Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → Wanafunzi wafundishwe ujasiriamali mapema

Wanafunzi wafundishwe ujasiriamali mapema

Habari
Tuesday, 25 November 2014


Kuna kaulimbiu za shule mbalimbali ambazo zimekuwa zikionekana katika nyaraka za shule.
Kwa mfano, unaweza utakutana na misemo kama “Elimu ni Maisha,” “Elimu ni Ufunguo wa Maisha” na nyingine nyingi.
Lengo la misemo hii ni kuonyesha jinsi taasisi husika inavyowaandaa watu wake kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Kwa maana hiyo waandaliwa hao wanatakiwa wawe wakala wazuri wa shule zao uko waendako kwa kufanana na kaulimbiu hizo.
Pamoja na kwamba taasisi hizo huwa na malengo mazuri, suala la utekelezaji wa malengo hayo huwa ni changamoto.
Nasema ni changamoto kwa sababu tunaona jinsi idadi kubwa ya wahitimu wanaotoka katika taasisi wasivyohusiana na kaulimbiu za taasisi zao.
Funzo tunalolipata hapa ni kuwa hatuna budi kusimamia na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu tunazoziamini.
Utekelezaji wake kwa vitendo utazaa matunda yaliyokusudiwa. Katika elimu ya ujasiriamali, matendo ndicho kitu cha thamani kubwa kuliko maneno yatokayo katika mdomo wa mtu.
Wataalamu wa elimu ya ujasiriamali kama vile Garavan na Barra wanasema kuwa madhumuni ye elimu ya ujasiriamali ni pamoja na kupata maarifa stahiki ya ujasiriamali.
Pia, ni kupata ujuzi utakaosaidia kutumia mbinu mbalimbali za uchambuzi wa masuala ya biashara. Vilevile ni kubainisha na kuchochea ujasiriamali.
Madhumuni mengine ni kujenga na kuendeleza mambo yanayowagusa wajasiriamali ikiwa ni pamoja na kusaidia masuala yote yanayohusiana na ujasiriamali.
Kama haya yakifanyika katika viwango vyetu vya elimu itakuwa rahisi kwa Taifa letu kuwa na maendeleo endelevu. Tutakuwa tumejenga watu wenye maarifa na ujuzi wa kufanya kazi kwa manufaa yao na taifa lao

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • Burkina Faso leaders agree transitional framework following the meeting held in Ouagadougou
      The blueprint for transition was agreed unanimously at the meeting in Ouagadougou A framework for a transitional government ...
  • John Doar, a civil rights lawyer who was a key figure in the struggle against racial segregation in the US, has died aged 92.
    John Doar was awarded the Presidential Medal of Freedom in 2012 Mr Doar dealt with some of the most prominent civil rights ca...
  • Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.
      OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semi...
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis