Wakati dunia ilipoadhimisha siku ya Walemavu Duniani wiki hii, kilichozua mjadala nchini Kenya ni iwapo ni haki kwa mzazi au mfadhili wa mtoto mwenye akili taahira kumfungza kizazi ili asiweze kuzaa kabisa.
Ingawa kuna wale wanaosema kwamba ni haki ya kimsingi kwa mtu mwenye akili taahira kufurahia tendo la ngono na hata kuzaa kuna wengine wanaosema kuwa kwa kuwa wao hawawezi kujitunza wenyewe wala hawana ufahamu wa kuamua kilicho bora kwao wasiruhusiwe kujitwika mzigo wa ziada.
Mwandishi wa BBC Muliro Telewa aLIsafiri hadi Magharibi mwa Kenya kujionea hali inayowakumba wasichana wengi wenye akili taahira.
Katika kituo cha Kona mbaya katika eneo la Likuyani, Kaunti ya Kakamega, nilimpata mwanamke mwenye akilia taahira, mwenye umri wa miaka thelathini nilipoingia katika nyumba yake ya vyumba viwili.
Alikuwa ameketi kwenye kiti kirefu akiwa amebanwa kwa upande mmoja na mama yake mzazi, mwenye umri wa miaka 83 na upande mwingine na dada yake mwenye umri wa miaka 40, Annet Nekesa Ngosia.
Mwanamke huyo alitutizama kwa hofu na kuchanganyikiwa usoni mwake.
Hata hivyo dada yake Nekesa, alimwagiza atabasamu kidogo kwa kuwa sisi ni wapiga picha. Alitabasamu kwa muda mfupi tu lakini baada ya dakika moja uso wake ukarejelea picha ya awali. Dada yake Annet Nekesa Ngosia aliendelea kuelezea.
''Ikiwa yeye mwenyewe hawezi kujitunza, atatuza vipi mtoto wake bila kusaidiwa? watu kama hawa wanapaswa kufungwa kizazi. Iangwa anelewa ni kinyume na mafunzo ya biblia, uhalisia wa maisha ya sasa ndio unatuongoza. Mimi siwezi hata kufikia kuhusu kufungwa kizazi na pia ni vigumu kuwaelewa watu hawa labda na wao wana hisia na wangetaka k
upata watoto na hata kuwa na familia, ''anasema Nekesa.
Mwanamke huyo mwenye akili taahira alikuwa amevalia rinda la bluu lililokuwa limefungiwa kifuani mwake kwa uzi.
Nilipomtizama usoni alionekana kama anayefuatilia tunayozungumza na kwa hivyo nikamwuliza iwapo anamjua mtoto wake akawa hana habari kulihusu hilo.
Alinielekeza kwa mkono wake alikokuwa msichana mrembo aliyekuwa ametoboa masikio yake yaliyokuwa hayajapona vizuri.
Anapofanya hivyo anatabasamu kidogo. Msichana huyo anasongea karibu nami ninapomwelekeza kufanya hivyo. Ananiambia jina lake na kunielezea zaidi.Nilipomuuliza ikiwa anamfahamu mtoto wake, alitabasamu tu.
Na mwendo wa kilomita 10 hivi kutoka aliko mama huyu, katika Kituo cha Biashara cha Moi’s Bridge, nilikutana na Bwana Daniel Mutimba, aliye na mtoto mvulana mwenye umri wa miaka 10 mwenye akili taahira.
Msimamo wake juu ya kuwafunga kizazi watoto wa aina hiyo unahitilafiana na ule wa Nekesa.
Dakitari bingwa wa maradhi ya akili katika hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi, mjini Eldoret, Edith Kwoba, alisema kuwa utafiti uliofanywa nchini Kenya unathibitisha kuwa asilimia 25 ya watu milioni 40 walioko nchini Kenya wana maradhiya akili ingawa wengi wao hawayajui.
Anaunga mkono kuwasimamisha uzazi wagonjwa wa akili:
Lakini Mkereketwa na mwalimu wa watoto wenye akili taahira, Mwaliumu Mkuu wa shule ya mtakatifu Vincent De Paul katika eneo la Likuyani, kaunti ya Kakamega, Bwna Konyango John Paul, anasema haki za kimsingi za watoto wenye akili taahira lazima zilindwe:
Sheria nchini Kenya hazielezi kikamilifu iwapo wagonjwa wanapaswa kukatizwa uzazi. Kwa sasa kuna kundi la kina mama walio na virusi vya HIV ambao wamefika mahakamani kuwashtaki baadhi ya madaktari kwa kuwafunga kizazi bila kuwafahamisha miaka ya 80.
Huku mjadala huo ukiendelea miongoni mwa wanaohusiana na wagonjwa wa akili taahira, msichana mwenye umri wa miaka 11 yungali anasubiri mama yake apone, huku yeye akizidi kufanya kazi badala ya kucheza kama watoto wenzake.