Mfanyabiashara huyo alikuwa akijishughulisha na biashara za maduka ya
bidhaa za jumla na nyumba za kupangisha katika eneo la Karanga pia ni
Mmiliki Serengeti Villa Bar and G house.
Tukio hilo lilithibitishwa na
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela.
Kamwela
alisema lilitokea juzi majira ya saa 11 alfajiri na kuongeza kuwa mwili
wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa uchunguzi
zaidi.
Kamwela alisema mke wa marehemu, aliyetajwa kwa jina la Elizabeth
Mallya, ndiye aliyebaini tukio la mumewe kujiua kwa kujipiga risasi moja
kifuani akiwa sebuleni kwake, ambapo alitoa taarifa polisi.
Shemeji wa marehemu huyo, Peter Masawe alidai shemeji yake alijiua kwa
kutumia bastola aina ya Browing yenye namba 96682, iliyokuwa na risasi
nane na inadaiwa alikuwa akiimiliki kihalali.
Masawe alidai
tukio hilo lilitokea siku moja kabla ya mfanyabiashara huyo hajatakiwa
kusafiri kesho kwenda India, ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya tumbo
kwa muda mrefu.
“Kwa taarifa za familia hii, tunafahamu kwamba Malya hakuwa na ugomvi na mtu yeyote akiwamo mkewe na wanawe wanne,” alisema.
Alisema katika tukio hilo la kujipiga risasi, Mallya alifariki papo
hapo akiwa nyumbani kwake na hakuna taarifa zaidi zilizotolewa juu ya
chanzo cha tukio hilo.
Hata hivyo, Masawe alisema Mallya mara kadhaa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo, ambalo hujaa baada ya kumaliza kula.
Masawe alisema mipango ilikuwa imekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kufika siku ya safari.