Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Tanpa Kategori → MWISHO WA MWAKA ROHO MKONONI MABASI YATEKWA, WANAWAKE WABAKWA

MWISHO WA MWAKA ROHO MKONONI MABASI YATEKWA, WANAWAKE WABAKWA

Wednesday, 17 December 2014
Jumla ya magari saba yakiwemo mabasi mawili yaliyokuwa yakitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanza, yametekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia Jumamosi ya wiki iliyopita, saa 6:30 usiku eneo la Ng’ungumalwa mkoani Mwanza.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
Miongoni mwa magari yaliyotekwa, mawili yalikuwa ni mabasi ya abiria, Super Najmnisa na Princess Mnaa huku mengine yakiwa ni malori na gari dogo moja ambapo inaelezwa kuwa watekaji walitegesha mawe makubwa barabarani kabla ya kutekeleza tukio hilo.
Wakizungumza na mwandishi wetu aliyekuwepo eneo la tukio, baadhi ya madereva wa magari yaliyotekwa walieleza kwamba walipofika eneo hilo, walikuta mawe yakiwa yametegeshwa barabarani huku kukiwa na kundi la watu wenye silaha za aina mbalimbali yakiwemo mapanga, marungu na bunduki.

Baadhi ya abiria waliotekwa.
“Walitushusha kwenye magari na kututaka tusalimishe kila kitu tulichokuwa nacho zikiwemo fedha na simu za mkononi. Waliokuwa wakionesha ukaidi walikuwa wakipigwa na kujeruhiwa vibaya,” alisema dereva mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Madereva hao waliendelea kueleza kuwa kazi hiyo ya utekaji iliendelea kwa takribani saa nzima ambapo kila gari lililokuwa likija eneo hilo, lilikuwa likitekwa na watu kulazimishwa kushuka chini na kutoa kila walichokuwa nacho.

Msichana huyu alizimia baada ya kutekwa.
“Walikuwa na mifuko mikubwa miwili, mmoja ulijaa simu walizotupora na mwingine ulijaa fedha, kwa kweli lilikuwa ni tukio baya sana, wengi walijeruhiwa vibaya,” alisema dereva mwingine ambaye naye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
Abiria wengine waliozungumza na Uwazi, walienda mbele zaidi kwa kueleza kuwa mbali na kupigwa na kuporwa, pia baadhi ya abiria wanawake walibakwa na kusababishiwa maumivu makali.
“Huu unyama tuliyofanyiwa wa kupigwa na kuporwa mali zetu huku baadhi yetu wakibakwa unatisha sana na unaonesha ni kwa jinsi gani nchi inaelekea kubaya, hakuna amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya,” alisema mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa waliotekwa, aliyejitambulisha kwa jina moja la Sara.

...Abiria wakiwa wameduwaa
Abiria hao waliliambia Uwazi kwamba eneo hilo lina pori kubwa ambapo panahitajika doria za mara kwa mara za polisi kwani ni eneo ambalo limekuwa maficho ya majambazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alipopigiwa simu na kuulizwa juu ya tukio hilo, alikiri kuwa na taarifa na kueleza kuwa polisi walifika katika eneo la tukio muda mfupi baadaye baada ya kupata taarifa na kufungua barabara iliyokuwa imefungwa na kuruhusu magari kupita.“Msako mkali unaendelea kuwatafuta watuhumiwa katika Wilaya ya Kishapu na Kwimba,” alisema Kamanda Mlowola.

Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • MAREKANI YAITUPIA LAWAMA KOREA KASKAZINI
    Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala ...
  • Mombasa based singer akothee gets naughty,Angalia hapa
  • Vita dhidi ya Ukimwi zashika kasi, mbinu madhubuti zachukuliwa !
    DESEMBA mosi, kila mwaka, watu wote duniani huadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani. Siku hiyo ilianzishwa mwaka 1987 na hubeba maudhui mbalim...
  • ,Juncker reveals giant EU investment planJuncker said Europe needed a kick-start and the Commission was offering the jump-leads
    Mr  European Commission President Jean-Claude Juncker has given details of a €315bn (£250bn;$393bn) investment plan to kic...
  • Kwaninii serikali imewekeza katika siasa na imesahau wakulima ?
      Hata hivyo, wakulima wamekwazwa na kodi nyingi wanazotozwa kwa kila gunia inapotokea wakauza sehemu ya ...
  • Mdogo wa Zari Hassan apaka matope uhusiano wake na Diamond
    Mdogo wake na Zari Hassan aka The Bosslady, aitwaye Karim ametumia Facebook kumkosoa dada yake kwa kuwa na uhusiano na Diamond Platnumz amb...
  • DAVIDO,TIWA SWAGE,DIAMOND, MR.FLAVOUR ON THE SHOOT,CHECK THE NEW VIDEO HERE
    Africa MultiChoice has launched it’s biggest  campaign yet, to celebrate Africa’s positivity , successes and the ability to  te...
  • Wayne Goss, former premier of Queensland, kicked the bucket at 63
    Mr Goss, who was premier from 1989 to 1996, had suffered from ill health in recent years including brain tumours. He became Q...
  • Third death confirmed in Mali The Pasteur Clinic in Bamako has been placed in quarantine and is under armed guard
      A nurse and the patient he was treating have become the second and third people to die from Ebola in Mali. The patient,...
  • The poorest president, Jose Mujica gets $1m offer for his VW Beetle
    7 November 2014 Last updated at 07:04 GMT Uruguay's President Jose Mujica says he has been offered $1m (£630,000) for his vinta...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis