Watengezaji wa kikombe hiki wanakiita Vessly, kitaanza kuuzwa mwakani na kitapatikana kwa kiasi cha dola 99 tu.
Haya ndiyo maendeleo ya kiteknolojia
ambapo unaambiwa hiki kikombe kina uwezo wa kupima cafeine kutoka
iliyopo kwenye kinywaji unachokunywa, pamoja na kitu kingine chochote
ambacho kimo ndani ya kinywaji hicho hata kama ni kilevi, iwapo ukanywa
halafu ukashusha kikombe chini na una kiu bado kinakupa ishara kwamba
unatakiwa unywe tena kinyaji unachokunywa.
Kikombe hicho kinatumia app maalum
ambapo unaweza kukifanyia sync kupitia Bluetooth, iPhone Operating
System na Android app, unaweza kukichaji kwa Wireless, kina uwezo wa
kukaa na chaji kwa muda wa siku tano mpaka siku saba na kinaweza kuingia
chupa moja ya soda ya kawaida.