Muigizaji
Salma Jabu aka Nisha ambaye hufanya kazi na kampuni hiyo ameiambia
Bongo5 kuwa imewabidi wafanye hivyo ili kuwawezesha watanzania wote kuwa
na uwezo wa kupata kopi halisi za kuacha kununua feki.
“Kweli
tumekaa na Steps, tunaona njia pekee ya kupambana na waharamia wa kazi
zetu ni kupunguza bei ya filamu zetu,” amesema Nisha. “Kuanzia mwezi
February 2015, filamu zitaanza kuuzwa kwa bei ya shilingi 1,500 za
kitanzania badala ya 3,000 kama bei ya rejereja. Kwahiyo kama utakuwa
unahitaji mbili ina maana utatoa shilingi 3,000. Tumeshuka ili
kumshawishi mtanzania kuacha kununuA filamu za mitaani kwa bei ya 1,000,
ni bora tupunguze hii filamu yetu orijino iliyokuwa inauzwa 3,000
tupunguze mpaka 1,500 ili aweze kuinunua,” ameongeza.
“Kwahiyo
kama alikuwa anahitaji mbili, anatoa shilingi 3,000 badala ya 6,000
ambayo ilikuwa bei ya mwanzo. Kwahiyo sisi kama wasanii tumeona bora
tuuze kwa bei hiyo tukiwa tuna imani tutauza filamu nyingi na tutakuwa
tunapata faida.”
Pia
Nisha amewataka watanzania kumuunga mkono kwa kununua filamu yake mpya,
‘Hakuna Matata’ inayotarajiwa kutoka December 22 mwaka huu.