Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → APIGWA MVUA YA MIAKA 60 JELA, KWA KUTOROSHA TWIGA

APIGWA MVUA YA MIAKA 60 JELA, KWA KUTOROSHA TWIGA

Habari
Friday, 5 December 2014
Aliyetorosha Twiga jela miaka 60
Aliyetorosha Twiga jela miaka 60 HATIMAYE Mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani Kilimanjaro, imemhukumu miaka 60 jela, Kamran Ahmed, raia wa Pakistani kwa kosa la kutorosha
wanyama hai 153, wakiwemo Twiga wanne
Hata hivyo mtuhumiwa huyo mpaka sasa haijulikani alipokimbilia baada ya kutoweka hapa nchini tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi mfawidhi ,Simoni Kobelo, alisema Mahakama hiyo imewaachia huru Watanzania watatu baada ya kutokuwapo kwa ushahidi wa kuwatia hatiani.
Kobelo, alisema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na dhidi ya mtuhumiwa huyo na kumtia hatiani kwa makosa yote manne yaliyowasilishwa na Jamhuri
Kobelo alisema Mahakama imewaachia huru Watanzania watatu ambao ni Hawa
Mang’unyuka, Mathew Kimathi na Michael Odisha Mrutu kwasababu ya Jamhuri kushindwa kuthibitisha ushahidi stahiki.
Alisema ushahidi uliowasilishwa haukuonesha kuwaunganisha washitakiwa hao moja kwa moja na kosa la kusafirisha wanyama hai nje ya nchi.
Katika hukumu hiyo, Kamran, alikutwa na makosa manne, kushiriki na kula
njama ya kutenda uhalifu kinyume cha kifungu 57 (1), sehemu ya 4(1),
sura ya kwanza ya kosa la uhujumu uchumi na kushiriki utoroshaji wa
wanyama hai wenye thamani ya shilingi milioni 170.5
Kosa la pili ni kufanya biashara ya kukamata na kusafirisha wanyama
hai wakiwemo Twiga, Chui, Pofu, Punda Milia, Swala ndege wa aina mbalimbali, Duma, Nyati bila leseni.
Kosa la tatu ni kukutwa na Nyara za Serikali katika uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Novemba 26, mwaka 2010 na kosa la nne ni la
kuisababishia serikali hasara ya Dola 113.7 kwa kufanya biashara
kinyume cha sheria.
Kuhusu mshitkakiwa wa pili Hawa Mang’unyuka anayetajwa kuwa mmiliki wa
kampuni ya Harm Marketing na Luwego Bird Trappers, inayodaiwa leseni
yake kutumika kuhalalisha ukamataji na utoroshaji huo, Hakimu Kobelo
alisema kwa mujibu wa vielelezo vilivyowasilishwa kampuni ya Hawa, ilipewa kibali halali cha kukamata wanyama hai na mamlaka husika
Washitakiwa Mathew Kimathi na Michael Mrutu,
Kobelo alisema kwa sababu hakuna sehemu yoyote inayoonesha ushiriki
wao katika utoroshaji zaidi kutekeleza wajibu wao kama walivyoekezwa
na wakuu wao wa kazi kipindi hicho.
Machi mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi, ilitoa amri ya
kukamatwa ndani ya saa 24, mshitakiwa namba moja(Kamran) baada ya
kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo kwa zaidi ya vikao viwili
mfululizo.
Amri ya kukamatwa kwa raia huyo wa Pakstani ilitolewa Machi 23 mwaka
huu Hakimu Kobelo baada ya kutoa hati ya kukamatwa kwa raia huyo
kufuatia ombi la mawakili wa upande wa Jamhuri kuomba hati hiyo
kutolewa kutokana mshitakiwa kutofika mahakamani.
Kutoroka kwa mtuhumiwa huyo kuliilazimu Mahakama kutoa hati ya hati ya
kukamatwa (Arrest warrant) kwa wadhamini wawili wa mshitakiwa huyo
ambaye ilidaiwa tayari ametorokea nje ya nchi.
Wadhamini waliotajwa mahakamani hapo , Jackson Kimambo na Peter
Temba,ambao awali walipewa wito wa kufika mahakamani hapo kutoa
uthibitisho wa uwepo wao ikiwa ni pamoja na kusaidia mahakama kumpata
mshitakiwa huyo kama walivyosaini katika hati yao ya udhamini.
Hata hivyo Mdhamini mmoja Peter Temba ndiye alikamatwa na kuhukumiwa
kifungo jela na Jackson Kimambo hakukamatwa .
Kesi hiyo iliyokuwa na mvuto wa kitaifa na kimataifa ,Novemba 25 mwaka
2010 watuhumiwa hao wanadaiwa kula njama ya kusafirisha nje ya nchi
zaidi ya wanyama hai na ndege 100 wakiwemo Twiga wanne ambao thamani
yake inakadiliwa kufikia dola za marekani 113,715 .
Kamran amebainika kutenda kosa la kusafirisha wanyama hai kwenda Doha,
nchini Oman kwa kutumia ndege aina ya C.17 yenye nambari AMA/MAB mali
ya shirika la Qatar Airways.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka ni kwamba wanyama hao, walisafirisha
kwenda Falme za Kiarabu baada ya kupita vizuizi yakiwamo mageti ya
namba 5A na 5B katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • Chuo kikuu cha ardhi ARU chatoa zawadi kwa wanafunzi 30, mmoja, ambae ni muhitimu wa masomo ya surveying aibuka na machine ya millioni 35
    CHUO Kikuu Ardhi (ARU), kimewazawadia wanafuzi 130 wa masomo mbalimbali zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 60 kutokana n...
  • Ajali ya gari huko south B kenya
    There was a bizarre accident today morning in Hazina Estate, South B involving a Range Rover that crashed into 7 vehicles. The Ran...
  • Arsenal yamlenga Kramer anaechezea klabu ya Borussia Monchengladbach
    Arsenal wako tayari kutoa p...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • MAREKANI YAITUPIA LAWAMA KOREA KASKAZINI
    Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala ...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis