Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Entertainment → Kiungo mpya wa Azam, Amri Kiemba akiwa katika jezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam jana

Kiungo mpya wa Azam, Amri Kiemba akiwa katika jezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam jana

Entertainment
Tuesday, 25 November 2014


 

 Klabu ya Yanga imemleta nchini kwa majaribio mshambuliaji raia wa Zambia, Jonas Sakuwaha anayeichezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Sakuwaha (31), pia amewahi kucheza soka katika klabu ya Zesco United (Zambia), Lorient (Ufaransa), Le Havre (Ufaransa) na El-Merreikh (Sudan).
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa Yanga, kama Sakuwaha atafuzu majaribio, basi atachukua nafasi ya Hamis Kiiza raia wa Uganda katika orodha ya wachezaji wake watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mbali na Kiiza, Haruna Niyonzima yuko hatarini kuiacha Yanga na tayari Azam FC imemkaribisha kundini ikijinasibu kuwa raia huyo wa Rwanda ni mchezaji wao.
Azam wamekuwa wakidai kuwa walikuwa wa kwanza kumsajili Niyonzima kabla ya kutua Yanga, lakini aliyekuwa kocha wao, Stewart Hall alimkataa kwa kigezo cha ufupi, ndipo walipomshauri ajiunge na Yanga.
Yanga tayari inao wachezaji watano wa kigeni ambao ni, Mbuyu Twite, Andrey Coutinho, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima na Mbrazili mpya, Emerson de Oliveira Neves Rouqe, anayetarajiwa kuwasili nchini kesho kuziba nafasi ya Mbrazili Genilson Santos ‘Jaja’.
Kuwasili kwa Sakuwaha aliyeichezea Zambia michuano mbalimbali ya kimataifa na pengine ujio wa Emerson ni mabadiliko yanayolenga kuimarisha mfumo wa uchezaji Yanga.
Hata hivyo, hilo litategemea kuondoka kwa Kiiza na Niyonzima, ambao wameonyesha nia ya kutotaka kubakia kwenye klabu hiyo.
Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kuwa Sakuwaha atawasili nchini akifuatana na wachezaji wengine wanne kutoka Zambia kwa ajili ya majaribio.
Jana kulikuwa na habari kuwa mshambuliaji chipukizi wa Uganda, Yunus Sentamu anayeichezea AS Vita ya DRC, naye atatua Yanga.
Katika hatua nyingine, Emerson de Oliveira Neves Rouqe anatarajiwa kuwasili nchini kesho saa 7.00 mchana kwa ajili ya majaribio.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Takribani watu 15 wapata upofu baada ya upasuaji nchini India
    Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji walisema walishindwa kuona tena baada ya kuondoa bandeji kwenye macho yao Maafisa wa utawala nchini Indiaa w...
  • Familia ya mateka yasihi Al Qaeda kumwachilia
    Marekani imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen. ...
  • Ona kilichotokea kwa jimama hili kipindi lina jaribu kucheza jirani na swimming pool.Noii huko Kenya mida ya jana jioni
       
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.
      OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semi...
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL
  • KAULI YA UHURU KWENYE MTANDAOWA KIJAMII (TWITTER) KENYATTA HII HAPA
    Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto. Baadhi w...
  • Maandano zidi ya kutupiliwa mbali kwa kesi ya afisa polisi mjini New York
    Maandamano mjini New York Waandamanaji wameingia katika barabara za miji mingi Nchini Marekani kwa usiku wa pili mtawalia, kupinga maamu...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • MORE THAN 10,000 GRADUATES TURN UP FOR SEVENTY JOB VACANCIES IN DAR ES SLAAM.
    According to the list of names seen by The Guardian yesterday morning, the department listed 10,816 candidates to perform the interview tha...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis