Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala Yousafzai raia wa Pakistani amesema kuwa siku zijazo anatarajia kuwa mwanasiasa.
Malala amesema ndoto yake hiyo anatarajia kuikamilisha baada ya kumaliza masomo yake na amesema ikiwezekana anapenda kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.
Binti huyo ambaye amekuwa akiendesha kampeni ya elimu dhidi ya wasichana alipigwa risasi na wapiganaji wa Talban miaka miwili iliyopita.
Mshindi huyo wa Nobel Malala yupo mjini Oslo ,Norway anatarajiwa kupokea Nishani anayoshirikiana na Bindi raia wa India Kailash Satyarthi