Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → Maonyesho ya elimu yaweza kuibua mambo mazuri zaidi

Maonyesho ya elimu yaweza kuibua mambo mazuri zaidi

Habari
Tuesday, 25 November 2014
KATIKA kutatua baadhi ya changamoto zinazohusu masuala ya elimu kwa vijana nchini, imebainika hali hiyo wakati mwingine inachangiwa na sekta husika kutokuwa na mawasiliano ya karibu.
Hata hivyo, baadhi ya wadau baada ya kubaini changamoto hizo hivi sasa wanajipanga kujenga mtandao katika sekta zote za elimu na kuwa kitu kimoja.
Akizungumzia hali hiyo, Mkurugezi Mkuu wa Global Education Link LTD (Gel), Abdulmalik Mollel, anasema ili kuzipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto hizi wameandaa maeonyesho ya elimu.
Maonyesho hayo ya kwanza na kimataifa ambayo yanatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, kuanzia Desemba 10 hadi 14 mwaka huu.
Anasema maonyesho hayo yanaandaliwa na kuratibiwa na Global Education Link Ltd (Gel), kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
“Maonyesho haya yanatarajiwa kuvuta washiriki zaidi 500 na watembeleaji zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
“Kaulimbiu ya maonyesho haya ni ‘Kuweka jitihada za pamoja katika kuboresha mfumo wa elimu Tanzania ni njia thabiti ya kuleta maendeleo endelevu katika taifa,” anasema Mollel.
Mollel anasema lengo kuu la maonyesho hayo ni kuwaunganisha wadau wote wa elimu kwa pamoja, ili waweza kutoa huduma kwa wananchi na kuwaelimisha juu ya mambo muhimu yaliyopo katika sekta husika.
Anafafanua kwa kuwataja wadau wa sekta binafsi wa elimu ambao ni mifuko ya pensheni, wachapishaji wa vifaa vya shule, taasisi za kielimu.
Nyingine ni asasi za kielimu, vyuo vikuu vya elimu vya ndani na nje ya nchi, shule za awali na sekondari pamoja na wadau wengine, akibainisha kuwa itakuwa ni sehemu yao kuuza bidhaa zao mbele ya wadau lengwa.
Mollel anasema maonyesho hayo yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa kuongeza ushindani katika sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (RBN).
“Warsha kama hizi za elimu zina lengo la kuhamasisha ubora wa elimu na uchumi kutokana na hali halisi ya nchi yetu,”anasema Mollel.
Anataja baadhi ya faida katika ushiriki wa asasi mbalimbali nchini kwa uchache ni pamoja na kutengeneza ushindani wa bidhaa za elimu katika sekta za elimu nchini zitakazosababisha elimu yenye tija na kwenda na soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Faida nyingine ni njia pekee ya kubadilishana na kuonyeshana ujuzi kutoka shule moja hadi nyingine, na wananchi watapata fursa ya kupata nafasi ya shule au chuo na kuweza kupata taarifa kwa uwazi juu ya elimu ya ndani katika eneo moja bila urasimu ndani ya eneo husika.
Pia wananchi watapata nafasi ya kuchagua kozi na kuzielewa vizuri kabla ya kufanya maamuzi yao ya mwisho na wanafunzi wazazi watapata ushauri kuhusu kozi mbalimbali wanazotaka watoto wao wakasome.
“Tume ya Vyuo Vikuu, sekta mbalimbali za elimu, benki na washiriki wengine toka nje ya nchi zitapata nafasi ya kutoa mada na kuuza biashara zao kwa wananchi zinazohusiana na bidhaa za elimu,”anaeleza Mollel.
Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade,  Jacqueline Maleko, anasema ili kuweza kufanya vizuri katika mambo mbalimbali yanayohusu biashara ni lazima kuwa na elimu ya kutosha, hivyo maonyesho hayo yatawasaidia wanafunzi kupata elimu bora itakayowasaidia kufanya biashara zao kwa umakini.
“Kama sekta ya elimu hatutaijengea mazingira mazuri na vijana wakaweza kujiari, kuna hatari hapo baadaye nchi ikaja kuingia katika mifarakano makubwa.
“Wakati vijana wa mataifa ya wenzetu walipata nafasi mbalimbali za kazi hapa nchini wa kwetu wanakosa kwa madai kuwa hawaajiriki,”anasema Jacqueline.
Anasema vijana wengi wa nje wanapata ajira nchini kwa sababu nchi zao zimekuwa zikifanya vizuri katika kujitangaza kimataifa.
“Sisi tunavyo vyuo vikuu ambavyo ni vizuri, lakini tunashindwa kuvitangaza," anasema Jacqueline.
Hata hivyo, Maleko amewataka wanafunzi pamoja na wazazi kujitokeza kwa wingi katika maonyesho.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • Burkina Faso leaders agree transitional framework following the meeting held in Ouagadougou
      The blueprint for transition was agreed unanimously at the meeting in Ouagadougou A framework for a transitional government ...
  • John Doar, a civil rights lawyer who was a key figure in the struggle against racial segregation in the US, has died aged 92.
    John Doar was awarded the Presidential Medal of Freedom in 2012 Mr Doar dealt with some of the most prominent civil rights ca...
  • Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.
      OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semi...
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis