Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → ZITHO "SHARTI MOJA , NARYDI CHADEMA"

ZITHO "SHARTI MOJA , NARYDI CHADEMA"

Habari
Friday, 5 December 2014


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kuwa mwanasiasa yeyote makini kutoka vyama vya upinzani mwenye dhamira ya kuiondosha madarakani Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hawezi kukwepa kufanya kazi na muungano wa vyama vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Zitto anasema kuwa hata vyama vichanga vinavyokua kama ACT-Tanzania na vingine, vina nafasi ya kuingia katika umoja huo ili kuzidisha nguvu ya upinzani kuing’oa CCM kwa maslahi ya nchi na wananchi.
Mwanasiasa huyo, alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na gazeti hili, yaliyofanyika juzi nyumbani kwake jijini Dar es Salaam juu ya masuala mbali mbali ya kijamii na kisiasa, huku akieleza namna UKAWA wanavyoweza kufanikisha ushindi wa kuing’oa CCM.
Zitto alisema kuwa, uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Disemba 14 mwaka huu, uchukuliwe kama sehemu ya kujifunza makosa yatakayofanyiwa kazi kuelekea katika ushindi wa mwaka 2015.
“Nimefurahi kukutana na wenzangu wa CHADEMA wakati wa mashauriano juu ya maazimio ya kamati ya PAC, nimekulia CHADEMA…nimefanya kazi CHADEMA, wapo niliowalea kisiasa, wapo niliowapokea kina Silinde, Lyimo na wengine, hivyo kukutana nao kwa pamoja baada ya mtafuruku ulioanza Disemba 22 mwaka jana, kumenipa faraja sana na sioni shida kufanya kazi na UKAWA kwa maslahi ya nchi,”alisema Zitto.
Alisema tofauti yake na chama chake haiwezi kumzuia kufanya kazi na UKAWA na kwamba hata kukutana kwao katika kujadili maazimio ya kamati ya Bunge kwa ajili ya kuwachukulia hatua watuhumiwa wa kashfa ya Escrow, ulikuwa mpango wa Mungu.
Kwa mujibu wa Zitto, ili UKAWA waweze kushinda katika uchaguzi ujao ni vema viongozi pasipo kujali maslahi binafsi, wakajiwekea malengo ya idadi ya viti vya ubunge watakavyopigania kwa nguvu zote wakiwa katika mgawanyo watakaokubaliana.
“Katika hili la ushindi kwa upinzani ndani ya muunagano ni dhahiri hauna mjadala, cha muhimu ni kukubaliana kwa mfano kuwa wanataka wabunge wangapi watakaowapigania kwa pamoja na hapa wasipungue 150 kwa mgawanyo utakaokubalika; mfano Zanzibar, CUF wasimamishe wagombea katika majimbo yote na bara wapate katika baadhi ya maeneo wanayokubalika,” alisema na kuongeza;
“CHADEMA NCCR-Mageuzi na ACT-Tanzania waweke wagombea kwa upande wa bara katika maeneo wanayokubalika na kila mgombea apiganiwe kwa nguvu zote katika eneo analokubalika dhidi ya mgombea wa CCM,”alisema Zitto.
Alisema vyama hivyo kwa umoja wao vikiwa na uhakika wa kupata wabunge 150, wasiokuwa na ushindani kutoka CCM, wanaweza kugombania majimbo mengine kwa ajili ya kuongeza idadi ya wabunge kwa lengo la kupata serikali yenye nguvu zaidi.
Kuhusu kutafuta maridhiano ndani ya CHADEMA, Zitto alisema maridhiano ya aina yoyote yatakayofanywa yanapaswa kuwashirikisha watu wote walioumizwa na shutuma alizopewa.
“Nimesamehe kila aina ya matusi niliyofanyiwa lakini mambo mawili sitoweza kuyaacha, moja ni kutaka shutuma kuwa ninatumiwa na CCM kwa ajili ya usaliti ithibitishwe na kama haupo waliotunga uongo huo wawajibishwe kwa kuwa hii pasipo kuthibitishwa kwa tuhuma hizo za usaliti, kutamuathiri hata mwanangu na kizazi change,”alisema Zitto.
Alisema yupo tayari kuwajibika kwa yale atakayoyafanya kuliko kuvumilia baadhi ya mambo yasiyokuwa na maslahi kwa Umma.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • Chuo kikuu cha ardhi ARU chatoa zawadi kwa wanafunzi 30, mmoja, ambae ni muhitimu wa masomo ya surveying aibuka na machine ya millioni 35
    CHUO Kikuu Ardhi (ARU), kimewazawadia wanafuzi 130 wa masomo mbalimbali zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 60 kutokana n...
  • Ajali ya gari huko south B kenya
    There was a bizarre accident today morning in Hazina Estate, South B involving a Range Rover that crashed into 7 vehicles. The Ran...
  • Arsenal yamlenga Kramer anaechezea klabu ya Borussia Monchengladbach
    Arsenal wako tayari kutoa p...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • MAREKANI YAITUPIA LAWAMA KOREA KASKAZINI
    Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala ...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis