Hatma ya rapper Chidi Benz kuhusiana na kama ataachia huru au kufungwa jela kutokana na mashtaka matatu yanayomkabili kufuatia kukamatwa na madawa ya kulevya, haikuweza kujulikana Alhamis hii baada ya kupanda tena kizimbani kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Chidi amepangwa kurejea tena mahakamani hapo January 15, 2015. Juzi rapper huyo alikuwa na imani kuwa Alhamis hii angeweza kujua hatma yake na pia kuwaomba watu wamkumbuke kwenye sala.
“Kesho ni judgement yangu na ni mwisho wa kesi yangu pale kwa hakimu mkazi Kisutu,” aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“Najua nimekosea lakini sio sana kuliko makosa yote,muhimu ni kusamehe na kuondoa hasira na mimi,msipoteze Imani na mimi,nimekua msanii mzuri na bora kwa kipindi choote..nikiwa kazini inafahamika nachokifanya,sijawai kosea kuifanya kazi yangu hayo mengine ni mengine tayari..mnaweza kutokea kwa Sapot na naomba Mniombee.nisirudi kuule.Tafadhar.”