Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → Mapya ya Dk.Slaa kuhusu IPTL

Mapya ya Dk.Slaa kuhusu IPTL

Habari
Friday, 5 December 2014





KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, amesema fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow ni sh bilion 400 badala sh bilioni 306 kama ilivyokaririwa na vyombo vya habari kutoka bungeni.
Hayo aliyabainisha juzi na Katibu Mkuu huyo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali  za Mitaa uliofanyika katika mtaa wa Mnazi mmoja Manzese, Tip top jijini Dar es Salaam.
Dk. Slaa alisema kutokana na tuhuma hizo, alifuatilia bunge hatua kwa hatua hadi likaisha kwa maridhiano, akiamini wezi wa fedha hizo watachukuliwa hatua lakini cha kushangaza hadi leo hawajachukuliwa hatua nab ado wanaendelea na kazi.
“Fedha alizochukua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ni ukweli uliowazi kuwa Rais Jakaya Kikwete anajua na ndio maana mawaziri hao wamekuwa na jeuri.
“Suala la Escrow ni bichi kuliko mnavyofikiria, lugha ya Mwalimu Nyerere aliposema watu wanaokimbilia Ikulu tuwaogope kama ukoma, Ikulu ni mahali patakatifu mahali pa heshima kumbe wakubwa walijua kuna nini? Atoke Kikwete hadharani kama nasema uongo,” alisema.
Alisema hajawahi kuona Waziri dhaifu kama Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwani kama angekuwa makini, angeweza kuzuia wizi huo usitokee.
“Mfumo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mbovu kuanzia Kikwete mwenyewe na serikali za mitaa hata wabadilishwe viongozi katika chama hicho bado hakutakuwa na mabadiliko ya kimaendeleo nchini,” alisema Dk. Slaa.
Naye Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe alisema kuwa nguvu ya CHADEMA ya kusimamisha wagombea katika mitaa na vitongoji kwa asilimia 98 katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini imewatia hofu CCM.
Mbowe, alisema  baada ya kubaini mbinu chafu za chama hicho, kuwawekea wagombea wa CHADEMA pingamizi huku wengine wakienguliwa kimizengwe ni dalili ya wazi kwamba chama hicho kinahofu ya kushindwa.
“Presha hiyo inawafanya wawaengue wagombea wetu kwa kuwajengea hoja zisizo na msingi mara utasikia jina limekosewa mara sijui jina la chama liko hivi ili mradi tu wakipunguze nguvu chama chetu.
“Nawaomba wakazi wa Vijibweni ikifika Desemba 14 siku ambayo itakuwa ya uchaguzi, mjitokeze kwa wingi kama mlivyojitokeza leo ili mkawapigie kura wagombea wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),” alisema Mbowe.
Mbowe, alisema CHADEMA haitaki ushindi wa dezo bali wanataka uchaguzi huru na wa haki ili mshindi atakayepatikana, ashinde kwa haki.
Aidha, CHADEMA imetahadharisha kuwa endapo vurugu za kuwaengua wagombea wake zitaendelea, chama hicho kitakwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi huo.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, Issaya Mwita, awali akitoa taarifa ya mchakato wa uchaguzi huo alisema katika Kata hiyo ya Vijibweni kuna mitaa sita.
Alisema katika mitaa hiyo, Chama Cha Wananchi (CUF), kimesimamisha wagombea wawili huku CHADEMA kikisimamisha wanne.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Takribani watu 15 wapata upofu baada ya upasuaji nchini India
    Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji walisema walishindwa kuona tena baada ya kuondoa bandeji kwenye macho yao Maafisa wa utawala nchini Indiaa w...
  • Familia ya mateka yasihi Al Qaeda kumwachilia
    Marekani imeeleza kuwa ilijaribu kumwokoa raia wake mzaliwa wa Uingereza Luke Somers, anayeshikiliwa mateka na al-Qaeda nchini Yemen. ...
  • Ona kilichotokea kwa jimama hili kipindi lina jaribu kucheza jirani na swimming pool.Noii huko Kenya mida ya jana jioni
       
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL
  • KAULI YA UHURU KWENYE MTANDAOWA KIJAMII (TWITTER) KENYATTA HII HAPA
    Taarifa ya mahakama ya ICC, kutupilia mbali kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta, imepokelwa na watu wengi nchini Kenya kwa hisia mseto. Baadhi w...
  • Maandano zidi ya kutupiliwa mbali kwa kesi ya afisa polisi mjini New York
    Maandamano mjini New York Waandamanaji wameingia katika barabara za miji mingi Nchini Marekani kwa usiku wa pili mtawalia, kupinga maamu...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • MORE THAN 10,000 GRADUATES TURN UP FOR SEVENTY JOB VACANCIES IN DAR ES SLAAM.
    According to the list of names seen by The Guardian yesterday morning, the department listed 10,816 candidates to perform the interview tha...
  • Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala amenukuliwa akisema "Nataka kuwa Waziri mkuu''
    Mshindi wa Nishani ya Nobel bint Malala Yousafzai raia wa Pakistani amesema kuwa siku zijazo anatarajia kuwa mwanasiasa. Malala a...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis