Kama
mwanzo wa makala ya hivi punde ya African Dream,mwanabiashara Mercy
Kitomari-ambaye alianzisha kampuni ya kutengeza aiskrimu hai ya Nelwa's
Gelato-anaeleza mbinu kumi bora anazotumia katika kuuza kwenye mitandao
ya kijamii kwa wanabiashara chipukizi:
Anza na Lengo.
Kwanini uko kwenye mitandao ya kijamii? ana nadi
Kuna
majibu matatu pekee yanayokubalika: a)kuongeza kujulikana kwa bidhaa
zako kwa kufikia watu zaidi b)kujenga imani ya wateja kwa kuwapa
usaidizi zaidi ama c)kuongeza mauzo kwa kutafuta wanunuzi
zaidi,watakaonunua mara kwa kwa mara.Usianze kama huwezi jibu swali
hili.
Wapuuze wapinzani wako-
Kujaribu kuiba wateja wa watu wengine ni mbinu mbovu.Utaanza kuunda maamuzi mabaya kwa sababu unajaribu kuwafikia.
Fikra
na kampeni bora zaidi bado hazijatendeka katika sekta yako.Angalia
nafasi ambazo hazijaguzwa unazoweza kupata na kutumia.Tazama kile watu
wanafanya kwenye sekta tofauti na ujaribu mbinu hizo.
Usiwe kwenye mitandao yote ya kijamii.
Usimamizi
wa kijamii utamaliza rasilmali zako zote.Kila mtandao wa kijamii
unaosimamia utakugharimu muda,pesa na nguvu zaidi,kwa hivyo amua zile
utazipa kipao mbele.
Una pesa na wakati wa kutosha.
Watu
huwa wanasema kuwa hawana muda na pesa za kuwekeza katika mitandao ya
kijamii.Lakini ukweli wa mambo ni kuwa hauwezi kutowekeza.Kama hauna
fedha za kutosha,inafaa uwe na wakati zaidi wa kuunda maudhui ama kuunda
mtandao.
Mercy Kitomari ana mkahawa wa Nelwa's Gelato mjini Dar es Salaam inayosambaza kwenye hoteli na biashara zingine.
Weka lengo rahisi-
Kwa
mfano,kuchapisha mara mbili zaidi kila wiki-ama kufikia bloga mmoja kwa
siku.Pia fanya ukaguzi wa ndani kujua jinsi unavyotumia muda wako kwa
sasa.
Mitandao ya kijamii ni bora,lakini watu wengi huchanganya
kushikika na kazi na kuwa na ufanisi.Tambua shughuli zinazoleta ''mapato
kutoka kwa uwekezaji'' ya juu zaidi,zipe kipao mbele na uweke mipaka.
Kuwa na nidhamu na kuwajibika kwa wengine.
Mwishowe,utahitajika
kuchukua msimamo mgumu.Utahitaji kugawanya rasilmali zako chache na
kuchagua kile utakachofanya (na kile utakachopuuza).Lakini utaona kuwa
uamuzi huu ni rahisi kama una lengo.Matumizi yako ya mitandao ya kijamii
yatakuwa na kusudi.Utapata kuwa una wakati wa kutosha wa kuitumia
kimkakati.
Tambua kile kinachohamasisha wasikilizaji wako.
''Sekta''
ama ''biashara'' hazichoshi-watu wanaosema hayo ndio wanaochosha.Jinsi
unavyojenga mawazo ya maudhui ya blogi ni kuelewa wasikilizaji wako na
faida ambazo bidhaa na huduma zako zinawapa.
Mercy Kitomari anasema kuwa huduma ya wateja ni muhimu sana kwenye mitandao sawia na ya uso kwa uso.
Kuwa na sauti.
Watu
hawapendi kuungana na mashirika yasiyokuwa na uso.Wanataka kuungana na
wanadamu wa kweli.Hakuna atakayiependa,amini ama kuheshimu kampuni yako
ikiwa hawezi kupata majibu yaliyo sawa na yenye uaminifu kwa wakati
ufaao.Mitandao ya kijamii ni zaidi ya ''kujiingiza katika
mazungumzo''.Ni njia mpya ya kufanya mambo,na vifaa kadhaa vipya
kukusaidia kufanya hivo.
Lakini misingi ya njia za mauzo inabakia.Unahitaji kuvutia watu,kujenga imani yao na kuwawezesha kushiriki zaidi.
Tamba sana kupia Facebook na Twitter.
Mitandao
ya kijamii na mauzo kwenye mtandao inaanza na DNA yako,bidhaa ama
huduma zako,na watu wako.Kwa hivyo kama unataka kuimarisha majibu yako
kwenye mitandao ya kijamii,anda na kushughulikia utenda kazi wa ndani wa
kampuni yako.