Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → Ukistaajabu ya Mussa ?Nusu ya sura yake inafanana na binadamu na Nusu nyingine inafanana na CHURA, ni mtoto aliye zaliwa huko dodoma

Ukistaajabu ya Mussa ?Nusu ya sura yake inafanana na binadamu na Nusu nyingine inafanana na CHURA, ni mtoto aliye zaliwa huko dodoma

Habari
Friday, 5 December 2014
MKAZI wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nusu ya sura yake inafanana na binadamu na nusu ikifanana na chura.
 
Mtoto huyo alizaliwa Desemba 2, mwaka huu katika Kituo cha Afya cha Mtakatifu Luka kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Mpwapwa. Alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.
 
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk Edwin Kihura mara baada ya mama huyo kufika katika kituo hicho cha afya alikuwa na uchungu ambao haukuwa na kikomo, lakini alishindwa kujifungua kwa njia ya kawaida licha ya njia ya uzazi kufunguka.
 
Alisema kutokana na hali hiyo iliwalazimu kumfanyia upasuaji mama huyo kwa lengo la kuokoa maisha yake na mtoto.
mtoto
  
Alisema wakati mama huyo akihudhuria kliniki walipojaribu kupima miezi ya mwisho mama huyo, mkao wa mtoto ulikuwa haupatikani pamoja na mapigo ya moyo lakini mtoto alikuwa anacheza tumboni jambo ambalo lilikuwa likiwashangaza waganga na wauguzi kituoni hapo.
 
Dk Kihura alisema mara baada ya mama huyo kufanyiwa upasuaji waliweza kutoa mtoto wa jinsi ya kike ambaye alikuwa na sura isiyoeleweka na kichwa kilikuwa na sura ya binadamu na nusu ikiwa ni sura inayofanana na chura huku viungo vingine vyote vya mwili vikiwa kamili.
 
Alisema zipo sababu kadha zinazoweza kusababisha tatizo kama hili ambapo alisema kuwa ni baadhi ya akinamama kukosa baadhi ya madini mwilini na uumbaji kutokamilika kutokana na sababu za kibaiolojia.
 
Alieleza kuwa hali ya mama huyo inaendelea vizuri na kwamba mtoto huyo alikuwa ni mtoto wake wa tano

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • MAREKANI YAITUPIA LAWAMA KOREA KASKAZINI
    Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala ...
  • MKUU wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Evarista Kalalu, awashauri wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii
    MKUU wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, Evarista Kalalu, amewashauri wananchi wa vijiji vya Ukami na Chogo Kata ya Mapanda wilayani hapa...
  • KAULI YA UHURU KWENYE MTANDAOWA KIJAMII (TWITTER) KENYATTA HII HAPA
    Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto. Baadhi w...
  • HAYA NDIO MAZITO ALIYO FUNGUKA YULE MSICHANA WA KAZI ALIYE MPIGA MTOTO
    Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Dun...
  • Ronaldo aosha vyombo baada ya kushindwa katika karata na mchezaji wa Tenisi Rafa Nadal
    Ali...
  • Wayne Goss, former premier of Queensland, kicked the bucket at 63
    Mr Goss, who was premier from 1989 to 1996, had suffered from ill health in recent years including brain tumours. He became Q...
  • IT 'S MATTER OF FEW MINUTES FOR WORLD CUP 2014 START SHINNING !!!!
    The World Cup  The 2014  Brazil™ is now just a matter of minutes away and to mark the occasion FIFA have launched an updated version of th...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis