Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → Michezo → Tatizo la kuwapo bandari bubu linazidi kuongezeka.

Tatizo la kuwapo bandari bubu linazidi kuongezeka.

Habari, Michezo
Wednesday, 26 November 2014


Rais Jakaya Kikwete.PICHA|MAKTABA 

 Jeshi la Polisi mkoani Tanga juzi lilisema kwamba kuna zaidi ya bandari bubu 50 katika mkoa huo ambazo zinaingiza bidhaa ambazo hazilipiwi ushuru, huku nyingine zikiwa bandia.


Laiti Rais Jakaya Kikwete angekuwa na utaratibu wa Serikali yake kufanya tathmini endelevu ya utekelezaji wa kazi wa mawaziri katika wizara zote, angegundua kwamba zipo baadhi ya wizara ambazo viongozi wake ni mizigo isiyobebeka kutokana na kutofanya kazi, huku wakilipwa mishahara minono. Mfano hai ni Wizara ya Viwanda na Biashara, ambayo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa kutotimiza majukumu yake. Ni wizara ambayo wananchi wengi wanasema haina lolote la kujivunia, kinyume na baadhi ya wizara, ambazo utendaji kazi wa mawaziri wake siyo tu umetukuka, bali pia ni wa kutolea mfano.
Wakati wa kuzindua mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) miezi kadhaa iliyopita, tuliambiwa kwamba mawaziri wote walipewa malengo ya utekelezaji wa mpango huo na kwamba kila waziri alisaini mkataba maalumu mbele ya Rais Kikwete, ‘akila kiapo’ kutekeleza majukumu hayo kwa mujibu wa mkataba huo. Vinginevyo angewajibishwa, kwa maana ya kupoteza kazi yake. Wapo mawaziri ambao wameonyesha uwajibikaji mkubwa katika utekelezaji wa malengo yaliyowekwa, lakini pia wapo mawaziri ambao wameendelea kufanya kazi kwa mazoea.
Pamoja na changamoto nyingi zinazoikabili Wizara ya Viwanda na Biashara, wananchi hawaoni nini kinafanyika katika kukabili changamoto hizo. Jana katika safu hii tulizungumzia changamoto ya ukosefu wa masoko kwa mazao ya biashara na chakula, tukisema wakulima wameachwa njia panda kwa mazao yao kutonunuliwa, huku wakibakia katika umaskini uliopitiliza.
Tunapozungumzia masoko tuna maana ya masoko ya ndani na nje ya nchi. Tani zaidi ya 16 milioni za mahindi ya wakulima zilizorundikana katika mikoa ya Morogoro, Rukwa, Katavi, Mbeya na Iringa kwa kukosa soko ni ushahidi usioacha shaka kwamba wizara inayohusika na biashara haina mbinu na mikakati ya kumaliza kero hiyo.
Ni kazi ya wizara hiyo kwa kushirikiana na wizara inayohusika na uwezeshaji kuwaunganisha wakulima na mitandao ya masoko mbalimbali. Sukari inayozalishwa nchini imelundikana katika maghala kwa kukosa soko, huku bidhaa hiyo kutoka nje ikiingizwa nchini kwa bei ndogo kwa sababu ya kutolipiwa kodi. Wizara hiyo haijui kinachoendelea, ingawa inazo habari kwamba bidhaa nyingi zisizolipiwa ushuru zinaingizwa nchini kupitia bandari nyingi bubu zilizoenea katika maeneo ya Pwani ya Bahari ya Hindi, yakiwamo maeneo ya Mbweni, Mlingotini, Ununio, Kawe, Msasani, Kunduchi, Kigamboni, Tegeta na Bagamoyo.
Tatizo la kuwapo bandari bubu linazidi kuongezeka. Jeshi la Polisi mkoani Tanga juzi lilisema kwamba kuna zaidi ya bandari bubu 50 katika mkoa huo ambazo zinaingiza bidhaa ambazo hazilipiwi ushuru, huku nyingine zikiwa bandia. Itakumbukwa kuwa, Waziri wa Biashara na Viwanda, Abdallah Kigoda alisema bungeni mwaka 2013 kuhusu kuwapo kwa bandari bubu na upitishaji wa bidhaa bandia katika maeneo mengi nchini. Kwa nini wizara husika haichukui hatua ni swali ambalo pengine linaweza kujibiwa na waziri huyo pekee.
Ndiyo maana wananchi wengi wanasema wizara hiyo ni mzigo, kwani imeshindwa siyo tu kuendeleza viwanda vidogovidogo, bali pia kuanzisha viwanda vya kusindika matunda kama nanasi, nyanya, maembe na machungwa ili wakulima wapate masoko ya mazao hayo. Ni kwa sababu hiyo tunasema wizara hiyo inahitaji waziri na watendaji wenye ubunifu na moyo wa kuwatumikia wananchi.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • Ajali ya gari huko south B kenya
    There was a bizarre accident today morning in Hazina Estate, South B involving a Range Rover that crashed into 7 vehicles. The Ran...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • MAREKANI YAITUPIA LAWAMA KOREA KASKAZINI
    Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala ...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis