Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → MTOTO ANYONGWA NA BABA WA KAMBO , FUATILIA KISA HAPA

MTOTO ANYONGWA NA BABA WA KAMBO , FUATILIA KISA HAPA

Habari
Tuesday, 9 December 2014







Baba mzazi wa marehemu (kushoto) akiwa na waombolezaji.
“Kaka yake alifika, vurugu kubwa ikazuka, baadhi ya vitu vilipotea na kuvunjika kutokana na purukushani hiyo. “Kulipokucha Hamis akaenda kuripoti ofisi ya serikali ya kijiji ambapo mgambo walifika nyumbani na kutuchukua hadi Kituo cha Polisi Mvomero ambapo baada ya kuhojiwa tuliamriwa tumlipe Hamis shilingi laki nne kufidia hasara iliyotokea nyumbani kwake, tulilipa nusu hadi sasa tunadaiwa iliyobaki.
” UGOMVI SIKU YA TUKIO “Novemba 28, mwaka huu, siku mbili kabla ya mauaji ulizuka ugomvi tena kati yangu na Zamili  akipinga kulipa lile deni. Jumamosi tuligomba tena, alikuwa akilalamika kwamba Hamis anamlipisha fedha wakati anamtunzia mwanaye, nikamwambia kama anakereka kumtunza mwanangu anipe talaka, akagoma akidai bado ananipenda.

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Zamili Shabani kwa madai ya kumnyonga hadi kumuua mtoto wake wa kambo, (mwaka mmoja na nusu) huku mauaji hayo yakihusishwa na wivu wa mapenzi. 
Abdulrahman Hamis Clemensi enzi za uhai wake.
Tukio hilo la ajabu lililowaacha vinywa wazi wakazi wa eneo hilo lilijiri saa 6 mchana wa Desemba 2, mwaka huu kwenye nyumba waliopanga wanandoa hao, Zamili na mkewe, Rehema Mustafa (21) iliyopo Kijiji cha Mbogo, Tarafa ya Turiani Wilaya ya Mvomero mkoani hapa.
ALIVYOSEMA SHUHUDA Kabla ya kuzungumza na mama wa marehemu, Uwazi lilipata mawili-matatu kutoka kwa shuhuda mmoja wa tukio hilo. ”Mimi moja kwa moja namlaumu mama wa mtoto, Bi. Rehema. Awali alikuwa kwenye ndoa na mumewe Hamis, wakabahatika kumzaa Abdulrahman.
“Mwanzoni mwa mwaka huu alifika Zamili akitokea Zanzibar. Kwa taarifa tulizonazo Zamili alikuwa na ishu kubwa kule  ndiyo maana akaamua kuja huku. “Unajua vijijini, mtu akitokea mjini wanawake wanamshobokea. Dada yetu Rehema akadanganywa na Zamili akatoka kwenye ndoa yake na kuolewa naye mwezi wa saba mwaka huu.
Rehema Mustafa mama mzazi wa mtoto Abdulrahman Hamis Clemensi.
“Toka waoane kila siku ni ugomvi hadi juzi yalipotokea mauaji hayo,” alidai Said Seleman Kindu, mkazi wa kijiji hicho.   MAMA WA MTOTO SASA Baada ya kuzungumza na Said, Uwazi lilimhoji Rehema ambaye alikuwa na haya ya kusema: “Awali nilifunga ndoa na Hamis Clemensi, tukabahatika kumzaa mtoto mmoja ambaye ni huyo marehemu.
Baada ya kuachana na Hamis nilikaa nyumbani miezi mitatu, nikaja kufunga ndoa na Zamili, Julai 28, mwaka huu. “Tukio zima nahisi kama lilianzia Agosti,  mwaka huu kwani nakumbuka siku moja nikiwa sokoni nilikutana na Hamis akamsalimia mwanaye, kumbe kuna mtu alituona akaenda kumwambia Zamili.
“Aliporudi usiku tuligombana sana akitaka nimpeleke mtoto kwa baba yake, nikamwambia mwanangu bado ananyonya siwezi kumpeleka kama vipi asubiri atimize miaka mitatu nitampeleka hata kwa mama yangu mzazi.
“Licha ya kumwambia hivyo, Zamili akagoma, nikamwambia basi anipe talaka nirudi kwetu pia akakataa.”  “Siku iliyofuata, usiku alichukua kisu na kuniamuru nimpeleke mtoto kwa baba’ke,  tukatoka mimi, yeye na mtoto, lakini baba yake alipotuona alijificha juu ya dari huku akimpigia simu kaka yake anaitwa Kilimo na kumjulisha.

Hata hivyo, aliahidi kwamba atafanya mauaji.” SIKU YA TUKIO “Siku ya tukio Jumanne, saa 5 asubuhi, Zamili alinituma dukani, nikataka kwenda na mwanangu, akasema nimwache atanichelewesha, nikamwacha. “Niliporudi sikumuona mtoto, nikamuuliza Zamili mtoto yuko wapi? Akanijibu  kalala, nikaingia jikoni na kusonga ugali, tukala.
“Tulipomaliza, mimi nikaenda chumbani kumwamsha mwanangu ili naye ale. Nilishangaa kumuona kalegea. Kwa utoto wangu sikujua kama amekufa, nikaenda kuita wakubwa walipofika wakamuona mtoto kichwa kimegeukia mgongoni, wakaniambia mbona amekufa! “Palepale nikaangua kilio, watu wakajaa, baadaye viongozi wa kijiji wakaja na mgambo wakamkamata Zamili na kumpeleka polisi na mimi nikakodi bodaboda, nikabeba maiti ya mwanangu kuja hapa Mkindo kwa wazazi wangu.

Waombolezaji wakiwa msibani.
Mwanangu tumemzika jana (Alhamisi iliyopita),_nimebaki na kumbukumbu ya picha tu,” (akaanza kulia). Rehama alipotakiwa kutoa picha ya Zamili alisema: ”Huyu Zamili hana picha, hata kwenye harusi yetu aligoma kupigwa picha, nadhani alikuwa akitafutwa kule Zanzibar.
Alipoulizwa kama atakuwa tayari kuishi tena na Zamili, alisema: “Siko tayari mimi nataka talaka yangu.” BABA WA DAMU WA MAREHEMU Naye baba mzazi wa marehemu, Hamis Clemensi ambaye alikuwepo kwenye msiba huo wa mwanaye alipohojiwa na Uwazi alisema:  “Huyu jamaa ni wakuja, tulipata taarifa zake kwamba hakuwa mtu mzuri kule Zanzibar.
Alishataka kuniua mimi baada ya kunivamia kwangu usiku akiwa na mke wangu  na mtoto, eti amemleta mtoto wangu, nikapanda kwenye dari na kumpigia simu kaka yangu. Nasikitika kwa kumuua mwanangu.”






Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • Burkina Faso leaders agree transitional framework following the meeting held in Ouagadougou
      The blueprint for transition was agreed unanimously at the meeting in Ouagadougou A framework for a transitional government ...
  • John Doar, a civil rights lawyer who was a key figure in the struggle against racial segregation in the US, has died aged 92.
    John Doar was awarded the Presidential Medal of Freedom in 2012 Mr Doar dealt with some of the most prominent civil rights ca...
  • Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.
      OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semi...
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis