Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → ANUSURIKA KIFO , NI BAADA YA KICHWA CHAKE KUCHIMBWA A SULULU

ANUSURIKA KIFO , NI BAADA YA KICHWA CHAKE KUCHIMBWA A SULULU

Habari
Tuesday, 9 December 2014




HAKUNA neno jingine la kutumia zaidi ya kusema; KWELI MUNGU MKUBWA! Ni miezi mitano sasa imekatika tangu kusambaa kwa picha mitandaoni zilizomwonesha mwanaume mmoja akiwa ameshindiliwa sululu kichwani huku kisa kikiwa hakijulikani.


“Kwanza kabisa napenda kusema kweli Mungu ni mkubwa, nimepona! Ingawa mwili bado hauna nguvu sawasawa lakini naendelea vizuri. “Ilikuwa tarehe 19, Julai mwaka 2013  katika machimbo ya Mgodi wa Miombo- Rwamgasa  wilayani Geita, mimi ni fundi wa kuchimba maduara yanayotumika kuchimbia dhahabu.
“Baada ya kumaliza kazi zangu majira ya jioni, nikaenda kupumzika ili kujiandaa kwa siku iliyofuata. “Nilikuwa nimepumzika na wenzangu zaidi ya mia moja, unajua tena migodini. Kufika saa 3 hivi usiku nikiwa nimeanza kusinziasinzia, nilishtukia kitu kizito kinaingia kichwani mwangu upande  wa kushoto.” ALISHINDWA KUPIGA KELELE “Nilishindwa kupiga kelele nadhani kwa sababu ya kule kusinzia. Wenzangu ambao nao walianza kulala walishtuka kwa kusikia harufu ya damu, wakaamka na kuja wakanikuta sululu ikiwa imezama kichwani.

Oka Kaombe kabla ya kufanyiwa upasuaji.
“Hii sululu kule machimbo ni maarufu kwa jina la Moko, hutumika kuchimbia madini katika migodi. Nilichukuliwa na sululu yangu kichwani na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza  kwa ajili ya matibabu ya haraka.” SIKU NNE BILA FAHAMU Oka anazidi kusimulia: “Mengine ninayosimulia niliambiwa kwani nilipoteza fahamu kwa siku nne.
Nilianza kujitambua baada ya siku nne nikiwa palepale Bugando na kujikuta nipo hospitali lakini nilikuwa siwezi kuzungumza wala kusikia vizuri. Maumivu yalikuwa makali sana kutokana na sululu kuzama kichwani maana ilipoingia ilikwenda kutokea upande wa pili wa kichwa. “Nikiwa nimeshafanyiwa upasuaji kwa kuchomolewa sululu, niliendelea kukaa Bugando kwa siku 52.”
ATOROKA BUGANDO, AMSAKA MBAYA WAKE Oka alisema kuwa, hiyo siku ya 52 aliamua kutoroka hospitalini hapo kwa sababu alishindwa kulipia gharama za matibabu ambazo ni shilingi laki tisa (900,000). “Kiasi hicho cha pesa kwangu kilikuwa kikubwa na hata sasa bado ni kikubwa ndiyo maana niliamua kutoroka,’’ alisema Oka. ALIYEMZAMISHA SULULU AJULIKANA Oka anaendelea kusimulia:
“Nilipotoka hospitalini kitu cha kwanza nilianza kumtafuta mtu aliyenifanyia kitendo kile cha kinyama, marafiki zangu wakanipa ushirikiano  na kuniambia unyama ule ulifanywa na jamaa mmoja anayeitwa  Masha. “Huyu Masha ni mchimbaji wa madini kwenye ule mgodi lakini alikimbia baada ya kufanya tukio na mpaka sasa hajulikani alipo.”
KISA CHA KUPIGWA SULULU PIA CHAJULIKANA Oka alisema taarifa alizopata baadaye kutoka kwa wachimbaji mgodini hapo ni kwamba,  lengo la Masha kumpiga na sululu lilikuwa ni kumtoa kafara (ndagu) ili aweze kupata dhahabu nyingi na awe bilionea kwa siku za usoni. “Ila Mungu ni mkubwa alitupilia mbali wazo hilo mpaka sasa niko hai,” alisema Oka.
AFYA YAKE KWA SASA Oka alisema kwa sasa anaamini amepona kabisa kidonda chake kichwani ila hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na mwili kukosa nguvu za kutosha.
UPASUAJI MWINGINE Aliendelea kusema kuwa, akiwa Bugando aliambiwa na madaktari kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine na kuwekewa vyuma kichwani baada ya kuwekewa vyuma hivyo itabidi akae miaka mitatu bila kufanya kazi yoyote ndipo atapata nguvu za kufanya kazi kama zamani.
MAISHA YAKE KWA SASA Oka alisema maisha yake kwa sasa ni magumu kwani ana watoto 5, lakini pia alitengana na mke wake hivyo yeye ndiye baba na mama wa familia kwani hata wazazi wake wamezeeka, hivyo wanamtegemea yeye. ANACHOWAOMBA WATANZANIA Alisema kwa sababu bado ana safari ya kujitibu na pia kutunza familia, amewaomba Watanzania wenye kuguswa na mkasa wake wamsaidie pesa kwa kiasi chochote atakachojaliwa mtu kwa kutumia simu yake ya mkononi ambayo ni 0682 013479. 






Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Takribani watu 15 wapata upofu baada ya upasuaji nchini India
    Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji walisema walishindwa kuona tena baada ya kuondoa bandeji kwenye macho yao Maafisa wa utawala nchini Indiaa w...
  • Familia ya mateka yasihi Al Qaeda kumwachilia
    Marekani imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen. ...
  • Ona kilichotokea kwa jimama hili kipindi lina jaribu kucheza jirani na swimming pool.Noii huko Kenya mida ya jana jioni
       
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL
  • KAULI YA UHURU KWENYE MTANDAOWA KIJAMII (TWITTER) KENYATTA HII HAPA
    Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto. Baadhi w...
  • Maandano zidi ya kutupiliwa mbali kwa kesi ya afisa polisi mjini New York
    Maandamano mjini New York Waandamanaji wameingia katika barabara za miji mingi Nchini Marekani kwa usiku wa pili mtawalia, kupinga maamu...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • MORE THAN 10,000 GRADUATES TURN UP FOR SEVENTY JOB VACANCIES IN DAR ES SLAAM.
    According to the list of names seen by The Guardian yesterday morning, the department listed 10,816 candidates to perform the interview tha...
  • Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala amenukuliwa akisema "Nataka kuwa Waziri mkuu''
    Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala Yousafzai raia wa Pakistani amesema kuwa siku zijazo anatarajia kuwa mwanasiasa. Malala a...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis