Ligi
ya kuu ya England iliendelea jana usiku katika viwanja mbali mbali.
Leicester inayoburuza mkia katika ligi hiyo ikiwa na pointi 10 katika
michezo 14 iliyocheza waliikaribisha Liverpool ambayo iliibuka na u
shindi
wa magoli 3-1 katika mechi hiyo. Hadi kumalizikakwa kipindi cha kwanza
timu hizo zilikuwa zimefungana goli 1-1. Kwa matokeo hayo Liverpool
imeshika nafasi ya 8 nyuma ya Asernal , zote zikiwa na pointi 20. Hata
hivyo Asernal imecheza mchezo mmoja pungufu ya Liverpool yenye mechi 14
ilizokwishacheza.
Matokeo mengine katika mechi za Jumanne usiku,
Manchester United wakiwa kwenye uwanja wao wa Old Trafford, wameicharaza
Stoke City mabao 2-1. Burnley imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na
Newcastle, Swansea wameitandika QPR magoli 2-0, Crystal Palace
wamepoteza katika uwanja wao kwa kucharazwa goli 1-0 na Aston Villa.
Nayo West Brom imepoteza kwa kufungwa 2-1 na West Ham.
Katika
mechi za leo usiku, Arsenal watapepetana na Southampton katika uwanja wa
Emirates, Chelsea vinara wa ligi watakuwa wenyeji wa Tottenham, huku
Everton wakiikaribisha Hull City. Na Machester City inayoshika nafasi ya
pili kwa kujikusanyia pointi 27 watataka kujiimarisha na kupunguza
pengo la pointi sita kati yake na Chelsea, pale watakapomenyana na
wenyeji wao Sunderland.