Kampuni ya BMW imezindua kifaa ambacho kinawezesha gari lako kujiegesha lenyewe..
Hakuna kitu kibaya kama kusahau ulikoegesha gari lako katika jengo la kuegeshea magari lenye goraf nyingi.Lakini
hivi karibuni hautahihajika kupanda gorofa kutafuta gari lako kwani
kampuni ya kutengeza magari ya BMW, imetangaza kuzindia kifuaa ambacho
kinaweza kuyawezesha magari ya kampuni hio kujiegesha yenyewe kwa
kubonyeza tu kifaa hicho.
Hata hivyo dereva wa gari hilo
atalazimika kuvaa saa ya Smartphone mkononi ambayo ataibonyeza na
kuiamrisha kwa sauti gari hilo kwenda kujiegesha.
Gari hilo kwa amri ya dereva litatoka liliko baada ya dereva kushuka
na kwenda lenyewe kwa kuhesabu muda utakalichukua kwenda kutafuta sehemu
ya kujiegesha.
Tawi la kampuni ya BMW mjini Munich, Ujerumani limezindua teknolojia hio ambayo inawezesha gari kujiegesha lenyewe.
Gari
hilo linatumia miale ya Leser iliyo kujitafutia ramani ya jengo ambalo
lipo. Dereva anaweza kuliamrisha gari hilo kwenda kujiegesha kwa kutumia
Smartphone.
Dereva anaporejea kutoka alikokwenda, analiamrisha gari kutoka sehemu ilikojiegesha na kuja kumchukua dereva.
Teknolojia hio inajulikana kama ' Remote Valet Parking Assistant,' na inafanyiwa majaribio kwenye gari la BMW i3.
Badala
ya kutumia GPS, teknolojia hio inatumia miale ya Laser ambayo hutengeza
ramani inayolisaidia gari hilo kutafuta sehemu ya kwenda kujiegesha.Teknolojia
hiyo inaiwezesha gari hilo kuona njia na nafasi ya kujiegeshea na pia
kuona vizingiti mfano kama magari ambayo hayajaegeshwa vyema.
Kwa
mujibi wa waliotengeza gari hilo, linaweza kujitafutia nafasi ya
kujiegesha na hata kuweza kutambua sehemu ambako kuna nafasi.Teknolojia hio inatengezwa sambamba na teknolojia nyinginezo zitakazoweza kuzuia gari hilo kugongana na magari mengine.
Gari hili linaweza kujiegesha lenyewe kwa kutumia saa ya mkononi ambayo inabonyezwa na dereva.