1.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na Zitto
Kabwe hakuniita ili kupata nafasi ya kujitetea, kutokana na shutuma
ambazo zimekuwa zikielekezwa kwangu, kwamba nilipewa fedha kupitia
akaunti ya Escrow.
2.
Kujiuzulu sio fasheni, kwa kuwa fedha nilizopata ni kwa ajili ya
mchango wa shule ya Barbro Johansson ya jijini Dar es Salaam na
kujiuzulu ni kitu ambacho kina sababu zinazohitaji uwajibikaji.
Nijiuzulu kwa kuwa nimepata mchango wa shule?
3.
“Nijiuzulu kwa sababu gani?… kwa kupata mchango wa shule!… kujiuzulu ni
kitu chenye sababu zake, kujiuzulu sio fasheni, lazima kuwe na sababu,
hata Rais aliyenipa kazi atashangaa. Naona ufahari kufanikisha mchango
wa shule yangu.
4.
Aidha, serikali haijatamka kama James Rugemalira ana fedha haramu na
kama fedha hizo, zikitajwa kuwa za haramu, shule yangu itazirudisha, kwa
kuwa shule yangu haiwezi kupokea fedha iliyo haramu.
5.
“Nilipostaafu kazi UN, Sweden waliniambia kuwa sasa naweza kuendelea
kuomba mchango katika nchi yangu na ni kweli kwamba kadri taifa
linavyokua wapo watu wenye uwezo na wanaoweza kuchangia katika masuala
mbalimbali,” alisema na kuongeza kuwa ndio maana alianza kuomba michango
kwa watu mbalimbali wakiwamo wa ndani ya nchi. Na kutokana na kuomba
mchango, hata Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi aliwahi
kutuchangia Sh milioni 278 kwa kuona umuhimu wa kuendeleza elimu ya
mtoto wa kike na mwaka 2012, ndipo nilipomuomba mchango James Rugemalira
kupitia kampuni yake ya Mabibo akiwa kama ndugu yake.
6.
Nilipomwandikia Rugemalira, alinjibu nitachangiwa, lakini kwa masharti
ya kwamba fedha hizo zipitie Benki ya Mkombozi. Na mimi sikuwa na
akaunti katika benki hiyo na Februari 23 mwaka huu ndipo nilifungua na
haukupita muda mwingi alinipigia na kuniambia kuwa tayari ameshachangia.
Baada ya kupata mchango huo, niliwapigia viongozi wa Bodi ya shule
kuwaeleza kwamba wamepata mchango `babu kubwa’ na alihamisha fedha hizo
na kuzipeleka Benki M kwa ajili ya kulipa mikopo ya shule.
7.
Profesa Tibaijuka anasema: “Nimejitolea maisha yangu kutafuta wafadhili
kwani ada za shule hizo ni kubwa kwani ya Dar es Salaam ni Sh milioni
nne na nusu na ile ya Bukoba ni Sh milioni mbili huku pakiwepo pia
wanafunzi ambao hawalipi ada wakipatiwa ufadhili.”