all my fans and friends in Uganda. And whilst I explore the option of seeking with a view of taking legal action against the  perpetrators/detractors and/or publishers, I want to assure all my family, fans and friends again to disregard such hurtful reports aimed at scoring cheap social points. Lastly, I call upon one and all to attend the All White Party as there'll be incredible performances from various artists including Diamond Platinumz, whose attendance is confirmed. I'd love to see you there, I'll be there to welcome you all and God willing, we shall have a great time like we always do. Bless you all, Zari.

BINGWA MBIO ZA MOTUMBWI KULAMBA KITITA CHA TSH. 2,700,000

14:01


Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za fainali za Kanda za mashindano ya bio za makasia zijulikanazo kama “Balimi Boat Race” zinazo dhaminiwa na bia ya Balimi Extara Lager zinazo tarajiwa kufanyika katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza leo.
BINGWA  MBIO ZA MITUMBWI KANDA YA ZIWA KUONDOKA NA 2,700,000/=
Na Mwandishi Wetu.Mwanza
Bingwa wa fainali za mashindano ya mbio za makasia Wanaume, chini ya udhamini wa Bia ya Balimi Extra Lager yajulikanayo kama “Balimi Boat Race 2014” anatarajia kujinyakulia kitita cha pesa taslimu Shilingi Milioni 2,700,000/=,Kikombe pamoja na medali za dhahabu kwa wanakikundi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya Balimi Exra Lager, Edith Bebwa alisema fainali hizo zitaanza majira ya saa tatu na asubuhi na kuendelea katika ufukwe wa Mwaloni jijini Mwanza ambapo jumla ya vikundi 15 vya Wanaume kutoka katika mikoa mitano ya Kanda ya ziwa vitachuana kumtafuta bingwa wa Kanda kwa mwaka 2014 na vikundi 11 upande wa Wanawake.
Edith alisema mikoa ya Kanda ya Ziwa inayoshiriki ni Kigoma,Kagera,Mwanza,Musoma na Kisiwa cha Ukerewe ambacho kinabeba hadhi ya Mkoa.

Mshindi wa pili Wanaume atazawadiwa pesa taslimu Shilingi 2,300,000/=,mshindi wa tatu Shilingi 1,700,000/= na wa nne 900,000/=.Wakati mshindi wa tano hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila kikundi alisema Edihi.

Upande wa wanawake bingwa wa mwaka 2014 ataibuka na kitita cha pesa taslimu Shilingi 2,300,000/=,kikombe na medali za dhahabu kwa wanakikundi wote.Mshindi wa tatu atazawadiwa Shilingi 1,700,000/=,wa tatu Shilingi 900,000/= na wa nne 700,000/= wakati mshindi wa 5 hadi wa 10 watazawadiwa kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi.

Nae Meneja wa Kampuni ya Bia nchini Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki aliwaomba wakazi wa jiji la Mwanza na vijiji jirani kujitokeza kwa wingi katika ufukwa wa Mwaloni kushuhudia fainali hizo zenye mvuto wa pekee na mwisho wafahamu nani atachukua ubingwa wa mbio hizo kwa mwaka 2014.


Meneja matukio wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema vikundi vyote vimeshawasili jijini Mwanza tayari kwa mpambano wa kumpata bingwa wa mwaka huu na maandalizi kwa ujumla yamesha kamilika hivyo nae aliwaomba watu wajitokeze kushuhudia mbio hizo.

SIMBA Vs EXPRESS YA UGANDA ,0-0 LEO UWANJA WA TAIFA

13:46


Katongole Henry akimtoka mshambulia wa Simba, Ramadhani Singano 'Mess'.
Kipa wa The Express, Mutumba Ivan akiruka juu kuokoa moja ya hatari langoni mwake.


Hii ndiyo kauli ya rapper chid benz

Hii ndiyo kauli ya rapper chid benz

13:39
Hatma ya rapper Chidi Benz kuhusiana na kama ataachia huru au kufungwa jela kutokana na mashtaka matatu yanayomkabili kufuatia kukamatwa na madawa ya kulevya, haikuweza kujulikana Alhamis hii baada ya kupanda tena kizimbani kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Chid Beenz_full
Chidi amepangwa kurejea tena mahakamani hapo January 15, 2015. Juzi rapper huyo alikuwa na imani kuwa Alhamis hii angeweza kujua hatma yake na pia kuwaomba watu wamkumbuke kwenye sala.
“Kesho ni judgement yangu na ni mwisho wa kesi yangu pale kwa hakimu mkazi Kisutu,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Najua nimekosea lakini sio sana kuliko makosa yote,muhimu ni kusamehe na kuondoa hasira na mimi,msipoteze Imani na mimi,nimekua msanii mzuri na bora kwa kipindi choote..nikiwa kazini inafahamika nachokifanya,sijawai kosea kuifanya kazi yangu hayo mengine ni mengine tayari..mnaweza kutokea kwa Sapot na naomba Mniombee.nisirudi kuule.Tafadhar.” 
 Mdogo wa  Zari Hassan apaka matope uhusiano wake na Diamond

Mdogo wa Zari Hassan apaka matope uhusiano wake na Diamond

13:17
Mdogo wake na Zari Hassan aka The Bosslady, aitwaye Karim ametumia Facebook kumkosoa dada yake kwa kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz ambaye anamzidi miaka 9.
 
Kwenye post hiyo, Karim aliandika: You are ashaming us, how can you date a boy my age. You moved from one man to another in less than 3 days.”
 
Akitumia akaunti yake binafsi ya Facebook yenye jina ‘Zarinah Tlale’, kujibu post hiyo ya mdogo wake huyo ambaye hapendezwi na kitendo cha dada yake kuwa na uhusiano na mtu mwenye umri kama wake, Zari alisema si Karim aliyeiandika.
zari
 
“Diamond is just a friend of mine. It’s never been written that female and male can’t be friends, it’s just the backward people that use that kind of perspective to blow things out of proportion,” aliandika.
zeetalk
10309502_10205619175663672_4957719935074097891_n
Katika hatua nyingine baada ya kumsindikiza Diamond kwenye tuzo za Channel O, Jumamosi iliyopita, Zari alimpa kampani pia kwenye utengenezaji wa video ya wimbo alioshirikishwa na kundi la Nigeria, Bracket.
10174778_10205619176663697_8518468057469568560_n
Tetesi Manchester United inaweza kutumia mpaka kiasi cha pauni milioni 350 kwa kipindi cha miaka miwili katika kusajili wachezaji wapya.

Tetesi Manchester United inaweza kutumia mpaka kiasi cha pauni milioni 350 kwa kipindi cha miaka miwili katika kusajili wachezaji wapya.

13:03
Manchester United inamlenga Kevin Strootman
Manchester United inaweza kutumia mpaka kiasi cha pauni milioni 350 kwa kipindi cha miaka miwili katika kusajili wachezaji wapya.
Hii inaweza kufikiwa kama watafanikiwa kuwasajili kiungo Kevin Strootman 24,toka roma, na beki wa Borussia Dortmund Mart Hummels, 25,pia inasadikika kocha Louis van Gaal anamtaka beki wa kulia wa Southampton Nathaniel Clyne, 23.
Arsenal wako tayari kurekebisha safu yao ya kiungo kwa kumuwania kiungo Morgan Schneiderlin, toka Southampton kwa dau la pauni milioni 15 pia wako tayari kutoa pauni milioni 8 kwa beki Tyrone Mings, 21,wa Ipswich Town.
Inter Milan wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambulaiji Joel Campbell, wa Arsenal raia wa Costa Rica pamoja na kiungo wa Tottenham Erik Lamela 22.
Henrique Pompeu wakala wa mshambuliaji wa Colombia Jackson Martinez 28, ameeleza kuwa mteja wake huyo hato ondoka katika timu yake ya Fc Porto japo timu za Arsenal, Liverpool and Tottenham zimekua zikimuwania.
Meneja wa Newcastle Alan Pardew, anawasiwasi nyota wake Moussa Sissoko,ataondoka St James' Park kuelekea Arsenal katika usajili wa dirisha dogo mwezi januari.
Real Madrid na Paris St-Germain wanapigana vikumbo kuweza kupata saini ya mshambuliaji Eden Hazard.Huku chelsea wakiwa tayari kumboreshea kandarasi yake ya sasa nyota huyo wa ubelgiji mwenye miaka 23.
Kiungo wa kibrazil Luca Silva,21,anayechezea klabu ya Cruzeiro yuko tayari kuzikata ofa za Manchester United na Arsenal ili kujiunga na miamba wa hispania Real Madrid.
Timu Leicester City itajaribu kutaka kumrejesha tena kwenye ligi ya Epl mshambuliaji Jermain Defoe, 32,toka klabu ya Toronto Fc.
HIVI NDIVYO Gangnam Walivyovunja rekodi huko YouTube

HIVI NDIVYO Gangnam Walivyovunja rekodi huko YouTube

12:56
Jump media player
Media player help
Out of media player. Press enter to return or tab to continue.

Na Kim Kardashian angekuwa amejeribu, lakini wimbo wa Gangnam ndio umevunja rekodi ya Internet.
Wimbo huo Umetazamwa mara bilioni mbili. Nambari kubwa ya watu kuwahi kutazama wimbo au chochote kwenye Youtube.
Wamiliki wa You Tube wanasema hawajawahi kutarajia kitu chochote kutazamwa hadi hapo. Wamelazimika kuongeza uwezo wa mtandao huo kuhifadhi data hadi 62 kutoka kwa 34.
Hii kali ya aina yake,Aliyewakosoa Sasha na Malia  kwa kuvaa nguo fupi ikulu ajiuzulu

Hii kali ya aina yake,Aliyewakosoa Sasha na Malia kwa kuvaa nguo fupi ikulu ajiuzulu

01:25
Sasha na Malia walikosolewa kwa kuvalia sketi fupi mbele ya umati katika White House
Mfanyakazi katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.
Rais Obama na mkewe wamejitahidi sana kuwalinda watoto wao kutokana na ndimi kali za vyombo vya habari 
 
Baadaye Lauten alifuta maandiko yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.
Bi Lauten pia alikuwa amewakosoa Sasha na Malia kwa kusema walionekana wasio na furaha walipokuwa wamesimama na baba yao katika hafla ya maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi kwamba Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla ile na hata kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi Lauten aliamua kujitoa kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa Facebook.
Sasha na Malia ni miongoni mwa vijana wadogo sana kuwahi kuwa katika ikulu ya White house
Mwanamke huyo akiomba msamaha, alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na kisha kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli aliwakera wasichana hao.
"ningependa kuomba radhi kwa wote niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha mwenendo wangu, '' alisema Lauten.
Arsenal yamlenga Kramer anaechezea klabu ya Borussia Monchengladbach

Arsenal yamlenga Kramer anaechezea klabu ya Borussia Monchengladbach

01:19
Arsenal wako tayari kutoa pauni milion 20 kumsajili kiungo wa timu ya taifa ya ujerumani Christoph Kramer, 23, anayechezea timu ya Borussia Monchengladbach, iwapo watamkosa nyota Sami Khedira wa Real Madrid.
Kocha wa PSG Laurent Blanc, anampango wa kumchukua mshambuliaji Thierry Henry, Kwa kumpa kandarasi ya muda mfupi.
Galatasaray nao wanawania saini mchezaji hiyo wa zamani wa Arsenal.
Liverpool watatoa ofa ya £25 kumpata kipa wa Fiorentina Neto, ili kuwa mbadala wa Simon Mignolet.
Mshambuliaji Lukas Podolski, 29, anaangalia uwezekano wa kuondoka arsenal mwezi januari na kurejea katika timu yake ya zamani FC Koln .
Inter Milan imeungana na Leicester City, Newcastle katika mbio za kumuwania mshambuliaji Luciano Vietto wa Villarreal.
Kiungo wa brazil Paulinho, 26, anatarajia kurejea nchini Brazil katika klabu ya Sao Paulo au Corinthians.
Boss wa Everton Roberto Martinez amekana kuwepo kwa makubaliano ya mkataba wa kumuuza kiungo James McCarthy 24, kwenda kwa washika bunduki wa London Arsenal.
Leicester yachezea kichapo cha goli 3 kwa 1 kutoka kwa Liverpool janam usiku

Leicester yachezea kichapo cha goli 3 kwa 1 kutoka kwa Liverpool janam usiku

01:17



Steven Gerrard akishangilia goli na wachezaji wenzake wa timu ya Liverpool, walipowalaza Leicester 3-1
Ligi ya kuu ya England iliendelea jana usiku katika viwanja mbali mbali. Leicester inayoburuza mkia katika ligi hiyo ikiwa na pointi 10 katika michezo 14 iliyocheza waliikaribisha Liverpool ambayo iliibuka na u
shindi wa magoli 3-1 katika mechi hiyo. Hadi kumalizikakwa kipindi cha kwanza timu hizo zilikuwa zimefungana goli 1-1. Kwa matokeo hayo Liverpool imeshika nafasi ya 8 nyuma ya Asernal , zote zikiwa na pointi 20. Hata hivyo Asernal imecheza mchezo mmoja pungufu ya Liverpool yenye mechi 14 ilizokwishacheza.
Matokeo mengine katika mechi za Jumanne usiku, Manchester United wakiwa kwenye uwanja wao wa Old Trafford, wameicharaza Stoke City mabao 2-1. Burnley imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Newcastle, Swansea wameitandika QPR magoli 2-0, Crystal Palace wamepoteza katika uwanja wao kwa kucharazwa goli 1-0 na Aston Villa. Nayo West Brom imepoteza kwa kufungwa 2-1 na West Ham.
Katika mechi za leo usiku, Arsenal watapepetana na Southampton katika uwanja wa Emirates, Chelsea vinara wa ligi watakuwa wenyeji wa Tottenham, huku Everton wakiikaribisha Hull City. Na Machester City inayoshika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 27 watataka kujiimarisha na kupunguza pengo la pointi sita kati yake na Chelsea, pale watakapomenyana na wenyeji wao Sunderland.
Mshambulaji wa Liverpool Mario Balotelli meomba radhi kwa kuweka picha yenye kuashiria vitendo vya kibaguzi

Mshambulaji wa Liverpool Mario Balotelli meomba radhi kwa kuweka picha yenye kuashiria vitendo vya kibaguzi

01:15

Mario Balotelli amekuwa akiandamwa na mashabiki wa soka kwa utovu wa nidhamu

 katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram. Balotelli 24, mwenye matukio mengi ya utukutu, haraka alifuta picha hiyo iliyokuwa kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“naomba radhi kwa yoyote aliekwazika. Nilifikiri kuwa ilikua ni ucheshi na sio ubaguzi ,sikujua kama inaweza kuwa na athari”.
Sakata hili la Balotelli limempelekea kocha wa Arsenal Wenger kuzungumza na kusema wachezaji wanapaswa kujichunga kwa kile wanachoweka kwenye mitandao ya kijamii
“Tunaweza kuwachunga na hatari ila hatuwezi kuwachunga wachezaji saa 24 za siku,wanawajibu wa kujichunga na nakuwa makini kwa kile wanachoandika”.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester City na Ac Milan atakosa mchezo wa leo wa ligi dhidi ya Leicester City sababu ni majeruhi.
AFCON 2015:Upangaji wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika

AFCON 2015:Upangaji wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika

01:10

AFCON 2015:Makundi ya timu 16 yatajwa

Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, AFCON
Upangaji wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17, 2015.
Upangaji wa makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo baada ya kutaka mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu nyingi zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani, pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015:
Kundi A Equatorial Guinea, Burkina Faso, Gabon, Congo
Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
Wenyeji Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu zilizopangwa kundi hilo.
Tatizo la kuwapo bandari bubu linazidi kuongezeka.

Tatizo la kuwapo bandari bubu linazidi kuongezeka.

04:25


Rais Jakaya Kikwete.PICHA|MAKTABA 

 Jeshi la Polisi mkoani Tanga juzi lilisema kwamba kuna zaidi ya bandari bubu 50 katika mkoa huo ambazo zinaingiza bidhaa ambazo hazilipiwi ushuru, huku nyingine zikiwa bandia.


Laiti Rais Jakaya Kikwete angekuwa na utaratibu wa Serikali yake kufanya tathmini endelevu ya utekelezaji wa kazi wa mawaziri katika wizara zote, angegundua kwamba zipo baadhi ya wizara ambazo viongozi wake ni mizigo isiyobebeka kutokana na kutofanya kazi, huku wakilipwa mishahara minono. Mfano hai ni Wizara ya Viwanda na Biashara, ambayo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kutotimiza majukumu yake. Ni wizara ambayo wananchi wengi wanasema haina lolote la kujivunia, kinyume na baadhi ya wizara, ambazo utendaji kazi wa mawaziri wake siyo tu umetukuka, bali pia ni wa kutolea mfano.
Wakati wa kuzindua mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) miezi kadhaa iliyopita, tuliambiwa kwamba mawaziri wote walipewa malengo ya utekelezaji wa mpango huo na kwamba kila waziri alisaini mkataba maalumu mbele ya Rais Kikwete, ‘akila kiapo’ kutekeleza majukumu hayo kwa mujibu wa mkataba huo. Vinginevyo angewajibishwa, kwa maana ya kupoteza kazi yake. Wapo mawaziri ambao wameonyesha uwajibikaji mkubwa katika utekelezaji wa malengo yaliyowekwa, lakini pia wapo mawaziri ambao wameendelea kufanya kazi kwa mazoea.
Pamoja na changamoto nyingi zinazoikabili Wizara ya Viwanda na Biashara, wananchi hawaoni nini kinafanyika katika kukabili changamoto hizo. Jana katika safu hii tulizungumzia changamoto ya ukosefu wa masoko kwa mazao ya biashara na chakula, tukisema wakulima wameachwa njia panda kwa mazao yao kutonunuliwa, huku wakibakia katika umaskini uliopitiliza.
Tunapozungumzia masoko tuna maana ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Tani zaidi ya 16 milioni za mahindi ya wakulima zilizorundikana katika mikoa ya Morogoro, Rukwa, Katavi, Mbeya na Iringa kwa kukosa soko ni ushahidi usioacha shaka kwamba wizara inayohusika na biashara haina mbinu na mikakati ya kumaliza kero hiyo.
Ni kazi ya wizara hiyo kwa kushirikiana na wizara inayohusika na uwezeshaji kuwaunganisha wakulima na mitandao ya masoko mbalimbali. Sukari inayozalishwa nchini imelundikana katika maghala kwa kukosa soko, huku bidhaa hiyo kutoka nje ikiingizwa nchini kwa bei ndogo kwa sababu ya kutolipiwa kodi. Wizara hiyo haijui kinachoendelea, ingawa inazo habari kwamba bidhaa nyingi zisizolipiwa ushuru zinaingizwa nchini kupitia bandari nyingi bubu zilizoenea katika maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi, yakiwamo maeneo ya Mbweni, Mlingotini, Ununio, Kawe, Msasani, Kunduchi, Kigamboni, Tegeta na Bagamoyo.
Tatizo la kuwapo bandari bubu linazidi kuongezeka. Jeshi la Polisi mkoani Tanga juzi lilisema kwamba kuna zaidi ya bandari bubu 50 katika mkoa huo ambazo zinaingiza bidhaa ambazo hazilipiwi ushuru, huku nyingine zikiwa bandia. Itakumbukwa kuwa, Waziri wa Biashara na Viwanda, Abdallah Kigoda alisema bungeni mwaka 2013 kuhusu kuwapo kwa bandari bubu na upitishaji wa bidhaa bandia katika maeneo mengi nchini. Kwa nini wizara husika haichukui hatua ni swali ambalo pengine linaweza kujibiwa na waziri huyo pekee.
Ndiyo maana wananchi wengi wanasema wizara hiyo ni mzigo, kwani imeshindwa siyo tu kuendeleza viwanda vidogovidogo, bali pia kuanzisha viwanda vya kusindika matunda kama nanasi, nyanya, maembe na machungwa ili wakulima wapate masoko ya mazao hayo. Ni kwa sababu hiyo tunasema wizara hiyo inahitaji waziri na watendaji wenye ubunifu na moyo wa kuwatumikia wananchi.
Mbeya City  Yashauriwa  kuchukua uamuzi mgumu

Mbeya City Yashauriwa kuchukua uamuzi mgumu

04:21
Joseph Kapinga 


Inawezekana kabisa Mwambusi amebeba msalaba ambao wengi waliutarajia. Kikosi chake kililewa sifa baada ya kufanya vizuri msimu uliopita kiasi cha kushika nafasi ya tatu ligi ilipomalizika.


Watafiti wa maisha ya binadamu na tabia zake, wanaamini kuwa kila mmoja utafika wakati atakutana na jambo litakalomlazimu kufanya au kutoa uamuzi mgumu.
Bila kujali jambo gani, lini na aina ya uamuzi anaoweza kuutoa, lakini ukweli unabaki palepale kwamba ipo siku lazima binadamu ataingia kwenye hali hiyo.
Katika maisha ya sasa yaliyojaa kila aina ya changamoto, chuki, visasi, migogoro na mabadiliko yenye ulazima ili kwenda sambamba na mahitaji ya maisha, yanawalazimu watu kufanya mambo ambayo hawatarajii.
Hata hivyo, kuna tofauti. Wapo ambao kutoa kwao uamuzi mgumu hutokana na shinikizo, hoja na mitazamo kutoka nje, wengine hufanya hivyo bila kusubiri misukumo ya nje bali ni kutokana na msuto wa dhamira kutoka ndani ya moyo.
Hongera kwa aliyekuwa kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi kwa kuchukua hatua ya kufanya uamuzi mgumu wa kuachana na timu hiyo bila shinikizo. Ni kama nilivyosema awali, Mwambusi amekutana na wakati ambao umemlazimu kufanya uamuzi mgumu ili kulinda heshima yake. Hakuna anayependa kuharibu ajira yake, lakini una sababu gani ya kusubiri kama mambo yameshaharibika?
Alichofanya Mwambusi ni ujasiri mkubwa kwa sababu, baadhi yetu wakati mwingine, iwe kwa kulewa madaraka au kwa lengo la kujishibisha, tunashindwa kutoa uamuzi mgumu hadi tulazimishwe.
Inawezekana kabisa Mwambusi amebeba msalaba ambao wengi waliutarajia. Kikosi chake kililewa sifa baada ya kufanya vizuri msimu uliopita kiasi cha kushika nafasi ya tatu ligi ilipomalizika.
Ilishangaza kwa timu ngeni, isiyo na wachezaji wenye majina na kocha wa ‘kawaida’ kupata matokeo mazuri kuizidi hata klabu kongwe ya Simba iliyojaza nyota kibao wa ndani na nje.
Kilichoiponza City ni kulewa mafanikio ya msimu uliopita na kudhani kuwa, wanaweza kufanya hivyo kirahisi msimu uliofuata. Walikosea!
Walidhani ligi ni peke yao, kwamba timu zingine zilizofanya vibaya msimu ambao wao walifanya vizuri, basi zingebaki kwenye nafasi hiyo ya kufanya vibaya. Walijidanganya!
Kila mmoja, kwa maana ya mashabiki wa soka Mbeya walikuwa wakisifu mafanikio ya timu hiyo, lakini, ni kwa kiasi gani walikuwa bega kwa bega kuisaidia kufanya vizuri msimu huu?
Sasa Mwambusi amefanya uamuzi mgumu, amejiuzulu. Ameiacha timu kwenye wakati mgumu.
Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa katika karata na mchezaji wa Tenisi Rafa Nadal

Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa katika karata na mchezaji wa Tenisi Rafa Nadal

06:52

Aliyekuwa mchezaji wa timu ya Brazil Ronaldo alilazimika kuosha vyombo baada ya kushindwa katika mchezo wa karata na mchezaji wa tennisi Rafa Nadal,na kumfanya mchezaji huyo wa tenisi kupokea dola 50,000 za hazina yake ya kutoa msaada huku Ronaldo akiosha vyombo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 alikabiliana vilivyo na mwana tenisi huyo kutoka uhispania katika mechi kati ya wawili hao katika meza ya pokerstar, Casino ya Hippodrome mjini London ambapo Nadal alishinda fedha hizo.
Duru ziliarifu kwamba kiini cha nyota hao wawili kukutana katika chumba kimoja ni chakula kilichoandaliwa katika hafla hiyo.
Hatahivyo kitu kilichowafurahisha wengi kulingana na wageni ni hatua ya Ronaldo kukubali kushindwa na kupewa kazi ya kuviosha vyombo vya Nadal alivyotumia kula.
Older Posts
Home
Subscribe to: Posts (Atom)

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL
  • KAULI YA UHURU KWENYE MTANDAOWA KIJAMII (TWITTER) KENYATTA HII HAPA
    Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto. Baadhi w...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • Ukistaajabu ya Mussa ?Nusu ya sura yake inafanana na binadamu na Nusu nyingine inafanana na CHURA, ni mtoto aliye zaliwa huko dodoma
    MKAZI  wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nus...
  • MASKINI MSUSI WA NYWELE AKUTWA AMEKUFA GESTI ,FUATILIA KUJUA ZAIDI
    Askari polisi pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya mtaa kata ya Gongoni manispaa ya Tabora akiangalia mwili wa mwanaume ...
  • Kafulila ampendekeza Dk.slaa kuwa mgombea urais UKAWA, Gazeti la mwananchi leo juma tatu
  • In long, dimly lit hallways, clusters of people wait anxiously outside courtrooms for their cases to come before a judge.
    The New York Immigration Court is an extraordinarily busy place. In long, dimly lit hallways, clusters of people wait anxiously outside co...
  • ZITHO "SHARTI MOJA , NARYDI CHADEMA"
    MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kuwa mwanasiasa yeyote makini kutoka vyama vya upinzani mwenye dhamira ya ku...
  • The New York clinic where Joan Rivers suffered a cardiac arrest during a medical procedure failed to follow standard protocols while treating her.Clinic cited for multiple failings
    Joan Rivers had been sedated during the procedure examining the back of her throat The comedian died on 4 September, aged 81,...
  • IT 'S MATTER OF FEW MINUTES FOR WORLD CUP 2014 START SHINNING !!!!
    The World Cup  The 2014  Brazil™ is now just a matter of minutes away and to mark the occasion FIFA have launched an updated version of th...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis