Kuna kaulimbiu za shule mbalimbali ambazo zimekuwa zikionekana katika nyaraka za shule.
Kwa mfano, unaweza utakutana na misemo kama “Elimu ni Maisha,” “Elimu ni Ufunguo wa Maisha” na nyingine nyingi.
Lengo la misemo hii ni kuonyesha jinsi taasisi husika inavyowaandaa watu wake kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Kwa maana hiyo waandaliwa hao wanatakiwa wawe wakala wazuri wa shule zao uko waendako kwa kufanana na kaulimbiu hizo.
Pamoja na kwamba taasisi hizo huwa na malengo mazuri, suala la utekelezaji wa malengo hayo huwa ni changamoto.
Nasema ni changamoto kwa sababu tunaona jinsi
idadi kubwa ya wahitimu wanaotoka katika taasisi wasivyohusiana na
kaulimbiu za taasisi zao.
Funzo tunalolipata hapa ni kuwa hatuna budi kusimamia na kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu tunazoziamini.
Utekelezaji wake kwa vitendo utazaa matunda
yaliyokusudiwa. Katika elimu ya ujasiriamali, matendo ndicho kitu cha
thamani kubwa kuliko maneno yatokayo katika mdomo wa mtu.
Wataalamu wa elimu ya ujasiriamali kama vile
Garavan na Barra wanasema kuwa madhumuni ye elimu ya ujasiriamali ni
pamoja na kupata maarifa stahiki ya ujasiriamali.
Pia, ni kupata ujuzi utakaosaidia kutumia mbinu
mbalimbali za uchambuzi wa masuala ya biashara. Vilevile ni kubainisha
na kuchochea ujasiriamali.
Madhumuni mengine ni kujenga na kuendeleza mambo
yanayowagusa wajasiriamali ikiwa ni pamoja na kusaidia masuala yote
yanayohusiana na ujasiriamali.
Kama haya yakifanyika katika viwango vyetu vya
elimu itakuwa rahisi kwa Taifa letu kuwa na maendeleo endelevu. Tutakuwa
tumejenga watu wenye maarifa na ujuzi wa kufanya kazi kwa manufaa yao
na taifa lao