Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Habari → Majonzi → HILI NDILO BALAA LA MAFURIKO YALIYOTOKEA HUKO MWANZA

HILI NDILO BALAA LA MAFURIKO YALIYOTOKEA HUKO MWANZA

Habari, Majonzi
Friday, 5 December 2014

Kivuko asilia ni ajira kwa wengine.

Wanajeshi wa Kikosi cha zimamoto Mwanza wakimvusha mama huyu kutoka juu ya paa la nyumba moja hadi upande wa pili penye usalama kupisha maji yaliyokuwa yamefurika hata kuzifunika nyumba za wananchi eneo la Mabatini jijini Mwanza. 

MVUA kubwa iliyonyeesha juzi (jumanne) asubuhi imeleta mafuriko katika maeneo mbalimbali Jijini Mwanza  huku eneo la mabatini likiathirika zaidi na mafuriko hayo yaliyoambatana na mvua kubwa iliyonyeesha takribani  kwa muda usipoungua  masaa mawili.

Mafuriko hayo yalisababisha maji kujaa katika nyumba za wakazi wa maeneo ya mabatini,pia mafuriko hayo yalisababisha magari kutopita eneo la daraja la mabatini linalotumiwa na waenda kwa miguu baada ya maji hayo ya mafuriko kuigawa barabara ya mabatini hali iliyosababisha kukatika kwa mawasiliano.

Juhudi za jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao walifika mapema eneo la tukio zilisaidia kuokoa baadhi ya wakazi wa nyumba zilizokumbwa na mafuriko yaliyosababisha nyumba hizo kujaa maji ndani.
Katika zoezi hilo la uokoaji watu mbalimbali waliokolewa wakiwepo watoto wadogo na akina mama huku mali mbalimbali zikiwemo runinga,vitanda,magari yakisombwa na mafuriko hayo.
Akizungumzia tathimini ya zoezi nzima la uokoaji Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Jijini Mwanza,Andrew James Mbate amesema zoezi la uokoaji lilienda vizuri na walifanikiwa kuokoa maisha ya watu waliokowepo ndani ya nyumba huku akitanabaisha changamoto mbalimbali walizokutana nazo katika zoezi zima. 
“Zoezi la uokoaji lilienda limeenda salama na linaendelea vizuri tunashukuru wenzetu wa shirika la umeme waliwahi kukata umeme mapema hali iliyopelekea sisi kama Jeshi kuanza kazi mara moja tulivyofika eneo la tukio”. Aliongeza Gadafi ambaye ni msemaji wa jeshi la Zimamoto

Akizungumza juu ya mafuriko hayo mkazi wa mabatini,Charles Samson alisema wamepoteza vitu vyao vya thamani huku wakioomba serikali iwasaidie kuhama mabondeni kwani madhara yaliyowakuta ni makubwa.

Tanesco walizima umeme kwaajili ya tahadhali.




Gari hili nyang'anyang'a mara baada ya kusombwa na mafuriko na kubinuliwa kisha kutoswa mtaroni. 
Msaada tutani.
Eneo la mabatini ni eneo ambalo mto mirongo unapita hali iliyosababisha mafuriko hayo kuwa makubwa kwa kuwa maji yam to huo yanatoka sehemu mbalimbali za wilaya zilizopo Mkoani Mwanza ikiwemo wilaya ya magu.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • Catalonia's regional president Artur Mas says an official referendum is needed following Catalonia vote: 80% back independence - officials
    \ An informal vote on independence for Catalonia has shown more than 80% in favour, officials say. The non-binding vote went ahead after ...
  • After more than two years of tension over a territorial row,the leaders of China and Japan hold formal talks on the sidelines of a major Asian summit.
    Chinese President Xi Jinping and Japanese PM Shinzo Abe met on the sidelines of the Asia-Pacific Economic Co-operation (Apec) summit in B...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...
  • Report says,Fossil fuel promises are being broken,World governments have been breaking promises to phase out subsidies for fossil fuels, a report says.
    The report said G20 nations had been spending almost $90bn a year on finding more oil, g...
  • Burkina Faso leaders agree transitional framework following the meeting held in Ouagadougou
      The blueprint for transition was agreed unanimously at the meeting in Ouagadougou A framework for a transitional government ...
  • Mamboya whatsapp haya hapa.!!!!! (18+)
  • John Doar, a civil rights lawyer who was a key figure in the struggle against racial segregation in the US, has died aged 92.
    John Doar was awarded the Presidential Medal of Freedom in 2012 Mr Doar dealt with some of the most prominent civil rights ca...
  • Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.
      OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semi...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis