Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, kesho Jumamosi Desemba 6 anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi Katika Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB).

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, kesho Jumamosi Desemba 6 anatarajiwa Kuwa mgeni rasmi Katika Mahafali ya Pili ya Chuo Kikuu Cha Bagamoyo (UB).

Habari
Friday, 5 December 2014



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo kwa vyombo vya Habari Dar Es
Salaam,  na Ofisa Habari wa  ( UB), Happiness Katabazi, inasema Kuwa
Membe ndiye Atakuwa mgeni rasmi Katika mahafali hayo ambayo yatafanyika Katika
Hoteli ya Kiromo  View Resort  kijijini Kiromo Wilayani Bagamoyo,Mkoani
Pwani.




Katabazi alisema jumla ya wahitimu 99 wanatarajiwa kutunukiwa Vyeti Katika
ngazi ya Shahada ya Uzamili, Shahada ya Kwanza, Diploma,  na cheti.




Wakati huo huo , Juzi Makamu wa Rais  Dk.Mohammed Gharib Bilal alishindwa
kuhudhuria sherehe za uwekwaji  wa jiwe la Msingi wa makazi ya kudumu ya
UB ikiwa ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa makao makuu ya UB kijijini hapo
ambapo ujenzi ukikamilia majengo hayo yatakuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya
wanafunzi 5000, yaliyopaswa yafanyike Katika kijijini Cha Kiromo ,Bagamoyo
Mkoani Pwani kwasababu alikuwa amebanwa na majukumu mengine ya Kitaifa na
akaomba apangiwe tarehe nyingine ya kuja kuweka jiwe Hilo la Msingi.




Akizungumza na waandishi wa Habari Katika kijijini Kiromo Juzi wakati
akiiarisha sherehe za Utiaji wa jiwe la Msingi , Makamu Mkuu wa UB, Profesa
Costa Ricky Mahalu alitoa historia fupi la shamba Hilo lililopo Kijijini Kiromo
Alisema  familia yake ililinunua rasmi Agosti 26 Mwaka 2003.





Profesa Mahalu alisema Katika shamba Hilo familia yake imeamua kukata heka 100
na kuzitoa kwa UB ili UB iweze kujenga makazi yake ya kufumu katika Kijiji cha
Kiromo na kwamba heka nyingine zilizosalia familia yake itazitoa  kwa
Taasisi nyingine za elimu ya juu  na kwamba Tayari Taasisi nne za elimu ya
juu ikiwemo Chuo Kikuu Kimoja Cha kigeni kimeishaonyesha nia ya kutaka Kuja
Kujenga Taasisi yake ya elimu Katika shamba Hilo.




Profesa Mahalu Alisema shamba hilo kabla familia yake haijalinunua lilikuwa
likimilikiwa na lililokuwa shirika la Serikali la NAFCO na baada ya kufirisika
mwaka 1990  lilichukuliwa na LART  ambaye alikuwa na jukumu la
kuchukua  kuuza Mashitaka ya serikali yalikuwa na matatizo ya kifedha.




' LART ikamkabidhi  kampuni ya PHLLIP&Ltd  iliyauza mashamba
matatu  ya NAFCO  yaliyopo Kiromo. Hayo mashamba matatu ,Moja
iliuziwa familia ya Mahalu na mkataba wa mauzo wa shamba Hilo la Mahalu na LART
ulisainiwa Agosti 26 Mwaka 2903  na baada ya hapo  umiliki wa
shamba  unachukuliwa  na familia ya Mahalu kwa mujibu wa Sheria.'
Alisema Balozi Mahalu.




Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • Chuo kikuu cha ardhi ARU chatoa zawadi kwa wanafunzi 30, mmoja, ambae ni muhitimu wa masomo ya surveying aibuka na machine ya millioni 35
    CHUO Kikuu Ardhi (ARU), kimewazawadia wanafuzi 130 wa masomo mbalimbali zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 60 kutokana n...
  • Ajali ya gari huko south B kenya
    There was a bizarre accident today morning in Hazina Estate, South B involving a Range Rover that crashed into 7 vehicles. The Ran...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • Arsenal yamlenga Kramer anaechezea klabu ya Borussia Monchengladbach
    Arsenal wako tayari kutoa p...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • MAREKANI YAITUPIA LAWAMA KOREA KASKAZINI
    Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala ...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis