Tabia ya wanawake kujiuza kwa kisingizio cha kusaka fedha kwa ajili
ya Sikukuu ya Krismasi imewatokea puani wanawake zaidi ya kumi akiwemo
mke wa mtu baada ya kunaswa mawindoni na kutiwa nguvuni.
Makamanda wa Polisi pamoja na kikosi cha OFM wakiwataiti wanawke waliokuwa wakijiuza.
Tukio hilo la aibu lilitokea katika msako maalum wa polisi waliotoa
kolabo kwa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers,
uliofanyika katika eneo ‘korofi’ la ltinga, Msamvu Kata ya Mwembesongo
mkoani hapa, wikiendi iliyopita.
Wanawake hao wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Awali, Kamanda wa OFM mkoani hapa alipokea malalamiko lukuki kutoka
kwa wananchi waishio jirani na eneo hilo waliokuwa wakiwalalamikia
wanawake hao kugeuza vibanda vyao vya simu kuwa gesti na kuvitumia
kufanyia ngono usiku na kuzagaa kwa kondom kila sehemu.
Mke wa mtu (wa kwanza kushoto) akijificha kwa aibu.
Kabla ya msako, OFM iliwashauri kupeleka malalamiko hayo kwenye serikali ya mtaa na polisi.
Kabla ya kufanya oparesheni hiyo, shushushu wetu alifanya upelelezi na
kubaini kwamba ni kweli wanawake hao huvitumia vibanda hivyo kama gesti.
Baada ya kujiridhisha, OFM na jeshi la polisi walipofika eneo hilo
majira ya saa 5:00 usiku na kuwanasa wanawake hao kisha kuwasukumiza
kwenye difenda na kwenda kuwasweka lupango kusubiri sheria ichukue
mkondo wake.
...Wakitupiwa kwenye difenda ili kuchukuliwa hatua za kisheria.
Katika hali ya kushangaza, mmoja wa wanawake hao alikuwa akiomba
msamaha kwa madai kwamba ni mke wa mtu hivyo mumewe akijua ishu hiyo
atamtoa roho.
“Jamani mimi ni mke wa mtu, mume wangu alivyo mkali akijua nimekutwa huko atanimaliza,” alisikika mwanamke huyo.