Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → Askari akamatwa ugoni,wawili wajeruhiwa kwenye mapigano

Askari akamatwa ugoni,wawili wajeruhiwa kwenye mapigano

Habari
Friday, 5 December 2014
WAKAZI wawili wilayani hapa, wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Kahama Mkoa wa Shinyanga baada ya kujeruhiwa katika mapigano kati yao na askari Polisi, baada ya kumshika ugoni mmoja wa askari katika hoteli moja maarufu mjini hapa.
Tukio hilo lilitokea juzi usiku baada ya mmoja wa vijana hao, kumkuta askari akijivinjari na mkewe, ndipo alipomshirikisha ndugu yake na kuibuka mapigano makali ya kurushiana makonde yaliyosababisha baadhi yao kujeruhiana vibaya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo limetokea baada ya askari, Sajenti Edward kufumaniwa akiwa na mke wa mmoja wa vijana hao aliyejulikana kwa jina la Paschal Matonange (26).
Kamugisha, alisema baada ya kufumaniwa akiwa na mwanamke huyo chumbani, vijana hao walianza kumshushia kipigo huku wakimpiga picha akiwa uchi, hali iliyosababisha vurugu kwenye hoteli hiyo iliyopo nje kidogo na mji wa Kahama.
Kamanda huyo, alisema baada ya vurugu hizo wasamalia wema walijaa eneo hilo na baadhi yao kupiga simu kituo cha polisi ambako askari walifika kujaribu kutuliza vurugu hizo bila mafanikio.
Alisema katika kutuliza ghasia hizo, yalizuka mapigano makubwa kati ya vijana hao na askari polisi, hali iliyosababisha kujeruhiwa kwa baadhi ya askari na vijana hao ambao wamelazwa katika hospitali ya Halmashauri ya Mji.
Aidha, waliolazwa ni pamoja Marco Matonange (27), na mdogo wake Paschal Matonange ambaye ndie mme wa mwanamke huyo aliyefumaniwa akiwa na askari.
Hata hivyo, Kamugisha alisema jeshi lake litamchukulia hatua za kinidhamu askari aliyefumaniwa na mke wa mtu, ambaye pia yumo kwenye kikosi maalumu cha kufanya uchunguzi wa makosa ya jinai, kwa kuwa kufanya hivyo ni utovu wa nidhamu.
“Kimsingi sisi kama polisi hatuhusiki na masuala ya ugoni na askari kwenda pale kwenye tukio hawakwenda kwa ajili ya kufumania, bali walikwenda kwa ajili ya kutuliza ghasia lakini ilikuwa ni kazi kuwakamata hao vijana, mpaka sasa pamoja na wao kujeruhiwa pia baadhi ya askari wamejeruhiwa,” alisema Kamugisha.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, alisema suala hilo  kwa kutumia nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, analifanyia kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.
“Ni kweli tukio hilo ninalo, vyombo vyangu vya usalama vinalifanyia kazi ikiwemo uchunguzi ili kujua hasa chanzo chake kilichosababisha kuwepo kwa mapigano hayo,” alisema Mpesya ingawa mmoja wa majeruhi hao alidai mkuu huyo ndie aliyewakoa wakati wakipata kipigo kituo cha polisi baada ya kupiga simu kwa mkuu wa polisi Wilaya (OCD).
Akizungumzia tukio hilo katika Hospitali ya Mji wa Kahama, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, aliyefika kuwapa pole majeruhi, alisema jeshi la polisi linatakiwa kufanya kazi kwa misingi ya sheria.
Mgeja, alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi, (IGP), Ernest Mangu, kuhakikisha anafanya uchambuzi wa askari wake wasiokuwa na nidhamu ambao hutekeleza majukumu yao kwa vitisho, hali inayosababisha wananchi kukosa imani nao.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Mji wa Kahama, Deogratius Nyaga, alisema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • Chuo kikuu cha ardhi ARU chatoa zawadi kwa wanafunzi 30, mmoja, ambae ni muhitimu wa masomo ya surveying aibuka na machine ya millioni 35
    CHUO Kikuu Ardhi (ARU), kimewazawadia wanafuzi 130 wa masomo mbalimbali zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 60 kutokana n...
  • Ajali ya gari huko south B kenya
    There was a bizarre accident today morning in Hazina Estate, South B involving a Range Rover that crashed into 7 vehicles. The Ran...
  • Arsenal yamlenga Kramer anaechezea klabu ya Borussia Monchengladbach
    Arsenal wako tayari kutoa p...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • MAREKANI YAITUPIA LAWAMA KOREA KASKAZINI
    Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala ...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis