Mwanafalsafa

  • HOME
Home → News and Updates → Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ametunukiwa Tuzo ya Mafanikio Katika Utumishi wa Umma kutokana na mchango alioutoa kwenye uchumi wakati wa utawala wake.

Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa ametunukiwa Tuzo ya Mafanikio Katika Utumishi wa Umma kutokana na mchango alioutoa kwenye uchumi wakati wa utawala wake.

News and Updates
Tuesday, 25 November 2014


 
Kwa ufupi
Kufanya kazi bila kuchoka, kusisitiza uwazi na ukweli katika kuboresha uchumi katika kipindi chake kwampaisha.

Dar es Salaam. 
Akikabidhi tuzo hiyo iliyotolewa na Umoja wa Watendaji Wakuu (CEOrt) juzi, Balozi Ami Mbungwe alisema Rais Mkapa ametoa mchango mkubwa katika kuimarisha utawala bora na uwazi ndani na nje ya nchi.
“Alifanya kazi bila kuchoka, akisisitiza ukweli na uwazi wakati wa kipindi cha kuboresho sera za uchumi. Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye masuala ya uwekezaji,” alisema.
Akipokea tuzo hiyo katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali, Mkapa alisema ameipokea kwa niaba ya wananchi ambao walikubali kupokea mabadiliko ya kiuchumi.
“Maono na mipango yangu wakati ule ilikuwa kuweka mazingira rafiki ambayo yangelinda haki za sekta binafsi, kuhakikisha mfumo wa fedha unakuwa rafiki kwa biashara, kukusanya mapato na kulipa madeni ya umma ili kufan uchumi uwe imara,” alisema.
Mkapa alisema hata alipogundua kuwa ujasiriamali unabanwa na kanuni zisizo sahihi, kodi kubwa, kukosekana kwa ushindani halali, alihakikisha anaondoa vikwazo na kuongeza ushindani wa kibiashara.
Alisema baadhi ya watu walilalamikia uboreshaji kwa madai kuwa sekta binafsi iligeuka sehemu ya kuficha kampuni za kigeni.
Mwenyekiti wa CEOrt, Ali Mufuruki alisema tuzo hiyo mwaka jana ilitolewa kwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, kutokana na mchango wake kwenye biashara huria, vyombo vya habari na kuanzisha siasa za vyama vingi.
Mufuruki alisema nishani hiyo haitolewi tu kwa viongozi wa kitaifa au marais, bali inakwenda kwa mtu yeyote ambaye mchango wake unatambuliwa na jamii.
Alisema kiongozi huyo aliingia madarakani wakati nchini ikiwa katika hali mbaya kiuchumi, lakini katika miaka miwili aliteremsha mfumko wa bei kutoka asilimia 30 mpaka nne.
“Aliweza kusimamisha kuporomoka kwa thamani ya shilingi, alihakikisha Serikali inatumia fedha ambayo inakusanya kutokana na mapato yake ya ndani. alisema Mufuruki.
Katika hafla hiyo, Mtendaji Mkuu kutoka Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omari Issa alipewa tuzo ya Mwaka ya Utumishi wa Serikali kutokana na mchango wake alioutoa kwenye sekta binafsi nchini.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Kwaninii serikali imewekeza katika siasa na imesahau wakulima ?
      Hata hivyo, wakulima wamekwazwa na kodi nyingi wanazotozwa kwa kila gunia inapotokea wakauza sehemu ya ...
  • The captain of the South Korean ferry which sank in April has been found guilty of gross negligence and sentenced to 36 years in prison
    Lee was found not guilty of the charge of homicide through wilful negligence The Sewol ferry was carrying 476 people when it ...
  • One Direction win big at Glasgow ceremony,MTV EMA awards.
    Brightly coloured signage adorning Buchanan Street, giant MTV statues dotted around the city centre, and specially created light shows d...
  • USHIRIKA WAHUSISHWA KWENYE KISA HIKI CHA MWANAMAMA KUMDUMBUKIZA MTOTO KISIMANI
    Hali ya sintofahamu imeibuka katika mtaa wa Azimio, kata ya Kihonda katika manispaa ya Morogoro, baada ya mwanamke mmoja, Veronic...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Aiburuza serikali mahakamani.
    ameshinda rufaa ya maombi ya marejeo yaliyowasilishwa na Serikali kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kumfutia mashitaka ya ugai...
  • UNAMFAHAMU MWANAUME MMBEYA ? JE WATU WANAMGUMZIAJE ? KAMA WEWE MTU MZIMA TUPE MAONI YAKO
    Sekta ya bidhaa za urembo, pamoja na urembeshaji wa watu inanawiri nchini Afrika Kusini.Na sio Afrika Kusini pekee bali barani Afri...
  • Ukistaajabu ya Mussa ?Nusu ya sura yake inafanana na binadamu na Nusu nyingine inafanana na CHURA, ni mtoto aliye zaliwa huko dodoma
    MKAZI  wa kijiji cha Chibwechangula –Behelo katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ruth Matonya (26) amejifungua mtoto wa ajabu ambaye nus...
  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis