Shughuli
za mazishi ya mtoto wa miaka miwili zimefanyika nchini Uganda, mtoto
ambaye kifo chake kimezua ghadhabu baada ya mtoto huyo kugongwa na gari
la halmashauri ya jiji la Kampala ,baada ya mama yake kukamatwa akiuza
matunda kinyume cha sheria.
Familia ya Ryan Ssemaganda na
wanasiasa wa upinzani walitishia kutomzika mtoto huyo mpaka maofisa hao
watakapo wajibika kwa kitendo hicho.Mwili wake ulichukuliwa wakati
wakiandamana kuelekea bungeni siku ya alhamisi.
Raia wa Uganda wanaona kuwa halmashauri hiyo inatumia nguvu nyingi kupambana na wachuuzi wa mitaani.
Mama wa mtoto Ryan alikamatwa siku ya jumatatu baada ya kukutwa akiuza matunda huku akiwa hana leseni.
Siku
iliyofuata, Bibi wa mtoto huyo alimpeleka katika Ofisi za Mamlaka ya
mji wa Kampala ambako mama mtoto alikuwa akishiliwa , nia ilikua kumpa
mama mtoto ili amnyonyeshe.
Maafisa wa Ofisi hiyo walikataa na
wakati wakijadiliana kuhusu hilo, mtoto alichoropoka kutoka kwa mama
yake na kugongwa na gari linalomilikiwa na Mamlaka hiyo.
Siku ya
Alhamisi polisi ilizuia kupelekwa kwa mwili katika Bunge, wakisisitiza
mwili huo uzikwe ili marehemu apumzike kwa amani, na kuwataka waepuka
jambo hilo kushughulikiwa kisiasa.