Mfanyakazi
katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya
kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha
na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi
Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake
wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi
kwenye hafla ya jioni.
Baadaye Lauten alifuta maandiko yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.
Bi
Lauten pia alikuwa amewakosoa Sasha na Malia kwa kusema walionekana
wasio na furaha walipokuwa wamesimama na baba yao katika hafla ya
maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi
kwamba Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla
ile na hata kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi
Lauten aliamua kujitoa kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa
Facebook.
Mwanamke huyo akiomba msamaha,
alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na
kisha kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli
aliwakera wasichana hao.
"ningependa kuomba radhi kwa wote
niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha
mwenendo wangu, '' alisema Lauten.