Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Habari
Tuesday, 25 November 2014
Gavana Benno Ndulu 





OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semina  kwa waandishi wa habari, mjini Bagamoyo  kujifunza mambo mbalimbali. Miongoni mwa mada zilizotolewa ni ukweli kuhusu umoja wa fedha katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mada hiyo Ilitolewa na Mchumi Mwandamizi kutoka Idara ya Utafiti BoT, Dk Suleiman Missango ambaye anaelezea ukweli kuhusu  umoja huo.
Miongoni mwa mambo aliyoyatolea ufafanuzi ni maeneo makuu ya itifaki ya umoja wa fedha, mambo muhimu ya kutekeleza kabla ya kuanzisha umoja wa fedha, mambo muhimu yatakayotokana na umoja wa fedha, manufaa ya umoja wa fedha na changamoto.
Umoja wa Fedha
Dk Missango anasema majadiliano ya kuandaa itifaki hiyo yalianza Januari 2011 na kukamilika Julai, 2013. Kukamilika huku kunatokana na itifaki hiyo  kupitishwa na mkutano wa tatu wa baraza la mawaziri wa sekta ya umoja wa fedha na kuidhinishwa na mkutano wa dharura wa 27 wa baraza la mawaziri la jumuiya uliofanyika Julai 2013 na kuridhiwa na baraza la mawaziri la sekta ya sheria na katiba Novemba 15, 2013.
Anaeleza itifaki hiyo ilisainiwa na wakuu wa nchi wa Jumuiya Novemba 30, 2013. Wakuu wa nchi wanachama waliagiza Itifaki hiyo iridhiwe na nchi zote wanachama ifikapo Julai, 2014, ili itekelezaji wake uanze mara moja.
Maeneo makuu ya itifaki ya umoja wa fedha
Akizungumzia itifaki ya umoja wa fedha, Dk Missango anaeleza ina maeneo makuu 10 ambayo eneo la kwanza linaelezea tafsiri ya maneno yaliyotumika katika Itifaki.
Eneo la pili linaelezea uanzishaji wa umoja wa fedha, madhumuni yake na upeo wa ushirikiano katika umoja wa fedha. Katika eneo hili, Itifaki inaanisha kuwa umoja wa fedha utaanzishwa hatua kwa hatua kwa kuzingatia mpango kazi ulioandaliwa, na nchi wanachama kufikia vigezo vilivyokubalika vya muunganiko wa uchumi mpana na masharti mengine yaliyoanishwa katika Itifaki.
Anasema eneo la tatu linaainisha shughuli muhimu za kukamilishwa na nchi wanachama kabla ya kuingia kwenye umoja wa fedha.
Katika eneo hili nchi wanachama zinakubaliana kukamilisha utekelezaji wa iItifaki ya umoja wa forodha na itifaki ya soko la pamoja kama msingi wa kujenga uchumi imara utakaopelekea kuunda umoja wa fedha tulivu na stahimilivu.
Aidha, nchi wanachama zinakubaliana kurazinisha (hormonise) sera za bajeti, sera za fedha, na sera za ubadilishaji wa fedha za kigeni, ili kurahisisha uanzishwaji wa umoja wa fedha na pia kujenga ukanda tulivu wa kifedha ndani ya Jumuiya.
“Eneo la nne linaainisha vigezo vilivyokubalika vya kupima utayari wa nchi wanachama kujiunga na umoja wa fedha na utaratibu wa upimaji wa utekelezaji wake,”anafafanua  Dk Missango.
Anasema eneo la tano linaanisha mahusiano katika sera za uchumi mpana wa nchi wanachama. Katika eneo hili Itifaki inabainisha kuwa jukumu la kutunga sera ya fedha (monetary policy) na sera ya ubalishanaji wa fedha za kigeni (exchange rate policy) litakuwa chini ya Benki Kuu ya Jumuiya na jukumu la kutunga na kutekeleza sera za bajeti (fiscal policies) litabaki kwa nchi wanachama.
Hata hivyo, ili kuondoa uwezekano wa mgongano wa kisera, nchi wanachama zitatakiwa kurazinisha na kuratibu utekelezaji wa sera zao za kibajeti.
Aidha, nchi wanachama zinatakiwa kuzingatia nidhamu ya kibajeti, ili kutodhoofisha umoja wa fedha na kusababisha mdororo wa uchumi ndani jumuiya.
“Katika eneo la sita nchi wanachama zinakubaliana kuimarisha na kuendeleza sekta ya fedha pamoja na kuimarisha na kuunganisha mifumo ya malipo (Payment and settlements systems), ili kurahisisha muamala wa kibiashara ndani ya umoja wa fedha,”anaeleza Dk Missango.
Anaeleza eneo la saba linahusu takwimu ambapo nchi wanachama zinakubaliana kuandaa mfumo wa pamoja wa kuandaa, kuchambua na kutoa takwimu sahihi kwa ajili ya utekelezaji wa umoja wa fedha.
Anasema katika eneo la nane, nchi wanachama zinakubaliana kuwa na sarafu moja baada ya kutimiza vigezo vya muunganiko wa uchumi mpana vilivyokubalika.
Pia kwa kutambua kuwa nchi zote wanachama haziwezi kufikia vigezo hivyo na masharti mengine ya kuanzisha umoja wa fedha kwa wakati mmoja, itifaki inaruhusu angalau nchi tatu zikifikia vigezo na masharti yaliyoanishwa katika Ibara ya 5 na 6 zianze kutumia sarafu moja. Aidha nchi nyingine zinaweza kujiunga baada ya kutimiza vigezo hivyo.
Anabainisha kuwa eneo la tisa linaainisha taasisi muhimu zitakazoanzishwa kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa umoja wa fedha. Taasisi ya kwanza ni Benki Kuu ya Jumuiya (The East African Central Bank) ambayo kwa kushirikiana na Benki Kuu za nchi wanachama zitaunda mfumo wa benki kuu wa Jumuiya (EAC system of Central Banks).
Katika mfumo huo, Benki Kuu ya Jumuiya itakuwa na jukumu la kutunga sera na benki kuu za nchi wanachama zitabaki na jukumu la utekelezaji wa sera husika (Ibara ya 20).
Taasisi nyingine zitakazoundwa ni pamoja na taasisi ya takwimu, taasisi ya kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa matakwa ya itifaki ya umoja wa fedha, ili kuhakikisha kuwa Jumuiya inaunda umoja wa fedha tulivu, endelevu na stahimilivu, na taasisi mbalimbali za kusimamia na kuratibu sekta za fedha.
Kwa mujibu wa mkataba wa uanzashaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wakuu wa nchi wanachama wataunda taasisi zilizotajwa baada ya kupata mapendekezo kutoka baraza la mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
“Eneo la kumi na la mwisho linaelezea kuhusu masuala ya ujumla ikiwemo Itifaki kupata nguvu ya kisheria baada ya kuridhiwa na nchi zote wanachama,”anaeleza Dk Missango.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • John Doar, a civil rights lawyer who was a key figure in the struggle against racial segregation in the US, has died aged 92.
    John Doar was awarded the Presidential Medal of Freedom in 2012 Mr Doar dealt with some of the most prominent civil rights ca...
  • Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.
      OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semi...
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL
  • Kiungo mpya wa Azam, Amri Kiemba akiwa katika jezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam jana
       Klabu ya Yanga imemleta nchini kwa majaribio mshambuliaji raia wa Zambia, Jonas Sakuwaha ...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis