Mwanafalsafa

  • HOME
Home → News → Kwaninii serikali imewekeza katika siasa na imesahau wakulima ?

Kwaninii serikali imewekeza katika siasa na imesahau wakulima ?

News
Tuesday, 25 November 2014


 
Hata hivyo, wakulima wamekwazwa na kodi nyingi wanazotozwa kwa kila gunia inapotokea wakauza sehemu ya mahindi yao yaliyolundikana. Malipo hayo ni kama kodi ya halmashauri, gharama za kuhifadhi mahindi ghalani, ubebaji wakati wa kushusha mahindi kituoni, kuchekecha mahindi, kuondoa uchafu na kupeleka kwenye mizani. 

Siyo siri kuwa, iwapo fedha inazotumia katika mambo ya kisiasa zingeelekezwa kwenye kilimo, wakulima wangejikomboa kiuchumi.


Zipo dalili nyingi zinazoonyesha kwamba kuna uwezekano mkubwa nchi yetu ikakumbwa na janga kubwa la njaa mwakani. Kinachoendelea hivi sasa ni wakulima katika mikoa inayolima mazao ya chakula kwa wingi kukata tamaa kutokana na mazao yao kukosa soko, huku wakulima hao wakijikuta katika ufukara wa kutisha kutokana na kuwekeza fedha zao katika kilimo cha mazao hayo, lakini Serikali imeshindwa kuwatafutia masoko.
Hapa hatuzungumzii mazao ya biashara kama korosho, tumbaku, kahawa na pamba ambayo kwa muda mrefu sasa yamegeuka kuwa laana kwa wakulima kutokana na viongozi wa vyama vya ushirika nchi nzima kuvigeuza vyama hivyo kama mitaji binafsi ya kujitajirisha wakishirikiana na baadhi ya viongozi serikalini.
Kwa miongo minne sasa wakulima hao hawana sauti wala mtetezi. Serikali ingetarajiwa kuvikwamua vyama hivyo, ambavyo vilianzishwa na wakulima wenyewe na kuwa nguzo yao kubwa kiuchumi. Hata hivyo, hakuna asiyejua kwamba Serikali kwa kuogopa nguvu ya vyama hivyo, iliingilia kati na kuvisambaratisha kwa kupandikiza uongozi uliowekwa mfukoni na wanasiasa.
Hapa tunazungumzia wakulima wa mazao ya chakula, hasa mahindi yanayolimwa kwa wingi katika mikoa ya Mbeya, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Iringa na Morogoro inayojulikana kama ‘Kapu la Chakula’. Hivi sasa wakulima wa zao hilo wamekata tamaa kutokana na kukosa soko la zao hilo, hivyo hawaoni tena sababu ya kuwekeza katika kilimo hicho kutokana na hasara waliyoipata msimu uliopita, ambao walikopa fedha kuandaa mashamba na kununua pembejeo na kufanikiwa kuvuna kiasi kikubwa cha mahindi. Wakulima walihamasika kutokana na Rais Jakaya Kikwete kutangaza bei mpya ya mahindi kutoka Sh350 hadi Sh500 alipokuwa katika ziara ya mkoani Ruvuma mwaka uliopita.
Matokeo yake ni kwamba mahindi yanaozea katika makazi ya watu, maghala ya vyama vya ushirika, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NRFA) na wafanyabiashara binafsi. Wakulima wamebaki wakiwa midomo wazi, wakisubiri kuona miujiza ya mahindi yao kupata soko ili wajikwamue katika ufukara na umaskini uliopitiliza. Takwimu zinaonyesha kwamba mikoa hiyo imezalisha tani milioni 16 za mahindi, huku Mkoa wa Rukwa pekee ukizalisha tani milioni nne.
Hata hivyo, wakulima wamekwazwa na kodi nyingi wanazotozwa kwa kila gunia inapotokea wakauza sehemu ya mahindi yao yaliyolundikana. Malipo hayo ni kama kodi ya halmashauri, gharama za kuhifadhi mahindi ghalani, ubebaji wakati wa kushusha mahindi kituoni, kuchekecha mahindi, kuondoa uchafu na kupeleka kwenye mizani.
Kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo ambayo inatoa ajira kwa zaidi ya asilimia 80 ya wananchi, tungetarajia Serikali iwekeze nguvu na rasilimali zake kwenye kilimo. Mipango ya Kilimo Kwanza na Matokeo Makubwa Sasa imeonekana kuwa ni nadharia zaidi kuliko utekelezaji. Ni kutokana na hali hiyo tunaishauri Serikali iwekeze kwa wakulima badala ya kuwekeza kwenye siasa. Siyo siri kuwa, iwapo fedha inazotumia katika mambo ya kisiasa zingeelekezwa kwenye kilimo, wakulima wangejikomboa kiuchumi.
Ni wakati wa Serikali sasa kufikiri nje ya kisanduku kwa kuwatafutia wakulima masoko ya uhakika kwa mazao yao, yakiwamo matunda kama nyanya, maembe, machungwa na nanasi yanayoozea mashambani kwa kukosa viwanda vya kusindika. Kipaumbele kiwekwe kwa wakulima na Serikali itambue kwamba wananchi hawawezi kupata shibe kutokana na siasa.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • MAREKANI YAITUPIA LAWAMA KOREA KASKAZINI
    Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala ...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • Burkina Faso leaders agree transitional framework following the meeting held in Ouagadougou
      The blueprint for transition was agreed unanimously at the meeting in Ouagadougou A framework for a transitional government ...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis