MSANII wa filamu na muziki wa taarabu Bongo, Upendo Mushi ‘Pendo’ yu kitandani baada ya kuugua ghafla kwa kile ambacho madaktari waligundua ni kunywa maji yasiyochemshwa.
Msanii wa filamu na muziki wa taarabu Bongo, Upendo Mushi ‘Pendo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, msanii huyo anayeishi Mwananyamala jijni Dar es Salaam, baada ya kupimwa na kukutwa na ugonjwa huo, alipatiwa matibabu na kurejea nyumbani ambako bado hali yake haijakaa sawa.
“Ni kweli, lakini nilishangaa sana madaktari walivyoniambia eti nilikunywa maji yasiyochemshwa wakati mimi siku zote nakunywa maji ya dukani, namshukuru Mungu lakini naendelea vizuri tofauti na nilivyopelekwa hospitali,” alisema Pendo baada ya kuulizwa kuhusu ishu hiyo