MKAZI wa kitongoji cha Ngena, wilayani hapa, Watsoni Mwakiposa (80) amefariki dunia baada ya kupigwa na radi akielekea kwenye kilabu cha pombe.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, William Ndille, alisema mzee huyo alikutwa na umauti jana majira ya saa 1:00 usiku wakati akielekea katika kilabu cha pombe za kienyeji.
Akielezea tukio hilo, Ndille alisema mzee huyo alikuwa na mauti akiwa njiani kuelekea katika kilabu cha pombe ambapo kulikuwa na mvua iliyoambatana na radi.
Ndille alisema baada ya tukio hilo waliliarifu Jeshi la Polisi wilayani humo ambao walifika eneo hilo na kuupeleka mwili wa mzee huyo katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa uchunguzi zaidi.
Alisema kwa kuwa tukio hilo ni la pili, aliwataka wakazi wa kijiji hicho kupunguza miti iliyozidi katika eneo hilo ili kuepusha madhara.