Korea Kaskazini sasa inataka
uchunguzi wa pamoja na Marekani kufanywa kuhusu wizi wa mtandaoni
uliosababisha kampuni ya Sony Pictures kuahirisha maonyesho ya filamu ya
ucheshi inayomdhihaki raia wa Korea kazkazini Kim Jong-un.
Imesema
kuwa shtuma hizo za shirika la ujasusi nchini marekani FBI kwamba
Pyongyang ndio iliotekeleza uovu huo inaliharibia jina taiafa hilo.
Chombo
rasmi cha habari nchini humo kilimnukuu waziri wa maswala ya kigeni
ambaye jina lake halikutajwa akisema kuwa taifa lake litachukua hatua
kali iwapo Marekani itakataa ombi hilo.
Taifa la Korea Kazkazini hapo awali lilikuwa limeunga mkono uvamizi huo wa kampuni ya Sony likisema kuwa ni kitendo cha haki.
Rais Obama amesema kuwa Marekani itajibu shambulizi hilo la mtandaoni wakati utakapowadia.
Rais wa Korea Kazkazini Kim Jong un.