Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.
Rais
Barack Obama wa Marekani amesema utawala wake utafanya hivyo baada ya
kuilaumu nchi hiyo kufanya uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony
Pictures.
Amesema mara tu mchakato wao huo utakapokamilika,
watajibu mashambulizi hayo. Korea kaskazini imeziita tuhuma hizo
zilizotolewa na Marekani dhidi yake kuwa ni za uzushi.
Korea
kaskazini ilikuwa katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, kabla ya
kuondolewa wakati wa utawala wa Rais George Bush wa Marekani mwaka 2008.
Katikati ni kiongozi wa Korea kaskazini Kim jong_un