IMEVUJA! Msanii wa filamu Bongo, Wellu Sengo, ‘Matilda’, licha ya kuwa na mtoto mdogo ambaye hajafikisha hata mwaka, inadaiwa tayari amenasa ujauzito mwingine.Chanzo makini kinaeleza kuwa ujauzito huo ni wa mmoja wa wasanii wenye majina maarufu hapa nchini, ambao wamekuwa katika uhusiano kwa muda mrefu sasa.
Katika mawasiliano kwa njia ya simu, Wellu baada ya kubabaika, alikiri kuwa na ujauzito na kumtaja msanii huyo kama ndiye mwenye mzigo, lakini jina lake linahifadhiwa kwa sasa kwa vile mwenyewe hakupatikana ili kuzungumzia madai hayo.
“Haa, wewe nani kakuambia habari hizi, lakini aah, ni kweli bwana nina ujauzito na mwenyewe ni (anamtaja jina). Si unajua tena mambo ya kawaida haya,” alisema muigizaji huyo.
Msanii huyo anayetajwa kuhusika na jambo hilo, ambaye hata hivyo ni mume wa mtu, amekuwa akionekana kuwa Wellu karibu katika maeneo mengi ya starehe na kijamii akiwa. Baadhi ya wasanii wamekuwa wakimdhihaki mwanaume huyo kwa kumuona kuwa haendani kimuonekano na mwanadada huyo.