Mwanafalsafa

  • HOME
Home → Breaking News → TOKA DIAMOND AANZE MUZIKI HAPA NDIPO ALIPOFIKIA

TOKA DIAMOND AANZE MUZIKI HAPA NDIPO ALIPOFIKIA

Breaking News
Monday, 15 December 2014









WIKI iliyopita katika simulizi hii ya Diamond  tuliishia pale ambapo staa huyo aliongelea namna wimbo wake wa Mbagala ulivyopendwa kiasi cha kumfanya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ‘JK’ kumteua kuwa mburudishaji kwenye ziara za kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, mwaka 2010.Wiki hii tunaendelea…

Mkali wa Bongo fleva Nasib Abdul Diamond Platinumz.  Oktoba 2, mwaka 2010, Diamond alipata safari yake ya kwanza kabisa ambapo alikwenda jijini London, Uingereza na kufanya shoo.Mwaka 2011, Diamond alishinda Tuzo ya
 Nzumari iliyotolea nchini Kenya akiwa Msanii Bora wa Kiume toka Tanzania.
Diamond aliweka rekodi ya msanii wa kwanza Bongo kufanya shoo kwenye Ukumbi wa Maisha Club jijini Dar na kujaza mashabiki wengi kiasi kwamba wengine walishindwa kuingia ndani ya ukumbi huo.
 AACHIA ALBAMU YA PILI
Ilikuwa Januari, 2012 Platnumz aliachia albamu yake ya pili  na kufikia rekodi ya kuwa msanii nambari wani Bongo kuuza kopi zaidi ya 1,200,000.
 Mwaka huohuo,  Diamond alifanya shoo bab’kubwa iliyoitwa Diamonds are forever iliyofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kwa kiinglio  cha shilingi 50,000. Diamond alikuwa peke yake na aliuza tiketi  zaidi 1,500.
 MSANII WA KWANZA BONGO KUSHUKA UWANJANI NA CHOPA
Mei, 2012, Diamond aliweka rekodi ya kuwa msanii wa kwanza kufanya shoo ya nguvu na kujaza zaidi ya watu 10,000 kwa kiingilio cha 20,000 ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live  huku akishuka uwanjani hapo na chopa (helikopta). Hata hivyo, Desemba 25, mwaka huu (Krismasi), Diamond atakuwepo tena ndani ya Dar Live!
 AENDA ULAYA, AKAMUA
Mwaka huohuo 2012,  Diamond alifanya
ziara Ulaya ambapo alitembelea nchi kadhaa kama Italia, Uholanzi, Sweden na Ugiriki, nako alifanya shoo za nguvu.
 Nyota ya 2012 ilizidi kuwa nzuri kwa Diamond kwani aliachia nyimbo mbili kwa mpigo, Nataka Kulewa na Kesho zilizoambata na video zake zenye ubora.
 AWA BALOZI
Mwanzoni mwa mwaka 2013, Diamond alichaguliwa kuwa balozi wa kampuni moja ya vinywaji baridi nchini na  kufanya ziara nchi za Afrika Mashariki, Burundi, DRC, Kenya, Uganda na Rwanda na kuwa msanii wa kwanza katika nchi za ukanda huo kupiga shoo peke yake kwenye uwanja na kujaza zaidi ya watu 30,000.
 ASHINDA TUZO TENA

June 2013, Diamond alishinda tuzo mbili  za Tanzania Kili
 Music Awards akiwa Msanii Bora wa Kiume wa Bongo Fleva
 na Msanii Bora  wa Kiume kwa wanamuziki wote nchini.
 NUMBER ONE

Julai 2013, Diamond  aliachia singo ya Number One ambayo 

video yake aliifanyia jijini Capetown, Afrika Kusini na 

Kampuni ya Ogopa Video. Aliweka rekodi ya kuwa msanii wa
 kwanza kuzindua video hiyo bila kiingilio ndani ya Hotel ya Serena na kuwaalika viongozi mbalimbali.
 Katika uzinduzi huo, Diamond alifanya tukio la kihistoria ambapo alimzawadia gari aina ya Totoya FunCargo aliyekuwa mwanamuziki nguli nchini, marehemu Muhidin Maalim Gurumo. 
Itaendelea wiki ijayo.







Share this article :
Tweet
✚
Newer Post
Older Post
Home

HABARI ZILIZO BAMBA TOP 10

  • Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste
    Lorna Rutto is an entrepreneur who founded Ecopost, a Nairobi-based company that recycles plastic waste. As part of the latest series o...
  • Wabunge wa Somali wameng'oa waziri mkuu
    Ni mara ya nne kwamba kura ya kutokuwa na imani dhidi yake ilipigwa baada ya majaribio ya awali kumalizika kwa ghasia. Waandishi ...
  • AJIITA KIJANA MWENYE BAHATI AKIWA KATIKATI YA WAREMBO WAWILI
  • John Doar, a civil rights lawyer who was a key figure in the struggle against racial segregation in the US, has died aged 92.
    John Doar was awarded the Presidential Medal of Freedom in 2012 Mr Doar dealt with some of the most prominent civil rights ca...
  • Ukweli kuhusu umoja wa fedha,Jumuiya ya Afrika Mashariki.
      OKTOBA 20 hadi 24 mwaka  huu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliandaa semi...
  • BRAZIL TO EDGE OUT GERMANY IN WORLD CUP SEMI FINAL
  • Chuo kikuu cha ardhi ARU chatoa zawadi kwa wanafunzi 30, mmoja, ambae ni muhitimu wa masomo ya surveying aibuka na machine ya millioni 35
    CHUO Kikuu Ardhi (ARU), kimewazawadia wanafuzi 130 wa masomo mbalimbali zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 60 kutokana n...
  • Ajali ya gari huko south B kenya
    There was a bizarre accident today morning in Hazina Estate, South B involving a Range Rover that crashed into 7 vehicles. The Ran...
  • Jennifer Lawrence has joined her castmates at the world premiere of the penultimate Hunger Games movie, Mockingjay Part 1, in London.
    Lawrence plays the heroine Katniss Everdeen in the hit franchise Jennifer Lawrence has joined her castmates at the w...
  • Arsenal yamlenga Kramer anaechezea klabu ya Borussia Monchengladbach
    Arsenal wako tayari kutoa p...

LABELS

  • Breaking News
  • condolonces
  • Entertainment
  • Entertainments
  • Habari
  • Majonzi
  • Michezo
  • News
  • News and Updates
  • Skendo
  • Sports and Games
Submit ExpressSEO Services & Tools

Total Pageviews

Copyright 2014 Mwanafalsafa
Template By Ridwan Hex And Game Gratis