Sekta ya bidhaa za urembo, pamoja na urembeshaji wa watu inanawiri nchini Afrika Kusini.Na sio Afrika Kusini pekee bali barani Afrika kote.
Mwaka jana pekee sekta hiyo ilikuwa kwa asilimia kumi.Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg Milton Nkosi aligundua kuhusu sekta hiyo ya manukato na bidhaa za urembo kwa wanaume pamoja na wanaume kujipamba sawa na wanavyofanya wanawake.
Sura ya bara la Afrika inabadilika. Kumekuwa na hii kasumba ya wanaume kujipamba kwenda katika saluni, kusafishwa miguu, mikono, makucha , ngozi na kufanyiwa shughuli zinazosifika tu kwa wanawake.
Wadadisi wanasema sekta hii imeendelea kukuwa hasa mwaka jana.
Kuna bidhaa nyingi tu za kuwapamba wanaume katika maduka na saluni nyingi.
Hilo ni dhahiri katika saluni ya wanaume mjini Sandtone am,bayo kazi yake ni kuwafanya wanaume kupendeza. Zamani kidogo wanaume walikuwa wakienda kwa kinyozi kunyolewa nywele na ndevu na kupaka tu 'spirit' ili kukabiliana na vidonda vyovyote kwenye ngozi.
Leo utawapata wanaume wameweka viganja vyao ndani ya maji ya vuguvugu, makucha yakioshwa huku nywele zao zikinyolewa na huku wakipambwa nyuso zao. Hio ndio imekuwa starehe ya baadhi ya wanaume siku hizi kwenye saluni ambako pia utapata wanawake wanapambwa.
Lakini je kwa nini wanaume wengi siku hizi wanakwenda kwenye saluni kupambwa, uraibu ambao unajulikana kuwa wa wanawake? na je nini kiliwafanyikia wanaume wa zamani waliokuwa wanajulikana kuwa wenye nguvu ambao kwao ilikuwa kuoga kwa maji baridi na kwenda kwa kazi zao?
Baadhi ya wataalamu wanasema siku hizi angalau watu wanapata mishahara mizuri na hivyo wana pesa angalau kidogo za kutumia kwa mapambo.
Misharaha hio inawaruhusu kujifakhirisha. Bara la Afrika linafuata mkondo huohuo.
Je wewe unakubali wanaume kwenda kupambwa kama wanawake kwenye saluni?