Katika hali isiyo ya kawaida mzee mwenye umri wa miaka 80 ameomba msaada wa serikali kuingilia kati na kuzuia mtoto wake kuuza shamba lake ambalo alilichimba zaidi ya miaka 35 iliyopita.
Shamba lenyewe lipo Mathira Kenya ambapo mzee analalamika kwamba mtoto wake wa kiume amekuwa akiuza sehemu ya shamba hilo kidogo kidogo.
Amesema tofauti na matarajio yake alikuwa akiamini Mtoto huyo angekuja kumsaidia uzeeni lakini ndio amekuwa akiuza shamba hilo bila ruhusa yake na kuhofia kuwa anaweza kuuza hata kipande cha shamba ambacho amechijimbia kaburi lake.
Hii ni taarifa niliyoirekodi kutoka kituo cha WBS TV unaweza kuisikiliza hapa kwa kubonyeza play.