Miili ya watu 36 waliouawa mjini Mandera Kaskazini mwa Kenya ilifikishwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City mjini Nairobi Jumatano asubuhi.







Jamaa na marafiki pamoja na familia za watu waliouawa walifika kupokea miili hiyo lakini kilio na simanzi ndivyo vilitanda katika chumba hicho.







Wengi walikosa nguvu ya kuiona mili hiyo iliyofikishwa katika chumba hicho na polisi pamoja na wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu au Red Cross.







Baadhi ya wanafamilia walishindwa cha kusema kwani taarifa hizi ziilikuwa za kutisha mno. Wengi wa waliouawa walikuwa wafanyakazi wa machimbo ya kokoto mjini Mandera, mji uanopakana na mpaka wa Somalia na Kenya







Taarifa za kuuawa kwa watu hao zilitokea Jumanne asubuhi siku kumi baada ya watu wengine 26 kuuawa wakiwa safarini kutoka mjini Mandera kuelekea likizoni. wengi walikuwa wafanyakazi wa serikali, ikiwemo walimu wa shule za msingi







Majonzi tele ndiyo yaliweza kusimulia tu hisiaza wanafamilia wengi waliofika katika chumba cha City asubuhi ya leo.







Serikali ya Kenya ililaani mashambulizi hayo yaliyofanywa na Al Shabaab wakisema wanalipiza kisasi kwa serikali ya Kenya kupeleka wanajeshi wake nchini Somalia. Picha hizi zimepigwa David Wafula