Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → CCM KUTOICHUKULIA HATUA AKAUNTI YA ESCROW

CCM KUTOICHUKULIA HATUA AKAUNTI YA ESCROW

Habari
Friday, 5 December 2014





Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema kuwa CCM haina mpango wa kuchukua hatua zozote dhidi ya wote waliotajwa kuhusika na kashfa hiyo kwa sababu chama hicho hakijawahi kuwajadili kwa jambo hilo ambalo siyo la chama chao bali ni la Bunge la Tanzania.

“Suala hili lipo chini ya Bunge na hivyo chama hakijaingilia kati na kuchukua hatua wabunge wake waliotajwa,” alisema Nape. Aliongeza kuwa chama hakiwezi kuchukua hatua zozote dhidi ya wabunge wake waliobainika kula fedha hizo kwani suala hilo halijawahi kufikishwa kwenye vikao vyao. “Hatujawachukulia hatua (waliotajwa), wala hatuna mpango wa kuwachukulia hatua kwa sababu suala hili haliko ndani ya CCM... liko ndani ya bunge, labda kama litaingia ndani ya chama ndiyo tutalitolea maamuzi,” alisema Nape.

Kauli ya Nape imekuja siku chache baada ya chama hicho kutoa msimamo wake dhidi ya wabunge wa chama hicho waliohusika katika sakata hilo kuwa bunge lichukue hatua stahiki. Nape, akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika ziara ya kukagua, kuhimiza na kusukuma utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010/15 mkoani Mtwara, walisema kila aliyehusika katika kashfa hiyo, abebe msalaba wake.

Nape alisema chama hakiwezi kulea maovu yanayofanywa kinyume na kanuni na taratibu za chama hicho, hivyo kama bunge limebaini waliokiuka maadili wachukuliwe hatua stahiki dhidi yao. Kwa upande wake Kinana alisema muda wa kulindana na kubebana ndani ya chama umeisha na anayekiuka taratibu na kanuni za chama hicho awajibishwe na akishindikana achie ngazi.

Wabunge kadhaa kutoka CCM wakiwamo mawaziri Sospeter Muhongo wa Nishati na Madini na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ni miongoni mwa vigogo waliotajwa kuhusika na kashfa hiyo na hivyo Bunge kuazimia kuwa waondoshwe.

Wabunge wengine wa CCM waliohusishwa na kashfa hiyo na kutakiwa kuondolewa kwenye nafasi zao za uenyekiti wa kamati za Bunge ni Mbunge wa Bariadi Mashariki anayeongoza Kamati ya Bajeti, Andrew Chenge , Mbunge wa Sengerema, Wiliam Ngeleja (Sheria, Katiba na Utawala) na Mbunge wa Lupa anayeongoza kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa.






Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Takribani watu 15 wapata upofu baada ya upasuaji nchini India
    Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji walisema walishindwa kuona tena baada ya kuondoa bandeji kwenye macho yao Maafisa wa utawala nchini Indiaa w...
  • Familia ya mateka yasihi Al Qaeda kumwachilia
    Marekani imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen. ...
  • Ona kilichotokea kwa jimama hili kipindi lina jaribu kucheza jirani na swimming pool.Noii huko Kenya mida ya jana jioni
       
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.
      OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semi...
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL
  • KAULI YA UHURU KWENYE MTANDAOWA KIJAMII (TWITTER) KENYATTA HII HAPA
    Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto. Baadhi w...
  • Maandano zidi ya kutupiliwa mbali kwa kesi ya afisa polisi mjini New York
    Maandamano mjini New York Waandamanaji wameingia katika barabara za miji mingi Nchini Marekani kwa usiku wa pili mtawalia, kupinga maamu...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • MORE THAN 10,000 GRADUATES TURN UP FOR SEVENTY JOB VACANCIES IN DAR ES SLAAM.
    According to the list of names seen by The Guardian yesterday morning, the department listed 10,816 candidates to perform the interview tha...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis